Kumtunza mwanamke kwa lengo la kumridhisha ni kupoteza muda wako

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,955
6,885
Habari Wana JF wenzangu,

Leo roho yangu imenituma kupoteza muda katika keyboard za simu yangu nikiwaza kuwa iwe isiwe lazima leo niwashtue wanaume wenzangu (amkeni) maana tumekuwa tukiumia sana kupambana kwenye Kila hali (Jua na Mvua) ili tukipata pesa basi tuhakikishe Eva anafurahi na ajivunie kuwa na nasi katika maisha yote. Msemo wa "nyuma ya mwanaume mwenye mafanikio basi kuna mwanamke" hauna maana tuifikiriayo kwamba Mwanaume ili kuwa na mafanikio basi lazima awe na mwanamke Bali maana yake ni kwamba mwanamke hufuata penye pesa au mafanikio hivyo ni ngumu kukuta mwanaume mwenye pesa akiwa Single ni lazima tu utakuta kuna Eva kajipenyeza na kashamuwahi mapema Washapu sana Hawa watu.

Haya twende direct kwenye kichwa cha Uzi huu kisemacho "Kumtunza mwanamke kwa lengo la kumridhisha na kumfurahisha ni kupoteza muda wako" Hapa nataka nikuambie tuu mapema kwamba Hawa watu huwaga hawana Shukrani na kama ipo basi ni ya mdomoni tu kwani wanaongoza kwa kusahau wema tuutendao, Kuna mzee aliambia mke wake alikuwa akilalama kisa yeye kawajengea wazazi wake nyumba lakini wazazi wa mke hajawajengea basi jamaa kumridhisha mkewe akawajengea na wazazi wa mwanamke ambao ni wakwe zake hilo likapita, Baada ya hapo sasa ikawa kila anachokifanya mwanaume kwa wazazi wake basi na mwanamke atalalamika Yani ukifanya kwenu basi ufanye na kwao mfano; Week hii mama wa mwanaume kaumwa basi jinsi mwanaume atavyospend muda mwingi kuhakikisha mama yake anakuwa sawa basi ajiandae maana muda si mrefu mwanamke Atafanya juu chini hata kwa uwongo tu ili hela imtoke tena mumewe iende kwao Hapa ninapoandika huu uzi mume tupo nae tunaparangana kwenye nyumba za kupanga na ana nyumba ila kamuachia mwanamke aishi tu mwenyewe maana visa haviishi mwanamke Kila siku anadai pesa tu Kila siku matatizo ya kwao anatatua hili linakuja hili, siku akisema Hana hela basi mke anaweza hata akatufuta danga ili limmege limpe hela yote hayo kumkomoa mumewe, Mwanaume kwa Sasa hua anatuma tu hela za matumizi ya nyumbani lakini hataki kukaa na mke wake ananiambia "Mwanangu hivi viumbe haviridhiki Yaani yote niliyofanya lakini bado ananiita mbinafsi nikimuambia sina hela wakati anahitaji"

Kwa siku ukiwa na mwanamke mnatumia 10,000 kwenye kula ambapo kwa mwezi ni sh.300,000, tuseme ungekuwa single basi wewe peke yako ungetumia 150,000 tu, kumaanisha kwa mwezi mzima na yeye mwanamke anatumia 150,000 yako kwenye kula basi Usishangae siku anakulalamikia Kuwa umeshindwa kumuudumia hela ya kusuka na akafall I love kabisa na jamaa ambae Kila week anampa 15,000 ya kusuka na akawa anamtunuku na tunda kabisa kwamba ndo anamuhudumia vizuri wewe humjali, Yaani jamaa anaetumia 15,000×4 kwa mwezi sh.60,000 kwa kusuka anasifiwa na Anaonekana ndo mwanaume mwenye upendo kuliko unaetumia 150,000 kumlishaSasa mwanaume mwenzangu Chagua moja Uhudumie chakula Ushindwe kuhudumia nywele usaidiwe au utaongeza hio 60,000 kwa mwezi? Mabantu walivyoimba "No love No stress" walitakiwa wajengewe sanamu lao pale posta Aisee, Ndio ni ukweli kabisa, maana ukiwa single kazi yako ni kumalizia vile walivyoshindwa wenye wake zao alafu ujishindie tunda kirahisi sana Ila kwa umakini mkubwa hapa ndo uelewe kwanini mwanaume akikufumania na mke wake basi adhabu mbaya wanayoipenda ni kukufumuarinda, Yaani anakumalizia hasira zake zote kwako,

