GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Nitainukuu tu hapa kidogo kauli yake Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mheshimiwa Glorious Luoga ambayo ameitoa asubuhi ya leo alipokuwa akizungumza ' mubashara ' kabisa katika Kipindi ' maarufu ' cha Clouds tv 360 on Saturday wakati akihojiwa na Watangazaji Kijjah na Sizya.
" Jamani Watangazi Mimi ndiyo Rais wa Wilaya ile ya Tarime hivyo siwezi nikakubali Mheshimiwa wangu Rais aharibikiwe kwa sababu tu ya Mbunge mmoja John Heche ambaye kimsingi hana machungu na wana Tarime na anakataa maendeleo yao kuletwa huku.....Mimi ni Rais wa Wilaya bhana na yeye ni Mbunge tu ".
Kauli hiyo niliyoinukuu hapo juu imenifanya nifikiri na hadi sasa sijapata jibu na sana sana tu naona Kichwa changu kinaniuma kiasi cha hata kufikiri kwenda kupata tiba ya haraka kutokana na ' upuuzi ' ambao kila uchao naushuhudia nchini Tanzania.
Nawaamini kabisa wana JF wote na kubwa zaidi nawapenda na nawakubali mno hasa kwa aina ya uwezo wenu mkubwa na wa kutukuka kabisa wa kufikiri na kujenga hoja zenye mantiki hivyo basi ni matumaini yangu kuwa hamtaniangusha.
Hivi ' logically ' tu kati ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bwana Glorious Luoga ambaye ' ameteuliwa ' tu Rais mwenyewe na Mbunge wa Tarime Bwana John Heche ambaye ' amechaguliwa ' hasa na wana Tarime kwa ujumla wao ni nani ana haki au ana uhalali au hata anapashwa kujiita Rais wa Tarime?
Nitashukuru mkinijibu na naomba kuwasilisha kwenu.