Kumtembelea Dr.ULIMBOKA ni KEJELI kuu...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Dr. Ulimboka hakulazwa kwakuwa ameanguka kwa presha alipokuwa Bungeni,Hotelini au kwenye Kikao cha Mawaziri.Amelazwa kufuatia mateso makali aliyoyapata kutoka kwa watu 'wasiojulikana'.Bado ana maumivu makali mwilini mwake.Anahitaji muda wa kutulia na kupokea matibabu ipasavyo kuokoa viungo na maisha yake.Kwenye chumba alimolazwa,yawapasa Madaktari tu wamshughulikie mwenzao na kiongozi wao.

Si vyema kumtembeleatembelea Dr.Ulimboka kana kwamba watu wanakwenda kwenye Maonyesho ya SabaSaba.Zipo sura zikionwa na Mgonjwa zinamtisha.Nyingine zinamhuzunisha.Zipo zinazomkasirisha.Kutishwa,kuhuzunishwa na kukasirishwa kwa mgonjwa mara kwa mara kuna maana kubwa.Kunaathiri matibabu yake.

Dr.Ulimboka aachwe apokee matibabu.Kwa hali aliyonayo,anahitaji faragha labda tu na familia yake.Dr.Ulimboka havutii machoni kwa sasa.Anasikitisha na kuhitaji maombi ya watanzania wote.Yeye si kiumbe adimu ambacho kinahitaji kuangaliwaangaliwa.Aachwe apate matibabu.Watu wasijitafutie umaarufu kwa kupitia mateso yake makuu.Apone.Na mwishio mwishoni aseme neno moja tu...
 
Hasa vyombo vya habari vinatafuta sifa na faida kubwa. Give him a break!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom