Kuna haja mafundi ujenzi kuangaliwa upya malipo yao kwa kweli!

Pendaelli

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
8,921
23,251
Salam kwenu wakuu.

Hoja yangu nimeweza kuangalia kazi zifanywazo na mafundi ujenzi,umeme, bomba, seremala nk, Ni kazi zinazodumu walao miaka 25 kwenda juu ndipo ziweze kufanyiwa marekebisho tena kidogo.

Mimi ni shahidi wa hilo, tokea kuanza rasmi kazi za ufundi seremala mwaka 2005, kuna kazi nimezitengeneza mpaka Leo hii sijawahi kuitwa ama imeharibia au kuhitaji marekebisho.

Kwa ufupi malipo niliolipwa hayakunifaa kitu ila huduma nilio itoa mpaka leo ipo na inaweza kuwepo miaka 20 mbele.

Kadhalika mafundi ujenzi na wengineo kazi zao zinadumu na kudumu, na tunafanya kwa moyo ili idumu lakini tumekuwa watu wa kudharauliwa mno na kuonekana si lolote wala chochote linapokuja tathimini ya garama za ujenzi, fundi anakua last kutasminiwa.

Kwa kweli tunatakiwa kufikiriwa upya malipo yetu yanatakiwa kua juu hata Mara mbili ya garama za material.

Nimeleta hoja tuu.
 
Nawakubali sana wazungu..huwa wanaomba likizo kabisa pamoja nafamilia yake wote wanajijengea nyumba zao wenyewe...
Hili linaweza likawa tango pori nusu na robo.
Nikiangalia ile mighorofa ya mjini new york, najiuliza ni likizo ndefu kiasi gani waliomba hawa jamaa hadi kuisimamisha.
 
Pricing zipo za aina mbili tu. Cost based... Na value based. Cost based ni kutoza bei kwa kuzingatia gharama za kukamilisha kazi au kutoa huduma. Hii ni sawa na kununua unga , mafuta, mkaa na maji kwa 10000 kisha unapata maandazi 100 unauza kila andazi 130... Hivyo elfu 3000 ndio ujira wako ukitoa gharama za msingi.

Value based ni bei inapangwa kwa kuzingatia faida utakayoipata. Mfano Mwanasheria, Architect, Engineer na Daktari wanakutoza consultation fee kwa matamanio kwamba ushauri wao utaleta tija. Na sio lazima ulete tija..

Sasa mafundi wangeweza kuangukia kwenye kundi hili la pili changamoto ni kuwa hawako organised na kujifanya high-class wenzako watajenga tofali kwa sh.50. cha kwanza muwe organised na ikibidi certified kujiongezea thamani.

Pili muwe na mitaji. Mainjinia wakati mwingine wanakuwa na uwezo wa kuchip in gharama especially ninapokuwa mbali na kazi haipaswi kusimama. Na utendaji wao ni transparent na unaweza kuwa audited. Hii aspect ya wao kuweza kujiendesha bila supervision na bado ukawa safe wewe mwenyewe jengo na jengo lenyewe inacommand malipo.

Mwisho... Mafundi wengi janja janja.. kazi hawaijui.. na hawapendi kusema hawajui.. wanakuja wanavurunda mwisho wake hasara kwa mwenye jengo kubomoa na kurudia. Hii inachangia watu kuwalipa kidogo km insurance, ukizingua basi nipate hasara ya material tu.. ya fundi nakukata kabisa.

Rekebisheni kwanza ndio tujadili pesa... Haya mapaaa yanaenda km mnara wa Babeli halafu mnataka mlipwe pesa nyingi!? Pesa yenu tumeongezea misumari NONDO na mabati.. :)
 
Nazungumzia zile nyumba zao za mbao..ambazo unakuta wengi ndio wanaishi humo wakishaachana na maisha ya mjini....
 
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Nimekuelewa mkuu.
Wengi wetu mafundi hatupo smat Wala hatupo na wakati.
Pia kukariri kwingi na wasio na ubunifu. Mfano Hilo la paa kua kama mnara hii Ni kutokana na kukariri.
Paa siku zote linatakiwa kuo uniform na jengo.

Lakini hoja yangu pamoja na changamoto zetu tumeonewa mno!
Unapandisha nyumba za watu toka msingi hadi mwisho kwa miaka zaidi ya kumi lakini hata chumba kimoja mtu huna! Malipo Ni madogo mno, hayalingani na huduma itolewayo kwa kweli.
 
Chief unaweza kuwa fundi mzuri sana.. shida ni ubongo wa consumer umeundwa kutaka kuongeza faida.

Kwann nikulipe milioni tano kama yupo ambaye yupo tayari kujenga kwa milioni moja!? After all nyote hakuna insurance... Ni imani yangu kwako tu.. ndio inatufanya wewe unijengee.

Lakini pia ujenzi wetu hauko regulated.. kwahiyo hakuna namna ya kutrack ubora wa ujenzi wako hatua kwa hatua kisayansi.

Ufinyu wa malipo yenu unatokana na taaluma kuwa ya holela.. nikikwama nasaidia fundi siku tano kesho nna mkonobao na mwiko na mimi fundi.. hapo hamuwezi..

Chochote ili kiwe na thamani lazima kiwe regulated na mdhibiti supply yake iwe reasonable na irandane na uhitaji. Sasa hili ni la kimfumo tu ndugu yangu.. japo yapo mawazo kadhaa ambayo ningeweza kushauri.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Naomba kujua umuhimu wa vents kwenye paa.

Naona kama ujenzi wa kisasa hauweki vents kwenye mabati ya paa .

Je nini changamoto au matatizo yanayoweza kujitokeza?

Mbona vents nyingi baada ya muda hupauka na kuwa kama uchafu?

Je mbadala ni upi?
 
Next time gharama zako zizingatie na life span ya thamani unazotengeneza!!
Life span inategemea na matunzo ya mtu.. kwa samani gharama inaweza kuangalia material inazopewa.. ukipewa mbao bora lazima uchaji zaidi na bima incase umeharibu ubao bahati mbaya..

Bei inaweza ikazingatia nature ya miradi... Kama ni kureplicate kitu haiwezi kuwa sawa na kuumba kipya kuanzia design.. yawezekana kisiwe kwa matarajio ya mteja tisa zaidi ukipaswa kurudia urudie kwa kujiamini.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Nani akufikirie???

Panga bei kutokana na ubira wa kazi yako na ujue kujibrand.....

Bila kusahau ubunifu na kuwasilisha kazi kwa wakati
 
Back
Top Bottom