Kumuangalia vyema mtoto wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumuangalia vyema mtoto wako

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jun 8, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  Ni jambo la busara kujitunza wewe na mwanao. Kutunza mtoto wako linaweza kuwa jambo la kukufurahisha, lakini ni kazi ngumu. Utampatia mtoto chakula/utamlisha mtoto mara ngapi na baada ua wakati mgani? Wewe hufanya nini mwanao anapolia au anapougua? Unozuia maradhia aje?  Unaweza kuwa mwepesi kushtuka/utakuwa na wasiwasi au lakini utayagundua hayo haraka. Utashtuliwa na ambayo unajua tayari. Katika sehemu hii, utapata kujua unayofaa kufanya utakapomleta mwanao nyumbani

  Kumpeleka mwanao nyumbani
  Mtoto aliyezaliwa anajiratibisha na ulimwengu ulio tofauti na joto na usalama wa tumbo la mamake. Watoto hawa wanastahili kupendwa,kulishwa, kuwekwa safi na wakiwa na joto inayofaa. Kuna mambo mengi mapya wazazi wanapaswa kujua.

  Afya ya mwanao

  Unafaa kumwita/kumpigia daktari wako kama utaona uafuatayo kwa mwanao:
  Kukosa kula/kukataa chakula
  Kuwa na rangi isiyostahili
  Nguvu kidogo
  Joto la juu ya 380c chini ya kwapa
  Ghasia/fujo zisio za kawaida
  Kulala zaidi ya kawaida
  Kutapika au kuhara
  Shida za kupumua


  Kumbadilisha nepi  Usimwache mwanao juu ya meza ya kumbadilishia nguo sababu anaweza kuanguka na kuumia. Weka kila kitu unachohitaji juu ya meza hii au karibu nawe. Wakati unasafiri, beba kila kitu kwa kifuko cha ‘diaper’.

  Jinsi ya kumbadilisha napi
  Mlaze mwanao mahali dhabiti na tambarare kama kwa meza kasha ufungue diaper iliyochafuliwa.
  Inua miguu ya mwanao kwa kuishikia kwenye kufundo na utoe ‘diaper’ hio.
  Osha mwanao vizuri kwa kutumia katani na maji moto (kwa watoto wachanga sana).
  Hakikisha umempamgusa mwanao mbile na nyuma ili kinyesi kisitapakae kea sehemu zingine za mwili.
  Tumia uvumbi wa wanga wa nafaka (comstarch powder) au Fulter’s Earth na usiguze uso. Usitumie uvumbi huu kwa watoto wachanga mno.
  Pitisha diaper chini ya mtoto. Vuta sehemu ia mbele kati ya miguu na ufunge.

  Vipele visabishwao na napi
  Mtoto hutumia diaper kama kumi kwa siku. Kama hutomgeuzia mtoto wako ‘diaper’ atapata vipele. Hili hutokea kama mwanao atakuwa na maji maji (ulowevu) akiwa amevishwa diaper. Huu upele hukaa mwekundu na hukaa kwa siku chache. ‘Diaper rash inaweza sababishwa pia na sabuni ya vumbi ya kuosha ilizo na nguvu sana au vitu vya kufanya ngozi iwe nyororo, kwa hivyo kama kumweka mwanao safi na mkavu hakusaidii geuza bidhaa unazo muosha nazo.

  Jinsi ya kushughulikia vipele vya napi
  Unapongeuzia mwanao diaper mwache kwa dakika 10 ili apunge hewa
  Lowesha nyuma ya mwanao kwa maji moto kisha ipanguze kwa tahadhari
  Geuzia mwanao Diaper ma utumie napi kwa muda au kama unatumia napi geuza na uanze kutumia diaper kwa muda
  Usitumie suruali za ndani zitakazo hifadhi ulowecu kwa diaper
  Tumia cream’ kama Fissmn Paste kwa ‘rash’. Usitumie uvumbi au ‘lotion’

  Kama vipele havittoweka baada ya siku tatu au mtoto anaanza kupata malengelenge, muone daktari wa watoto.

  Kumnyonyesha mwanao  Kwa watoto wengi, maziwa ya mama ndicho chakula bora zaidi. Ni rahisi kwa watoto wako kulisaga kulicho ya kununua (infont fomula). Maziwa ya mama humlinda mtoto kutokana na maradhi Fulani na waru wengine hudhani pia husaidia kumfanya mwanao mwerevu. Maziwa ya mama pia huwa na viwango vistahilivyo vya mafuta, sukari, maji na protein. Kumnyonyesha mwanao pia huhifadhi wakati na pesa.

