Msuguano huu hauhitaji miwani kuona. Utaona tu hata kama una macho ya kichina.
Wapambe, wananchi na wapenda mabadiliko muonekano wa wazi ni Mh huyu kugombea popote pale ili mradi anagombea.
Hii dalili ya kubadili ratiba ni ishara iliyomlenga Bwana Lowasa
. Lazima ieleweke ndan ya ccm kuna wapenda mabadiliko wanaamini yanaweza kutokea ndani ya ccm
Kimsingi Mwandosya hawez tena. Salim A. Salim anaona jins atakavyochafuka tens hatakubali. Judge hawezi hapa namaanisha bwana Ramadhani.
Ule msemo wa baba Nyerere utadhihiri Leo. Ikulu ni mahali patakatifu ukiingia kichw kichw utaaibika tu
Tanzania tumekosa kitu kimoja tuu, tungekuwa Ulaya ya africa. Elimu ni Tatizo kubwa tu kwa wananchi, wengi wetu tukiwa vijiweni tunashindwa kujenga hoja mbele ya kundi kubwa la vijana wanaoweza kuichambua political science, hili linawapelekea waone mkombozi wao kuwa yule wanaeamini.
Nionavyo mimi, Nape anahangaika kumzuia Lowassa, huyu jamaa ni kama maji ya mafuriko utashindwa tu. Lowasa sijui kwa nini amekubalika haraka sana. Lowassa ameamua tu kutumia busara na utu uzima wake. Lakini kama alivyofanya zzk Lowassa angeweza pia. Lakin ukubwa dawa. Sasa watanzania ambao wamekosa elimu rasmi ya chuo kikuu wao chuo kikuu chao ni street, mara nying wengi ambao hawakubahatika wanatumia street university.
Kiukweli wameelimika na hawakubali. Hapa utawataja wapiga debe, machinga, mama ntilie, Bodaboda wanavyuo nk. Huyu ni LOWASA na Mbowe na Slaa. Kwa sasa siasa za Tanzania ni LOWASA NA CHADEMA. UTAKE USIKATAKE.
Kwingineko ndani ya CCM kuna wapenda mabadiliko, na hapa mtoe nape, Kwa ccm shida iko hapa kuzuia mabadiliko, mabadiliko ya kumuweka mgombea jinsia K yanakaribia kupitwa na wakati, kwa sababu hakuna wakuhimili mikiki ya siasa na hapa ukumbuke ni pamoja na siasa za kimagharibi.
Sasa utashangaa mwananchi asiejua chuo kikuu anakuchambulia siasa. Na anaamini maneno yake.
Mkuu ulikuwa umenena vema,lakini umechanganya
kile kitu Gwajima anaita ''kula maharage sijui ya nini?''
Suala la university na uwezo wa kuchambua siasa ni vitu viwili
tofauti,simahanishi wale wa vitivo vingine namaanisha
wanaoitwa nguli tena waalimu wa siasa nitoe mfano wa wa Profesor yule wa kuhindi
pamoja na Dokta Bona bana,hawa ni walimu wa chuo kikuu,je uliona walivyoharibu
mchakato wa katiba? hawa wamewafanya watu wengi kuhamini
kuwa hata kama mtu ni msomi hafurukuti mbele ya njaa,tena afadhali asiye
soma ''has nothing to loose''.
Hili limepelekea vijana wa vijiweni kujiwekea utaratibu wao
wanaouamini kwamba utawaletea mabadiliko,kuliko kuendeshwa na njaa
za wanaojiita wasomi huku wakipelekeshwa na maslahi binafsi.
Nikuombe kama unajiamini kuwa unajua siasa za chuo kikuu
jitoe upite vijiweni ili utoe elimu,wakupime unachokisema
kama ni chema watakusikiliza kama kuna unazi watakutosa
maana elimu ya siasa imejaa mitaani kupitia TV
kwa kutumia watu makini kama akina Tundu LIssu.
Binafsi namtakia kila la Kheri EL
CDM,UKAWA na wapenda mabadiliko wote.