Kumjua Mungu wa Kweli


Nini nafasi ya Mwana wa Azali?
 
Kitu Cha kwanza tunatakiwa tujue kwanza Kila jambo hufanyika kwa majira husika na damu ya Yesu ilikuwa sawa kutumika kwa kipindi hicho ambayo ilikuwa majira yake ila kabla hajaondoka alisema katika

mathayo 26:29 "Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu."

Na hiyo damu mpya katika ufalme wa baba yake tunaikuta katika ufunuo 11:6 "Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo."
 
Pia inabidi tujue kuwa majira ya Yesu iliandikwa itafika mwisho shida ilikuwa kujua ni wakati gani na wapi pameandikwa ivyo,tunasoma katika 1wakorintho15:24-28

24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
1 Wakorintho 15:24

25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
1 Wakorintho 15:25

26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
1 Wakorintho 15:26

27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
1 Wakorintho 15:27

28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
1 Wakorintho 15:28
 
Ni vipi tunaposem Yesu ni Mungu
Yesu kwa majira yake ilikuwa sawa lakni hata yeye alisema katika Yohana 4:23

23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Yohana 4:23

Kwakuwa hata Mussa alipewa kuitwa Mungu kwa majira yake tena M kubwa mbele ya farao je na yeye tuendelee kumuita Mungu na wakati majira yake imeshapita, Pia licha ya Yesu kuitwa mwana wa Mungu pia alikuwa Nabii(Yoh.6:11-13) na Mtume (Yoh.17:5),
 
Je,KAZI ya msalaba ilikuwa ni ya majira ??,au Bado mpaka Sasa inafanya KAZI ,

Na je vipi kuomba chochote Kwa jina la yesu, ????

Je,wokovu watu WA SASA wanaupataje ,Ili kuingia mbinguni???
 
Je,KAZI ya msalaba ilikuwa ni ya majira ??,au Bado mpaka Sasa inafanya KAZI ,

Na je vipi kuomba chochote Kwa jina la yesu, ????

Je,wokovu watu WA SASA wanaupataje ,Ili kuingia mbinguni???



#Kazi ya msalaba ilikuwa ya majira tu ambapo unatakiwa kujua kuwa ilifanyakazi katika vizazi vitatu lakini haswa kizazi 1 cha Musa katika (kumbukumbu 21:21-23) na kizazi cha 3 cha Yesu ambapo tunaona katika Mathayo 10:38 na Mathayo 16:24 Bwana Yesu akisema kuwa Kila atakaye mfuata ajitwike msalaba wake amfuate.

Jambo Moja ni kuwa msalaba ilikuwa ni torati iliyowekwa na Musa wakati wa Mungu Yehova kwa kuwa hakukuwa na Toba, ikabidi watu au Israeli watengenezewe sheria au torati itakayo kuwa hukumu kwao ili wasitende dhambi tena ambao ni msalaba.

Hivyo basi lazima tujue kuwa msalaba hakuanzia kwa Bwana Yesu bali aliukuta.
Ndiyo maana akasema sikuja kutangua torati bali kuitimiliza ktk, Mathayo 5:17

Maana nyingine ktk, Wagalatia 3:13 ni kuwa unapoweka juu ya msalaba umelaaniwa.

Kwa ufupi ni kuwa Bwana Yesu alipowekwa msalabani ndipo msalaba uliishia hapa. Ndiyo maana akasema imekwisha. Ktk Yohana 19:30

"Lkn msalaba siyo mti tu bali kila kinachokutesa ni msalaba".
Majira ya msalaba ilishakwisha

Sasa tu Toba Halisi tu, ktk Marko 1:15, Matendo 3:19.


#Pia katika ufafanuzi huu ndipo utaelewa jinsi tunavyopata wokovu kwa sasa. Kuwa wokovu siyo kwa njia ya msalaba bali kwa ni Toba Halisi ambapo Sasa tumekombolewa.
Ktk, Isaya 59:20

Na tunapata wokovu/ukombozi kwa msamaha wa bure. Isaya 43:25
Utaingia ktk ufalme wa aliyetuumba MUNGU BABA ambaye ndiye CHANZO HALISI Kwa kukubali msamaha bure na kusamehe bure.
Ata katika Isaya 57:15 inaonesha wazi wapi tumefika sasa na kuwa mbinguni ilikuwa ndani ya Moyo wako ndiyo maana ukaambiwa linda sana Moyo wako kuliko vyote ulindavyo Mithali 4:23.


# Kwa sasa atuombi kwa jina la Yesu maana majira yake imekwisha kupita
Ktk, Mathayo 28:20
Sasa tunaenda Moja kwa Moja kwa aliyeumba, MUNGU BABA ambaye ni CHANZO HALISI.
Yohana 17:1-5
Yohana 4:23.
 