  Mnyonyesha mwanao anapokuwa na njaa au baada ya masaa 2-3. Kama mtoto wako anapata kuzichafua (kukonjolea na kukumia) nappy 6-8 ni ishara ya kwamba anashiba. Unafaa kungoja hadi mwanao atakapokuea na miezi 4-6 ili kuanza kumlisha chakula kikavu. Ni jambo la busara kuuliza daktari wako aina ya chakula unachofaa kumlisha mwanao au wakati unataka kumpatia chakula kipya ambacho hujawahi kumpatia tena.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kumpa maziwa kwa chupa  Kama unamlisha mwanao kwa chupa, hakikisha umechanganya maziwa hayo sawasawa ili mtoto apate malisho yanayofaa. Pia zungumza na daktari wako wakati utaanza kumlisha mwanao mchanganyiko (familia) ulio na ‘iro’.

  Vipi, lini na nini unalisha mtoto wako ni muhimu. Kila kitu kutoka aina yamchanganyika, joto la mchanganyiko na aina ya chupa unazotumia hujalisha. Unaweza ujumbe huu kutoka kwa daktari wako au kliniki.

  Hakikisha umemuliza daktari wako kuhusu utakapoanzia kumpa mtoto wako chakula kikavu. Hata kama mtoto wako ataanza kujaribu kukifikia/kushika kijiko, ni vizuri umuulize daktari kwanza.


  Kumuosha mwanao  Ni vizuri kumweka mwanao safi na mkavu km. kumgeuzia ‘nappy’ mara kwa mara. Hakikisha kuosha napi vizuri baada ya kuchafuliwa. Uso, sehemu za siri na mikono ya mtoto wako zinafaa kuoshwa kwa sifongo (sponge) kila siku. Unafaa kumwosha mwili wote baada ya siki mbili au tatu. Watoto wachaga bado wana ugue wa kitovu. Unapaswa kumwosha kwa sifongo hadi wakati ugue huu utakatika kabisa. Uoshe ugue huu kwa uangalifu mwingi na utumie mvinyo (spirit) wa upasuaji uliotiwa kwa kitakia cha katani. Usivute ugue wa kitovu unapaswa kujiangusha mwenyewe.

  Usije ukamwacha mwanao ndani ya karai la kuogea. Watoto wanaweza kufa maji yaliyofika inchi mbili tu. Unapomwosha, hakikisha una vifaa vyaa kumwoshea, sabuni na kadhalika ili usimwache mwanao kwa karai la kuogea bila wakumwangalia unapoenda kuvichukua.

  Maji yaliyo moto sana huenda yakamchoma mwanao. Kama unakifaa cha kupasha maji moto weak kwa joto la 49oC . Pima joto la maji kwa kiko cha mkono wako. Kabla hujamweka mwanao ndani na uhakikishe maji ni vuguvugu


  Kumvisha nguo  Mvishe mwanao na kunjo moja zaidi wakati yu mchanga na jiepushe na kumwacha mwanao kuliko na baridi kwa muda mrefu.
  Watoto hupoteza joto haraka sana, hivyo hakikisha umewafunika kichwa na miguu
  Wakati kuna joto jingi, mweke mwanao mbali na jua. Linda mwanao kna nguo za mikono-mirefu(long-sleeve), nyepesi na umweke kivulini
  Nguo zote mpya zinafaa kufuliwa kabla ya kutumia

  Kuota meno  Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengine huanza kkuudhika kwani huumia kabla meno hayajatokea kwa ufizi. Watoto wengi humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.

  Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.

  Mawaidha wakati mtoto anaota meno
  Wakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ule utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.
  Mpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka. Unaweza kumpa kijiko cha mpira au kitambaa safi.
  Usifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.
  Kuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote

  Baada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kumuona Daktari

  Kuchagua daktari wa mtoto  Unatakiwa kumchagua daktari wa mtoto wako kama ungali mja mzito miezi 3 kabla ya kujifungua. Waulize marafiki, jamaa au daktari wako. Waweza kupata matibabu ya bure kwa watoto wachanga kutoka kwa hospitali za mikowa au kliniki za jamii, kwa malipo ya chini katika hospitali za serikali. Mchaguwe daktari uliye na imani naye aliyemzuri mwenye kuelewa na maono tofauti na pana.

