Pole sana Belinda! Kitu pekee tunachowezza kufanya ni kukupa moyo na kukufariji. Umefanya vizuri kulileta swala hili hapa kwani moja katika mbinu za kuponya ni kulizungumza hili na marafiki na jamaa zako. Kwa upande wangu, ninaungana na wale waliosema kwa namna moja au nyengine "Hata jambo baya lina uzuri wake", nikimaanisha kuwa "hukuwa unastahiki kuishi na mtu asiyejali kama huyo". Ni vyema kuwa hili limetokea mapema; Mungu kakuepusha na majanga mengi. Fikiria angekuja kukusaliti baada ya kufunga naye ndoa!, maumivu yake yangekuwa makali zaidi.
Baada ya kuondokewa, utapitia katika hatua hizi nne:
1. Kutoamini na kutokubali kilichotokea lakini ndio ukweli.
2. Kwa kuwa ndio ukweli, hili litakuuma sana,
3. Maumivu yataambatana na huzuni.
4. Mwisho utakubali matokeo na ukweli wa mambo. Ni maji yaliyomwagika.
Kwa ushauri jinsi ya "kukusanya vipande vya moyo uliovunjika", fanya baadhi katika haya:
- Kila unapowaza kuwa "Ninampenda na siwezi kuishi bila yeye", utakuwa unakumbuka mazuri tu uliyoyapata na mliyogawana kabla ya mambo kuharibika. Lakini kama unavyokiri kuwa "mlikuwa na matatizo yenu madogomadogo", ukweli ni kuwa hayakuwa madogo kama ulivyokuwa unafikiria. Yalikuwa makubwa lakini ukavumilia kwa sababu ulikuwa unapenda. Sasa ni wakati wa kuyafikiria haya kwa lengo la kukutoa katika mawazo ya kuwa kulikuwa na mazuri tu. Hii itakusaidia umuone kwa jicho jengine.
- Kimbilio lako la mwanzo iwe paketi za tisues - lia kadiri uwezavyo. Jifungie chumbani kwa muda unaotaka, hata masaa 24 mfululizo, lakini ukitoka hapo, jufute machozi na kumbuka "Maisha yanaendelea". Kama ulivyokwisha shauriwa kabla, kimbilio lako la pili iwe marafiki, wazazi, ndugu au jamaa wa karibu. Hakuna tiba nzuri kama kupata bega la kulilia, hasa likiwa la mama, dada, au rafiki. Pamoja nao au peke yako, tembea/tembeeni sehemu za wazi. Epuka vilabu kwa kipindi hiki.
- Kama una uwezo, tafuta mnyama wa nyumbani, hasa mbwa au paka. Huyu atakupa mapenzi yote bila kukudai saaaana zaidi ya mlo wake na kumjali.
- Jiunge na kozi, masomo au amali ambayo daima ulikuwa unahamu uifanye. Muda wako mwingi utakuwa unashughulika na hili badala ya kukaa kumfikiria au kusubiri miujiza...AMESHAOA,hakufai, hakustahiki.
- Fanya kazi za kujitolea kama vile kuwahudumia wazee, watoto na makundi hitaji.
KANUNI YA DHAHABU: KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUUGUZA, USIMSOGELEE; USIMTAFUTE; USIMRUHUSU KUTAFUTA FARAHA NA WEWE NA KUMWACHA AKUMWAGIE UONGO
...- Kila unapowaza kuwa "Ninampenda na siwezi kuishi bila yeye", utakuwa unakumbuka mazuri tu uliyoyapata na mliyogawana kabla ya mambo kuharibika. Lakini kama unavyokiri kuwa "mlikuwa na matatizo yenu madogomadogo", ukweli ni kuwa hayakuwa madogo kama ulivyokuwa unafikiria. Yalikuwa makubwa lakini ukavumilia kwa sababu ulikuwa unapenda. Sasa ni wakati wa kuyafikiria haya kwa lengo la kukutoa katika mawazo ya kuwa kulikuwa na mazuri tu. Hii itakusaidia umuone kwa jicho jengine....Binafsi nafikiri kuna kitu kilichosababisha jamaa kukuacha na kwenda kumwoa mwingine. Kila kitu kinatokea kwa sababu. Inaonyesha umeumia sana japokuwa kwenye maelezo yako unaonyesha kuwa hukuyasababisha haya...
