Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 284,456
- 738,852
Wengi tunakutana na vituko vya hapa na pale majumbani mwetu na kudhani ni ushirikina au majini nk...umekaa sebuleni mara unaona kitu kinapita kwa kasi na kupotea ukijaribu kufikicha macho uone vizuri hamna kitu
Au ni usiku wa manane unashtuka usingizini na kusikia kabisa mlango wa chumba fulani kilichofungwa ukifunguliwa au dirisha, kuna wakati pia Utasikia vyombo jikoni vikitingishwa lakini ukija kufuatilia kwa karibu hakuna kitu
Matukio ni mengi kukuta chakula kimeliwa kidogo kujikuta umelala upande mwingine wa kitanda kuota ndoto zilizo halisi kabisa kusikia watu wanaongea wanatembea au wanacheka... .mara nyingi hivi vitu hutokea kukiwa kimya kabisa na utulivu na hasa kama ndani ya nyumba upo pekeyako, hizi roho hukupa kampani ma kukuchangamsha
Hizi ni roho zinazotangatanga zinazotafuta makazi kwahiyo zikikosa makazi misituni kwenye miti na miili ya watu hizi hukimbilia kutafuta nyumba zizipendazo na kuishi huko
Kuna mada ya kutakasa nyumba tuliijadili hapa ...kuna roho zikiona nyumba iko tupu kwa muda mrefu basi hupenda kuweka makazi yao humo na inapoingia familia bila kuitakasa hiyo nyumba mengi hutokea kwakuwa zile roho huona kama zimeingiliwa
Kwahiyo kati ya hivi vituko na mambo ya ajabu ajabu yatokeayo ndani ya nyumba zetu si yote ni ushirikina ulozi uchawi wala kuwangiwa..baadhi ni hawa washikaji zetu wasioonekana hupenda kucheza nasi