ideal safarimate
Member
- Mar 17, 2016
- 71
- 91
Kwa muda takribani wa wiki tatu sasa wabunge wa upinzani "wamegomea" vikao vyote vya bunge vinavyoongozwa na naibu Spika Tulia Atson wakiwa na malalamiko ya kwamba anatumika kubana demokrasia ya bunge.
Ikumbuke kwamba hii si mara ya kwanza kwa wabunge wa upinzani kuchukua hatua kama hii, kiuhalisia mara nyingi (kama sio mara zote) hii ndio imekua kama hatua ya mwisho (last resort) ya wabunge wa upinzani pale wanapoona kutotendewa haki au kutokubaliana na maamuzi ya kiti/uongozi wa bunge.
Tofauti pekee safari hii wameenda hatua moja mbele zaidi,kuanzisha kampeni ya kumng'oa naibu spika kwa kuja na azimio la kumpigia kura ya kutokua na imani nae.
Katika mifumo ya kibunge wale wachache mara zote huwa na haki ya kuonyesha kutoridhishwa na jambo fulani kama boycotting,filibustering n.k
Kwa hapa nitajaribu kujadili mantiki,tija ,athari na maoni yangu kuhusu hatua zote mbili zilichokuliwa na upinzani:
MGOMO
Kumekua na mjadala mkubwa kuhusu hatua hii huku wapo baadhi ya watu wakiwa na maoni tofauti hasa kuhusu mgomo huu wakiona wabunge hawa hawatendei haki wananchi waliowatuma kuwawakilisha kwa kushindwa kuhu dhuria vikao vya bunge.
Kwa upande wangu naona wenye maoni hayo wako sahihi hasa ukizingatia asimilia kubwa ya wananchi uelewa wao wanaamini kazi ya ubunge(hasa katika eneo la uwakilishi bungeni) ni kuhudhuria vikao,kuchangia na kuuliza maswali.
Lakini kiuhalisia hiyo sehemu ndogo tu ukiangalia upana wa kazi ya ubunge.
Mfano kuna vikao kama vya kamati za bungeni ambavyo ndio chanzo cha agenda/maamuzi na maazimio ya kibunge.Mfano hivi sasa tuko kwenye bunge la bajeti,kuna kamati mbalimbali za kisekta ambazo hujadili na kutoa maoni ya wabunge katika bajeti za sekta husika,ukweli ni kwamba kama mbunge ameshindwa kushaawishi mchango wake kupitishwa na wajumbe(wachache) wa kamati yake ndani ya kamati husika ni ngumu zaidi kuweza kushawishi bunge zima kupitisha.
Vilevile kama msingi wa uwakilishi bora ni kuuliza swali na kuchangia bungeni pekee, ni asimilia chache sana ya wabunge ambao hutimiza hili kwani wengi wa wabunge(hasa wa chama tawala) huwa hawachangii lolote na hata wale wachache wanaochangia huongozwa zaidi na msimamo wa kichama badala ya utashi wao na maslahi ya wananchi.
Lakini pamoja na sababu lukuki za kugomea vikao vya bunge kuna maswali muhimu ya kujiuliza
-Je, baada ya kua kutoka nje ya bunge imetumika mara kadhaa,imekua na tija gani kusukuma hoja za upinzani zinazolalamikiwa?
-Je, uwezo wa wananchi kuelewa sababu na umuhimu wa hatua ya kugoma umezingatiwa?
-Kwa aina ya uongozi wa bunge na serikali ya sasa(yenye kupenda kusifiwa tu) hawatoona hii kama ndio "ideal situation" ya kuendeleza propaganda zao ndani ya bunge huku wakikwepa kuhojiwa maswali magumu ambayo yangeonyesha kasoro zao lukuki za kiungozi?
AZIMIO LA KUMNG'OA NAIBU SPIKA.
Kwanza niweke wazi naamini pamoja na miaka yote nafasi za uspika na naibu zikishikwa na wanasiasa kutoka CCM kutokana na mfumo wetu, bunge hili hali hii imekua mbaya zaidi(hasa kwa nafasi ya naibu spika).
Hali hii ya juhudi za serikali kuingilia na kua na mpango maalumu wa kulishika bunge ilianza kuonekana kwenye mchakato wa kumpata mgombea wa naibu spika kwani ndani ya siku mbili alichukua fomu ya uspika,akashindwa kisha akateuliwa harakaharaka kuwa mbunge na raisi na kuchukua fomu ya unaibu spika huku wagombea wengine wakilazimishwa kujitoa na kubaki yeye kama mgombea pekee.
Hii ilionyesha dhahiri ni mteule wa raisi (executive) kwani there is no two coincidences hali ambayo mtu yeyote(rational) angeona inaenda moja kwa moja kuathiri uhuru wa bunge.
Lakini pamoja na haya yote azimio la kumng'oa kwa kumpigia kura ya kutokua na imani nae linaacha maswali mengi;
-Je, kuna uhakika wa kua na kura za kutosha kupitisha azimio hilo? hasa ukizingatia idadi ya wabunge wa upinzani ni ndogo,
-Kuna mpango wowote au idadi yoyote ya wabunge wa CCM waliotoa uhakika wa kuunga mkono azimio hilo?(not likely)
-Kumefanywa tathmini ya athari ya siasa za kibunge iwapo azimio hilo likishindwa ?
-Je, iwapo mpango huo utashindwa,nini kitafuata?kurudi tena bungeni ama mgomo kuendelea kwani wameshatangaza kutokua na imani nae?
HITIMISHO
Pamoja na kuelewa "spirit" ya kambi ya upinzani kuhusu hatua zote mbili za kugomea na azimio la kumng'oa naibu spika hesabu zote za mafanikio yake zinakataa.
Nachelea kusema msingi wake umebebwa zaidi na matamanio(idealism) na si uhalisia wa hali halisi ya kisiasa ndani na nje ya bunge.Kiukweli ni kwenye "ideal world" tu ndio naona mafanikio ya haya yote.
Nimebaki na imani tu kwamba viongozi wa upinzani would be smart enough to have an exit strategy incase of failure(which is most likely)!
Vinginevyo haya yote yataenda kuathiri zaidi uendeshaji wa bunge na ajenda za upinzani kwani uongozi wa bunge na serikali utaona upinzani umetumia karata zake zote na kushindwa hivyo watazidi kukanyaga na kutingisha uhuru wa muhimili huu muhimu.
IN POLITICS YOU DON'T PICK A FIGHT YOU CAN'T WIN!