Urafiki wa nini na mtu kama huyu?Mfanye rafiki yako wa kawaida, mpigie simu na mwambie kuwa umemsamehe na anza kuwasiliananaye kama mtu wa kawaida. utapona.
Mfanye rafiki yako wa kawaida, mpigie simu na mwambie kuwa umemsamehe na anza kuwasiliananaye kama mtu wa kawaida. utapona.
Kwa faida ya wengi walio/wanao/watakao/pitia hali kama hii, tungeomba mtumie lugha ya kiswahili...tunathamini michango yenu...Tafadhali..mtutafsirie na sisi wengine,
Mfanye rafiki yako wa kawaida, mpigie simu na mwambie kuwa umemsamehe na anza kuwasiliananaye kama mtu wa kawaida. utapona.
atampata ndio ila sio kama yule....changamoto za hapa na pale.... Huenda kwa mwenzio zilikuwa sio changamoto bali matatizo ndo maana kakutema. Tulia hii Dunia haikosi mwenza itakupatia tu.
Hivi ikitokea umempoteza mtu unayempenda unaikabili vipi hii hali?
Yani hata sijui nisemeje, nimechoka kwa mawazo hadi akili kumfikiria sana huyu mtu.
Roho inaniuma na ninakumbuka sana vitu vingi tulivyofanya tukiwa wote. Nahisi nilimpenda sana na kumpa kipaumbele zaidi kuhakikisha tuna penzi imara na lenye muelekeo japokuwa changamoto za hapa na pale hazikukosekana.
Lakini sijui kwa nini amenifanyia hivi? Na hii ndiyo inayonichanganya zaidi akili kwa sababu sipati jibu..Kifupi, ni kuwa ameoa (naomba nisielezee zaidi).
Ooh!..kweli nahitaji ushauri wenu juu ya kuendelea na maisha yangu bila kumkumbuka huyu mtu..japokuwa ukweli ni kuwa siwezi kumsahau 100%!!
I'm so confused, stressed & deeply hurt!!..
Apumzike kwa muda ili apone jeraha la moyo alilopataand remember in life there are three things
1. things you can fix
2. things others can fix and
3. things God can fix
and in your case you need God to fix your situation , all the time pray pray pray, according to your faith.
God Bless u
Ndugu yangu asante kwa maono yako. Naomba nikwambie kitu kuwa mimi ni mtu mzima, ingekuwa tumekwaruzana na kuachana wala nisingejisikia hivi. Mimi siyo malaika ila sioni kitu gani nimechangia cha ajabu mpaka kushtukizwa hili jambo. Pia kumbuka angeniambia mbona ningeumia na kujiandaa kiakili hatimae kukubaliana na hilo suala mana nisingeweza kumzuia hata kama nampendaje.
Nimejaribu kutoa short story mana nimeshindwa kuielezea kiundani zaidi kwa vile imetokea karibuni. Nilivyoiweka hii issue ni kuwa nimeshtushwa na jambo la mwenzangu kuoa wakati tulikuwa serious sisi kuoana mwishoni mwa 2011, sijui imenipata. Sasa kama alikuwa na tatizo najiuliza kwa nini hakunishirikisha? kama vile kuniambia tisingeweza kuwa wote au kampenda mtu mwingine na hivyo mimi na yeye basi. simpo as that!
Kweli tulikuwa serious na sijawahi kupinga jambo lolote kuhusu ndoa alivyogusia na tukakubaliana..unajua nini, natamani mwenyewe nipate jibu la hili swali ila sina kwa sababu ukweli anaujua mwenyewe jamaa. Hata kama angeniumiza kuambiwa ukweli ila ungesaidia sana na ningekabiliana nao na maumivu yake.
Shukrani kwa mtazamo wako..