Kumpenda mtu unaangalia nini?

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
496
Reaction score
379
Mapenzi ya sasa yana mtihani mgumu sana, kumpata akupendae kwa dhati toka rohoni mwake ni ngumu japo wapo wachache sana siku hizi.

Kwa mfano msichana anaweza kumpenda mvulana kutokana na mambo yafuatayo:

1. Maneno ya Mvulana huyo.

2. Sura na mwonekano wa mvulana.

3. Pesa za Mvulana.

4. Cheo cha baba/mama wa mvulana.

5. Nafasi ya wazazi wa mvulana katika eneo husika.

6. Nafasi ya mvulana katika eneo husika.

Hiyo namba tatu, chukulia mfano mvulana anafanya kazi iwe serikalini au private company, ikiwa atamtongoza msichana au kumchumbia binti atakubali haraka sana.

Hiyo namba nne, chukulia mfano mtoto wa Rais au waziri amtongoze au amchumbie binti unadhani binti atamkataa? hatakama binti hampendi ila atajitahidi sana aonyeshe kuwa anampenda!!

Hiyo namba sita, chukulia mfano wasanii, mfano Diamond au Dimpoz unadhani akimtongoza au akimchumbia binti atakataa?

Kwa ujumla mapenzi ya dhati cku hizi hamna tena! Fikiria unamuoa mwanamke lakini bado atamkumbuka mpenzi wake wa zamani na wakati mwingine anaweza kugegedwa naye! labda ukute mwanaume huyo ana hofu na ndoa za watu.

Kiujumla, Kwa kuwa hali ndo hii na haitaweza kubadilika basi itabidi twende hivyo hivyo, mabinti wa kisasa wamekuwa wadhaifu sana katika kukabiliana na vishindo na purukushani za wanaume, na chanzo huwa ni wanawake, unakuta mwanamke/binti anajenga mazingira ya kutongozwa, na wanaume baadhi huwa hawafanyi kosa.

Tubadilike!!
 
Kubadilika labda no 3 isiwepo kuwe na barter system.
 
Hivi ulimpata mchumba?? Mbona hutupi mlisho nyuma??? Tuandae matumbo???
 
wanaume ndio chanzo cha umalaya, ikiwa wanaume wataamua kubadilika wanawake hawawezi kuwa malaya tena kwani hawatatongozwa na wakitongoza watakataliwa.
 
hiyo namba 4 na 5 nilishakutana nayo ila nilipomkubali sikuwa najua kwamba ni mtoto wa kigogo nilikuja baada ila alinishinda kwa tabia zake za kudeka nikampiga chini bila kujali hiyo position ya baba yake, hiyo namba 6 kwangu ni never kutoka na mtu anaeitwa msanii hata kama angekuwa na mali za kununua kisiwa
 
Yote sawa ila mi napendaga ma wowowo
 
Kwa mtazamo wangu hivyo ni vivutio (attraction) upendo waweza kuja baadae au usije mkawa mnapotezeana muda tu.
 
....Wangu hapendi pesa, yaani yeye ukimtamkia pesa anachukia sana, teh!!!
 
To be honest,Me naangalia pesa,hasa zikiwa zake....akini-approach ht km sim-feel kivile nitajikaza ,...mapenzi hayo ntaangalia mbele ya safari
 
Mabinti na wanawake wa humu JF inaonekana wachunaji wazuri eeh! Eeh Mungu naomba uniepushe na kikombe cha mademu wa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…