Kumpenda mtu asiyekupenda

Kumpenda mtu asiyekupenda

Mkono Wa Nyani

New Member
Joined
Jan 13, 2019
Posts
2
Reaction score
7
Umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.

Lakini ukitizama WhatsApp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status.

Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu?
Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?

Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote.

Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae.
Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!

Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande!
Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.
Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hua nawaza niwaweke ufahamu, watambue kua wako wengi na lengo ni kuwatesa kwa zamu...niwaumize ili wapeleke salamu....nashangaa warembo wanavyongoja pete kwa hamu
IMG_20200330_095649_310.jpeg


It's Scars
 
Wangu mna roho 7 kama za paka dadeki,

Pisi juzi kati namwambia tuonane akasema hawez saivi yuko amepata anae mpenda, nikamwambia hongera na asante.

Nakutana nae njiani baada ya week buyu, ananitext badae mbona nimemtenga nilimjibu staki unitie majaribu kwa wake za watu kwa maana na mm nisha pata anae nipenda,

Alishia kusema nilikuwa nakutania jmn sio kweli, na mm nikamwambia huwa sitanii mm nisha pata mwingine, ikawa end.
 
Giving someone all your love is never an assurance that they love you back.Don't expect love in return..Just wait for it to grow in their heart.But if it doesn't,be content it grew on yours.
 
Wangu mna roho 7 kama za paka dadeki,

Pisi juzi kati namwambia tuonane akasema hawez saivi yuko amepata anae mpenda, nikamwambia hongera na asante.

Nakutana nae njiani baada ya week buyu, ananitext badae mbona nimemtenga nilimjibu staki unitie majaribu kwa wake za watu kwa maana na mm nisha pata anae nipenda,

Alishia kusema nilikuwa nakutania jmn sio kweli, na mm nikamwambia huwa sitanii mm nisha pata mwingine, ikawa end.
We KE au ME?
 
Kupendana kijinga jinga mamna hii sio salama kwa afya ya akili nafsi na roho.take your time.Get urself busy with something valuable
 
Back
Top Bottom