Yoyote ya yote hapa ni kutaka Kuonesha jinsi wanawake wasivyokuwa na shukrani na wasahaulifu wa fadhila, Kwa Mimi hata mke wangu itokee kwamba Figo yake imefeli Alaf natakiwa nitoe yangu asee atanisamehe kwa kweli japo siombei, Hivi mnakumbuka kisa cha msanii anaeitwa MABESTE jamaa alimaliza akiba na mtaji wake wote kumtibu mkewe kitendo mkewe anapona jamaa akawa hana ramani kabisa Tena hivyo akawa homeboy tu mke karudi uraiani kaendelea na kazi zake kwa kuwa kaajiriwa basi kwake haikuwa ngumu sana, mke akajitahidi kulisha familia ndani week mbili tu kaanza kumsimanga MABESTE kwamba hajishughulishi anamtegemea tu yeye MABESTE anashangaa tu mke kaona haitoshi kamzunguka jamaa na akaanza Kutoka na mchizi wa MABESTE ambae kwa wakati huo yeye alikuwa fresh anajiweza, Ila wanawake mtuonee huruma hivi mnataka mwanaume yupi kati ya Hawa
-Mrefu,Mweusi,mweupe,Mwenye hela, Mpole,Mkali,Mcha MUNGU, mcheshi,Mwenye ndevu,Mwenye tege, Mwenye mashine,Mwenye shoo,Mwenye six-packs,Mwenye hela au maarufu?

Maana kwa Mimi mwanaume naweza nikataja sifa chache tu za mwanamke tumtakaye na wote tukaapriciate kwa mfano;Mwanamke wangu nataka awe na shepu nzuri, Akili timamu, Mtafutaji na Mcha MUNGU, Sidhani kama Kuna mwanaume hapa ana Cha kuongeza ila hapa ndo utajua tofauti yetu na wanawake ambao kwanza hawaeleweki wanataka nini.

Je, wewe kama mwanaume niambie kisa chako kilichofanya ukasema hawa viumbe hawaridhiki na hutokaa kuwaaamini
 
Mi msimamo wangu huwa ni mmoja siyumbishwi,nikisema no ni no ,nikimwambia usirudi kuniletea ishu hizi ndo hivo ,anapata nguvu wapi kuingilia maamuzi yangu,nikiona ushauri mzuri nitauchukua sifanyi kwa kumridhisha kama hawezi aondoke
 
Mwanamke unaweza ukawa unatoka jela pia akakuuliza umetuletea nini? Na ukitaka kujua wanawake sio wema kama una mjengo na familia we mchomekee mwambie nataka kuuza nyumba utasikia akisema "Unauza nyumba ukifa unataka niteseke na watoto?"

Ndivyo walivyo wanaamini sisi wanaume ndio tutangulia kufa..ni kuishi nao tu kwa akili!
 
Siku zote kwenye r/ship Invest what you are willing to lose

Hapa naamanisha ..km ni pesa bhac iwe ambayo haikuathiri ..km ni material things hali kadhalika ...coz hawa viumbe hawatabiriki ...

Kinachofanya sisi wanaume tuumie sana tukitendwa n investmest tunazowafanyia hawa ..washenzi
 
hawa viumbe natamani niwaandikie makala ndeeefu,lakini ni kama kazi bure.kuna wanaume wenzetu hawasikii hata uwaelezeje,wanaona wewe ndiye hujui au ulikosea sehemu yakakukuta unayowasimulia.wanaanza ulipoanzia upyaa.

wakati bible inasema tuishi nao kwa akili sijui kama kuna watu walielewa sehemu hii sawa sawa.
tunatakiwa kuishi nao kwa akili tu wala sio kitu kingine,ukitumia mapenzi,huruma,sijui staha shauri yako utajua mwenyewe mbeleni huko.

mwanamke ukimpenda akajua anakusumbua.

ukimuheshimu anakudhalilisha.

ukimwogopa anakudharau.

nachotaka kusema,mwanamke mpe sababu ya kukukosea.ataitumia kwa tahadhali sana au asiitumie kabisa,sasa wewe jifanye dactari wa mapenzi,utajua hakuna kitu unajua.
 
Wana ujinga sana.
 
Kuna jamaa alimfumania mpenzi wake jamaa akaamua kumove on ila stress zilikuwa kwenye Pete aliyomnunulia yule mwanamke ilikuwa milli of money alafu katika kuifuatilia mwanamke akamuambia aliipoteza.
 
hawa viumbe natamani niwaandikie makala ndeeefu,lakini ni kama kazi bure.kuna wanaume wenzetu hawasikii hata uwaelezeje,wanaona wewe ndiye hujui au ulikosea sehemu yakakukuta unayowasimulia.wanaanza ulipoanzia upyaa.

wakati bible inasema tuishi nao kwa akili sijui kama kuna watu walielewa sehemu hii sawa sawa.
tunatakiwa kuishi nao kwa akili tu wala sio kitu kingine,ukitumia mapenzi,huruma,sijui staha shauri yako utajua mwenyewe mbeleni huko.

mwanamke ukimpenda akajua anakusumbua.

ukimuheshimu anakudhalilisha.

ukimwogopa anakudharau.

nachotaka kusema,mwanamke mpe sababu ya kukukosea.ataitumia kwa tahadhali sana au asiitumie kabisa,sasa wewe jifanye dactari wa mapenzi,utajua hakuna kitu unajua.
naomba ufafanuzi pm
 
Back
Top Bottom