  Uchunguzi wa mara kwa mara


  Mtoto wako anahitaji kuonekana na daktari kila mara ili akuwe kwa raha na afya. Watoto wana ratiba yao ya kupelekwa kwa daktari.

  Kati ya masaa 24 baada ya kuzaliwa
  Siku 2-4 baada ya kuzaliwa ikiwa mtoto atapelekwa nyumbani chini ya masaa 48 baada ya kuzaliwa.
  Wiki 2-4
  Miezi 2
  Miezi 4
  Miezi 6
  Miezi 9
  Miezi 12.

  Unachotarajia kwa uchunguzi wa kila mara

  Kila uchunguzi daktari hutizama urefu wa motto,uzito,na kichwa cha mtoto ili kufahamu jinsi motto anvyokuwa.Daktari pia atachunguza macho ya mtoto, masikio, mapafu, moyo, mdomo, sehemu nyeti na tumbo. Katika muda wa mwaka mmoja mtoto wako antakiwa kukaa,kugaagaa na kujivuta mwenyewe hadi asimame.

  Chanjo:

  Mtoto kupelekwa kupata chanjo ni muhimu, inapendekezwa watoto wapate chanjo hizi kuzuia maradhi kuhatarisha maisha yao.

  Homa ya manjano B (Hepatitis)

  Dondakoo, Pepopunda na Pertussis – Diptheria, Tetanus, Pertussis (DTP)
  Polio
  Surua, matumbwitumbwi, Rubella – Measles, Mumps, Rubella (MMR)
  Haemophilus influenzae type B (HIB)
  Varicella, Tetewanga – Chicken Pox

  Kumpeleka mwanao nyumbani
  Mtoto aliyezaliwa anajiratibisha na ulimwengu ulio tofauti na joto na usalama wa tumbo la mamake. Watoto hawa wanastahili kupendwa,kulishwa, kuwekwa safi na wakiwa na joto inayofaa. Kuna mambo mengi mapya wazazi wanapaswa kujua.

  Afya ya mwanao

  Unafaa kumwita/kumpigia simu daktari wako kama utaona uafuatayo kwa mwanao:

  Kukosa kula/kukataa chakula
  Kuwa na rangi isiyostahili
  Nguvu kidogo
  Joto la juu ya 380c chini ya kwapa
  Ghasia/fujo zisio za kawaida
  Kulala zaidi ya kawaida
  Kutapika au kuhara
  Shida za kupumua

  Kuwaelewa Watoto
  Kumuelewa mtoto wako ni muhimu sana, ili kushughulikia mahitaji yake. Watoto ni tofauti kuelewa ishara zake kutaendelea katika kila kiwango. Ikiwa una haja ya kufahamu tabia za mwanao, muite daktari wa watoto au nenda katika kliniki ya jamii.

  Mtoto wako anvyokua na kubadilika hata ishara zake zitabadilika, lakini miezi michache ya kwanza kulia kutakuwa ndio njia ya pekee ya mawasiliano.

  Kumliwaza mtoto wako anapolia
  Hata kama mtoto haumwi na tumbo , kumnyamazisha motto anayelia ni vigumu sana . Kama umejaribu kila mbinu na hujafaulu , jaribu yafuatayo:


  Mfunge mtoto kwenye vitambaa au blanketi ili ahisi joto kiasi na atulie.
  Jaribu kucheza muziki muororo au muimbie nyimbo za kumbembeleza.

  Mbebe kwa makini au nenda matembezi naye katika gari lako na hakikisha umemkalisha nyuma.
  Kumkanda mgongoni au tumboni kwa weza kumliwaza hasa kama ana hewa tumboni.

  Kumnyonyesha
  kwa weza kutuliza mdundo wa roho yake kutuliza tumbo lake na viungo pia.
  Habari njema ni kuwa watoto hupita hatua hii wanapokuwa. Mtoto wako anapokuwa wiki 6 au 8 watakuwa katika hali ya kuweza kujiliwaza na kulia kwingi kutakwisha.

  Kwa Nini watoto Hulia?

  Njaa:
  Mtoto anaweza kuwa njaa.Watoto hula kama mara 8 hadi 12 kwa siku wanaponyonya,na mara 6 hadi 10 kwa siku anaponyonya chupa.

  Nepi chafu: Mtoto hana raha anapokuwa kwa nepi chafu, akiachwa kwa muda mrefu ataambukizwa vipele.Mbadilishe nepi kila wakati.

