Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,849
- 730,378
Hili naliandika kwa uchungu mno kwakuwa waathirika ni wengi na hata pengine baadhi ya wana JF ni wahanga.
Maisha yanatufunza mengi yanatuonyesha mengi na yanatufunulia mengi
Kuna familia zimebarikiwa, hawa maisha yao ni full shangwe mafanikio na baraka kwao si kitu cha kuuliza , kwao ishu za magonjwa na mifarakano au kuishiwa ni nadra sana kusikia.
Halafu kuna hizi familia ambazo ni matatizo mwanzo mwisho hakuna kinachosimama hakuna kinachoenda sawa si kimahusiano si kibiashara si kikazi wala si kielimu...inaumiza mno unapoona familia ya fulani inaelea kwenye ulimwengu wa mafanikio wakati yako inaelea kwenye ulimwengu wa matatizo ...! Inauma mno asikwambie mtu.
Kimsimgi hakuna kitu kinachokosa chanzo na mara nyingi ikiwa ni mababu na wazazi wetu, matambiko na maagano. ..kuna mahali kuna kitu kilikosewa na hakuna akiyekirebisha aidha kwa makusudi au kwa kutojua sometimes ishu za uchawi na ushirikina vikichangia.
Cha kuleta faraja ni kwamba huinuliwa mmoja katika familia kuja kurekebisha hali hiyo..yeye atakuwa tofauti na wengine yeye ataangaziwa kuiona hali ilivyo na atataka kuchukua hatua...huwa ni mmoja tu katika familia.
Mpendwa mwana JF utakayebahatika kusoma uzi huu, chukua muda kutafakari juu ya familia yako na maisha mliyonayo...! Je, yanaenda sawa? Je changamoto zimekuwa nyingi? Waweza kuwa wewe ndio mkombozi... Basi kama ni hivyo chukua hatua sasa usichelewe kizazi kisije kikapotea.
NAKUOMBEA..