Kuna cha kujifunza hapa mafundi ujenzi

Kuna cha kujifunza hapa mafundi ujenzi

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Mafundi ujenzi wanahitaji kuwa na ujuzi wa vitendo, maarifa ya kina na mbinu za ubunifu za kufanya kazi. Hii ni kwa sababu taaluma yao inahusiana moja kwa moja na usalama wa majengo, madaraja na mifumo mikubwa ya jamii.

Elimu ya darasani pekee haitoshi; mafundi wanapaswa kujua kutumia vifaa, programu za uhandisi na teknolojia za kisasa. Ubunifu wao hutumika kutatua changamoto mpya kama ujenzi wa miundo rafiki wa mazingira na ya gharama nafuu. Bila vitendo na ubunifu, taaluma yao hubaki nadharia zisizoleta suluhisho halisi kwa maendeleo ya jamii.
 
Sema tu mafundi wa tanzania tunakutana na changamoto sana. Hususani changamoto za clients.

Kazi ya 1m mtu anakulilia ana 300,000, yaani unabaki tu unashangaa.

Hali ngumu za uchumi za wateja wetu zinapelekea shida kwa mafundi.
Anyway, tutafika.
 
Tatizo pia Sisi Mafundi hatubadiliki kujiongeza kuendana na wakati. Kama ubunifu unakuwepo hiyo M1 mteja ataitoa tuu
 
Sema tu mafundi wa tanzania tunakutana na changamoto sana. Hususani changamoto za clients.

Kazi ya 1m mtu anakulilia ana 300,000, yaani unabaki tu unashangaa.

Hali ngumu za uchumi za wateja wetu zinapelekea shida kwa mafundi.
Anyway, tutafika.
Sababu clients tunajua katika hiyo M1 tunapigwa
 
Mafundi wengi wa bongo pasua kichwa. Hata mashine ndogondogo zinazopatikana madukani hawajiongezi walio wengi. Huishia kuazima au kubaki analogi
 
Back
Top Bottom