G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Hakuna sababu nyingine ya kumkaimisha Jaji mkuu wa Tanzania ofisi zaidi ya kumuweka kwanza katika mizani ili kuona kama ataendana na matakwa yako ndipo umpe nafasi kamili.
Kumuapisha Jaji mkuu kukaimu ofisi kwenye utawala unaoonyesha kila dalili ya ukandamizaji wa uhuru ni kumrubuni kwanza kufuata mkondo wako ndipo umpe zawadi kamili! Hii ni dalili nyingine ya utawala unaominya uhuru kwa nguvu zote.
Mahakama kwa sasa zinatoa hukumu tata kwenye kesi za wanasiasa, hukumu ambazo zina kila dalili ya shinikizo fulani. Kwa hali ya kutaka kufurahishwa ni kwa nini rais asikaimishe ujaji mkuu?
Mchakato wa kumteua Jaji mkuu wa Tanzania ni wa kimfumo, napingana na wale wanaodhani kuwa hapakuwepo na maandalizi ama mchakato wa kumpata Jaji mkuu na hasa ikizingatiwa kuwa mtangulizi alikuwa anajiandaa kustaafu. Ama rais alitengua mchakato huo ndipo akaja na wa kwake wa kukaimu?
Ni dalili mbaya sana kumuweka Jaji mkuu kwenye mizani na hasahasa kwa kipindi hiki ambacho tunathubutu kusema kuwa mahakama imekanyagwa na utawala wa rais Magufuli!
Haya ndugu Ibrahim, nenda kakaimu pindi utakapomfurahisha mteuzi basi utapewa mamlaka kamili! Dalili mbaya za uongozi ndizo hizo ambazo kila uchwao tunazipigia kelele!