  Baridi au joto: Watoto wana ngozi nyororo na hupata baridi haraka.Wanahitaji kufunikwa vyema lakini sio kupita kiasi.
  Umakinifu: Watoto wanachoka watalia.Mchukuwe na umpapase mgongoni ili afahamu upo.

  Ugonjwa: Mtoto wako anaweza kuwa mgonjwa ,mtizame joto la mwili na wasiliana na daktari.
  Hewa tumboni: Watoto wachanga huhitaji kukandwa kila mara au la hewa humjaa tumboni na kumpotezea starehe.

  Usingizi: Mtoto akiwa amechoka na ana usingizi atalia,jaribu kumlaza apate usingizi.
  Nitafanya nini ikiwa mwanangu bado yuwalia?

  Pengine hutagunduwa kwa haraka shida zake, umejaribu mbinu zote na hajanyamaza. Anaweza kuwa na msokoto wa tumbo kwa masaa 2 au 3 kwa siku mara tatu kwa wiki. Msokoto wa tumbo humuondokea mtoto anapotimiza miezi 4.
   
 4. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mzizimkavu ukojuu sana mkuu nimekusoma nashukuru sana kwa shule yaleo maana wazazi wengi tunajisahau sana haswa pale tunapowaachia housegirl watoto wetu ina kuwa janga na wengine kupoteza maisha kiurahisi kutokana na kuachwa na nguo zilizolowana au kama sio hivyo usafi wanaofanyiwa sio wakuridhisha.Asante sana na ubarikiwe.
   
 5. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,350
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ahsante mzizi
   
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,897
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu nashukuru sana Mungu huku nilishapita. mwaya ahsante sana umenikumbusa with my kichanga nitajitahd kumtunza.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Umeshapita yaani huzai tena? Hata tukitaka tupate katoto kamoja ka uzeeni mimi na wewe hatuwezi tena kupata?... gfsonwin
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,897
  Trophy Points: 280
  lolz! yani MziziMkavu na utu uzima huu nikaanze kusukuma mtoto labour , na mabinti wa miaka 20+ lol! au nikapate sessiorian section na uzee huu ilihali nimezaa mara 3 kwa kupush, hakuna cha stitch wala nini na tumbo safi hakuna makovu ya visu na ukiniona ni kama binti wa miaka 18 upo hapo. chezeya........... mwl weye. kwa sasa nakula maisha tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ngoja si tuendelee na mashindano ya miss-labour
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hii itanisaidia sana kumlea mwanangu "IKRIMA"ngoja namtafuta humu ndani then I will be back soon!
   
 11. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Kumbe na wewe unakichanga?ni cha "me au ke?"changu ni me!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,897
  Trophy Points: 280
  mimi nina vidume 3. hajambo lakin mama na mtoto? ush mtoboa maskio tayari nini?
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,897
  Trophy Points: 280
  mwaya,jitahd tu utamaliza, kila jambo kwa wakati wake. ila kwangu mimi ni bpra kuzaa haraka umalize mapema uanze kurudisha mwli wao uwe binti tena.
   
 14. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Wako poa wote!
   
 15. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Kua binti?
  How easy?
   
 16. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ndo nataka hivyo nitavipa interval ya wk nataka kufika 30 Mungu akinisaidia nifikishe 4 nastop
   
 17. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,897
  Trophy Points: 280
  yaani ukweli ukiwapa wanao interval ya miaka 2 ukamaliza kuzaa na miaka 32 that is very good tena ukute huzai kwa siza kama wadad wa siku hizi lol unarudiaje usichana? yaani utakuta mwanao anaambiwa mdogo wako. ji keep smart and uwe mtu wa mazoez japo uwe unaruka kamba asbuhi na kupiga seat ups. yaani sijisifii lakin najipenda manake nimekuwa kama kabinti ka form iv ka jangwani.
   
 18. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #18
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Kwa sasa unamiaka mingapi?na unatutoto tungapi?umri wao jee?
   
 19. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #19
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hahaha?Vp maufundi yanachujaga kweli?
   
 20. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #20
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,897
  Trophy Points: 280
  mbona unauliza kwa kushangaa spika? ni rahisi kwa mama anayemaliza kulea kuwa binti au anayelea. njia ni moja tu. anajikeep flexible kwa kufanya mazoezi anakuwa smart kimavazi na kila kitu na pia anahakikisha hanenepeani sana. plus lotion yako nzuri na ukaujulia mwili wako kimavazi mbona anakuwa binti kuliko umaowaona huko bara barani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...