barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,324
- 29,586
Kumbe usipokaribishwa ikulu ndo ujeuri?? Aendelee tu kuwa jeuri ndugu JPM!Siasa ni dynamic siasa sio static. Siasa ni issues na matukio. Siasa za enzi ya chama kimoja miaka ya 80 ni tofauti na siasa za miaka ya 90 na 2000.
Msingi wa hoja yangu ni kwamba CHADEMA bado inatumia mbinu zile zile walizotumia wakati wa Mkapa na Kikwete kutaka kufanikisha malengo yao dhidi ya utawala wa sasa wa Magufuli.
Siasa za Magufuli zinabebwa na dhana za ubabe na jeuri tofauti na siasa za Kikwete aliyekuwa akiwakaribisha ikulu.
Siasa za leo sio za kistaarabu ni siasa za kejeri, kubeza, siasa za kujitoa ufahamu, hivi unafikiri wanaotukana watu 'wapumbavu' hawajui kuwa wanatukana. Unapotukanwa na kusema hewala namwachia Mungu opponent wako wanakucheka usifikiri watakuonea huruma, unapopigwa na kugeuza shavu la pili basi utaumizwa zaidi.
Leo Lissu kapigwa risasi hadharani no any serious action taken zaidi ya kusikia matamko, kesho atapigwa Lema keshokutwa Mbowe mtakaa kimya.
Katibu mkuu Mashinji angefaa sana siasa za enzi ya Kikwete sio siasa za Magufuli. Siasa za leo zinawafaa watu kama Heche, Lema, Msigwa, Mdee, Bulaya waweke wasemaji wakuu wa chama, watu ambao wakisema Lumumba wanasikia, ikulu inaamuka, mwandishi wa rais anajibu hata ikiwa weekend.
CCM walipoona katibu mkuu wao Mukama haendani na kasi waliyoitegemea alibadilishwa ndani ya miezi sita hawakuwa wajinga.
Ningekuwa mimi Mbowe ningefanya reform kuendana na siasa za wakati huu.
John Heche angechukua nafasi ya Mashinji immediately na Msigwa angekuwa Katibu Mwenezi wa chama. Sio kwamba waliopo hawafanyi kazi bali hawaendani na kasi ya sasa, wanaweza kutumika kwa utawala wa ndani (administration).
Naelewa hoja hujibiwa kwa hoja lakini sometime kwenye siasa vioja ndivyo vinavyosikika zaidi ya hoja yenyewe. Mimi naona nafasi ya uenezi itamfaa sana Msigwa kwa vile kwenye hoja yupo na kwenye vijembe yupo ndiyo siasa.
Nawasilisha.