Kuna baadhi ya watalii wa kigeni wanaroho mbaya sana

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Yaani unakuta mtalii tena mgeni yuko mbugani na mikamera yake alafu akikuta mnyama anaekula mnyama mwenzake kama fisi simba au chui anataka kula mnyama badala ya kumsaidia huyo mnyama anaeliwa asiliwe eti ndio kwanza anaseti kamera vizuri kushoti video mnyama anavyoliwa.

Kinachouma zaidi unakuta mnyama kama twiga au pundamilia na nyati ambae serikali ndio inawathamini zaidi ndio wanauwawa, badala ya kuzuia wanawaacha. Inauma sana/nimeumia sana, hawa watalii hata kama wanatuingizia hela nimewachukia sana.

Mbona kwao wanyama wao wanawapa nyama, tena mara nyingi naona ya ng'ombe hawaachi wakaua ovyo ovyo kama huku kwetu? Au wanafurahia wanyama wetu wanavyouliwa?
 
Yaani unakuta mtalii tena mgeni yuko mbugani na mikamera yake alafu akikuta mnyama anaekula mnyama mwenzake kama fisi simba au chui anataka kula mnyama badala ya kumsaidia huyo mmyama anaeliwa asiliwe eti ndio kwanza anaseti kamera vizuri kushoti video mnyama anavyoliwa.

Kinachouma zaidi unakuta mnyama kama twiga au pundamilia na nyati ambae serikali ndio inawadhamini zaidi ndio wanauwawa badala ya kuzuia waacha.
Inauma sana/nimeumia sana hawa watalii hata kama wanatuingizia hela nimewachukia sana.mbona kwao wanyama wao wanawapa nyama tena mara nyingi naona ya ng'ombe hawaachi wakaua ovyo ovyo kama huku kwetu? Au wanafurahia wanyama wetu wanavyouliwa ?
Acha ushamba bablai...hata askari wanyama pori hawawezi kuzuia simba kula mnyama mwingine.
Ni kosa kisheria kuzuia mnyama kula mnyama.
 
Yaani unakuta mtalii tena mgeni yuko mbugani na mikamera yake alafu akikuta mnyama anaekula mnyama mwenzake kama fisi simba au chui anataka kula mnyama badala ya kumsaidia huyo mmyama anaeliwa asiliwe eti ndio kwanza anaseti kamera vizuri kushoti video mnyama anavyoliwa.

Kinachouma zaidi unakuta mnyama kama twiga au pundamilia na nyati ambae serikali ndio inawadhamini zaidi ndio wanauwawa badala ya kuzuia waacha.
Inauma sana/nimeumia sana hawa watalii hata kama wanatuingizia hela nimewachukia sana.mbona kwao wanyama wao wanawapa nyama tena mara nyingi naona ya ng'ombe hawaachi wakaua ovyo ovyo kama huku kwetu? Au wanafurahia wanyama wetu wanavyouliwa ?
Yale ndyo maisha yao waache walane wenyewe kwa wenyewe
 
Sasa amekuja kuamua ugomvi wa nature au kaja kutalii

We ukiona paka anavizia panya unamfukuza

Sasa wakale wapi gengeni ama
Mnyama anaepewa nyama ni zoo tu ila hao wanajitafutia wenyewe Sasa ugomvi usiomhusu auingilie wa nini?

Kama umewahi kumsikia Kevin Carter basi huyu ndio ungemtukana sana na hata kulia kwa uchungu

Alikuwa anarekodi vulture akimsubiri mtoto wa kiume afe ili amle
Ilikuwa mwaka 1993 huko Sudan

Dunia nzima ilimlaani ila alikuwa best photographer na alipewa tuzo NY

Baada ya miezi 4 tangu apate tuzo alijiua mwenyewe
Alishindwa kuvumilia maneno kwani angeweza kumsaidia yule mtoto na hata kumpa maji na chakula pia kumpeleka katika kambi ya wakimbizi iliyokuwa nusu maili tu kutoka hapo

Sasa yeye anasema alikuwa anafanya kazi ya kuripoti matukio anaeliwa sio kazi yake

Hii picha iliniliza pia
 
Back
Top Bottom