Kumuona Daktari Tsh.10,000/=

Kumuona Daktari Tsh.10,000/=

Ibravo

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
539
Reaction score
202
Hivi huu utaratibu wa kutoa elf 10 kwenda kumuona daktari kabla ya tiba ni sahihi wajameni !?

Nimetozwa mwekundu kumuona daktari wa ngozi (Temeke Hospital),maelezo niliyopewa na huyo Skin Specialist nikilinganisha na muda nilioutumia kuitafuta hiyo buku kumi hayalingani kabisa. Wa hali ya chin tunaumia maana nimeshindwa kununua hata dawa naona kama nimeenda kumtunza daktari pumbaaavuu.

Serikali liangalien hili naona sasa watoa huduma za afya wameona kugoma ni kupoteza muda badala yake wanacharge pesa ambazo hazistahili.
 
Hivi unaelewa tofauti ya General medical doctor na Medical specialist? Kuwa specialistsiyo kitu cha mchezo kijana. Tena hiyo ni ndogo mimi ningekutoa upepo wa Tshs 50,000/= (Consultation fee).
 
Pole sana ndugu yangu! Hapa Mwanza yupo mmoja naye ni Specialist wa magonjwa ya ngozi kumwona sh 30,000 (tu)
 
"Daaa! Hiyo pesa nyingi kumlipa daktari wa Tanzania. Serikali itupeleke India kama viongozi wanavyogharimiwa kutibiwa mafua" Tafakari,chukua hatua.
 
Hayo Mambo ndio ulimboka aliyokuwa anayapigania lakini "Aliyemteka Ulimboka Huyu Hapa" akafanya yake.
 
Kijana una masikhara kweli wewe, yaani kumuona Daktari bingwa kwa elfu 10,000/- nani kakuongopea??

Kumuona Dr bingwa siyo chini ya shilingi 50,000/- minimum!!
 
Duh! tusiokuwa nazo tutaangamia tupende tusipende.
 
Watanzania Nyerere aliwaharibu. Mnataka afya bure. Elimu bure. Kila kitu bure. Sasa wewe walalamika kwa elfu kumi ambayo ni consultation fee ya clinical officer au Nurse... ukija tunako charge kwa dola si utakimbia...
 
Aliwekeza muda na pesa hata akawa specialist,ww pia unaweza fanya ivo ili ue kama yeye ila kama huwezi mlipe chake uhudumiwe.
 
Kijana una masikhara kweli wewe, yaani kumuona Daktari bingwa kwa elfu 10,000/- nani kakuongopea??

Kumuona Dr bingwa siyo chini ya shilingi 50,000/- minimum!!
Huo ubingwa wake sijauona maana maelezo yake aliyonipa hayatoshelezi kabisa kwa yeye kuitwa bingwa,na kama yangetosheleza nisingesema chochote,mnajivisha majoho ya ubingwa kumbe bure kabisa.Huu ni wizi.
 
Siye walalahoi tukiumwa hatuna tabu tunazama porini...tunafukua mizizi tunatafuna....tunaendelea na kusaka tonge....
Mabingwa ndio hao wanaopasua miguu badala ya vichwa...si bora kumi yangu nikanywee ulanzi tu kusukumia mizizi niliyotafuna....
 
Hiyo 10 mbona nafuu mi nilichajiwa 30 na specialist wa ngoz tena hapo unaanzishiwa clinic ya kila wiki 2 kurudi kumuona dk kwa maendeleo yko sasa ikiwa ni mfululizo wa miez 2 niambie iyo consultation fee itakuwa nimetoa kiasi gan
 
DK bingwa kumwona ni expensive sana wala sio 10,000/= una bahati sana kumwona kwa gharama hiyo...!!
 
Back
Top Bottom