Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Katika Maisha kuna mambo tofauti sana yanafanyika kwa wanandoa yaan mke na mume. Kuna wakati mwanaume hufanya mambo yake bila kumshirikisha mke wake kama vile kununua viwanja, mashamba, kujenga nyumba, kununua gari na mambo mengine kadha wa kadha.
Jambo hilo lina mapungufu makubwa sana katika kusukuma gurudumu la maisha. Kwa mtazamo wangu wanawake ni watu wa Anasa sana, akipata pesa au akiona umepata pesa mwanaume kipaombele chake cha kwanza ni urembo hapo nazungumzia saloon, Nguo za bei kubwa, Simu za Gharama kubwa, Vyombo vya kisasa na vya gharama kubwa.
Kama hutomshirikisha kwa mambo ya kutumia pesa utajikuta unayumba nazungumza hivyo kwa mifano thabiti wakati wa kununua kiwanja nikaamua kumpa mwanamke pesa aweke kwa ajiri ya kiwanja kila nikipata mshahara nampa aweke ghafla nikamwona safari ya saloon amepunguza, Alikuwa ananunua mashuka mara kwa mara nikashuhudia miezi sita hajanunua chochote ndani hatimaye tukanunua kiwanja cha bei kubwa sana kibamba hondogo. Na katika kujenga nikampa jukumu hilohilo nikaona nishirikiane nanyi ndugu zangu wanawake wapeni majukumu ya kusimamia shughuri za maendeleo wanajali na kuheshimu pesa kama nini. Hata kutoa 5000 kununua matunda ya juice wanaona kama wanapoteza pesa. Ila ukiwatenga na kujifanya ufanye mwenyewe utafanikiwa lakini ilipobidi mjenge na kununua gari mtajikuta umejenga tu.