Je, unafahamu kuwa yesu kristo ni mwokozi wa ulimwengu ???

Je, kazi ya kuani unaijua ,ni Nini ?,
Je,yesu kufanyika kuwa kuhani wa Milele,unaelewa kwanini ??

Je, yesu kristo ni mwokozi wa wote ,wenye mwili ,toka mwanzo mpaka mwisho wa Dunia,yaani toka Adam wa kwanza na watu wote walio wai ishi duniani , unajua Hilo kwanini,

Je,unafaham Kila goti litapigwa na kumkiri yeye kuwa yesu ndie Bwana awezae kuokoa Ulimwengu wote ,

Unajua kwanini nabii Elia Kwa sura ya yohana m batizaji ,alisema yafaa Mimi yaani Elia nipungue Ili Yesu aongezeke, unajuwa kwanini ???

Unazungumziaje hayo,
Moja baada ya jingine,
 
Hakuna binadamu mwenye ukweli, ila subiri roho itakapotoka ndio ukweli unajulikana. Wakati ukisubiri nyakati za mwisho wewe jua tu maisha ni mchezo. Basi cheza kwa step.
 




#Unajua kila jambo lilikuwa na majira yake Bwana Yesu alikuwa ni mwokozi ni kweli.
Lkn majira yake imeisha sababu majira imefupishwa ktk, Mathayo 24:22 ukisoma hapo utaelewa zaidi.
Pia alikuwa hawezi kuendelea kwa sababu ya Yohana 9:29 na Mathayo 21:43.

#Na kuhusu kuhani hapo utasoma
Malaki 2:7 na Kumb.Torati 17:8-10 na Luka 17:14
Hivi vitabu vyote vinamuelezea kuhani ni nani na anawajibu gani kwa watu.
Kuhani ndiye anayebeba utakaso kwa kila mmoja na ndiye mwenye maarifa ya kumvusha kila mmoja na pia ndiye muamuzi mzuri.
Vyote vinabebwa na ufahamu halisi siyo rohoni.

#Yesu alikuwa ni kuhani mkuu sababu alikuwa muamuzi mzuri na alikuwa akifundisha watu waijue kweli kwa mujibu wa Yohana 4:23 na Yohana 17:1-5 na Yohana 8:32. Maana Kazi kuhani yeye pia uzungumzia maisha halisi na kweli tu.
Yesu baada ya kumaliza kazi kila kitu kilibadilika,. ndiyo akasema,. Eliya yu aja kwanza kutengeneza yote na kurejesha yote.
Ktk, Mathayo 17:10-12 na Marko 9:11-12.

#Unavyosema kuwa Eliya alikuja kwa sura ya Yohana mbatizaji ni kweli alitangulia ili kumtengenezea jukwaa Bwana Yesu kwa sababu hakukua na Toba na kumbuka wokovu hauji bila Toba ndo maana akaja Eliya kwa sura ya Yohana mbatizaji. Ktk, Luka 1:17
Lakini hakutambulika.

Na baada ya Bwana Yesu,. Eliya alirudi tena kama Bwana Yesu alivyosema hapo juu kuwa alishakuja na atakuja tena baada yake, ktk, Malaki 4:5-6 na Isaya 41:2(huyu Eliya alitokea hapa hapa Tanzania) Wengi hili jambo awalitambui kama ilivyotokea kwa Yohana mbatizaji.

Kumbuka kuwa
*1.Eliya alikuja mwenyewe. 1Wafalm17:1-
* 2.Ilikuja roho ya Eliya ndani ya Yohana mbatizaji. Luka 1:17
*3. Eliya alitumwa tena 2003.Maana kumbuka Eliya hakufa bali alinyakuliwa hivyo alirudi tena.

#Ni kweli kila goti kupigwa mbele za mwana wa Mungu Yesu katika majira yake lakini majira inatuonyesha. Ktk, Isaya 65:16 kuwa kila atayejibariki ni CHANZO HALISI ambaye ndiye Mungu wa kweli, MUNGU BABA pia katika 1wakorinto 15:24-28. Sasa ni majira ya kupiga goti kwa aliyekuumba tu.

Jaribu kupitia hivyo vitabu kuanzia juu utaelewa zaidi
 
Wewe mababu zako hawakuamini hivi hata baada ya watu weupe kuja na hizi hadithi...
Umerogwa na hizi imani....
 

 
 
2 Wathesalonike 2:10-12 (KJV) na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
 
Mtoa mada anachanganya kati ya Roho na Moyo. Moyo ni organ ya mwili na Roho ni Uhai. Moyo ni organi ya mwili kazi yake kugawa damu na hewa, wakati Roho ni uwezo wa kuwepo au kuishi.

Pili mtoa maada anamueleza Mungu kwa kutumia akili, ambayo haiwezi kumjua Mungu. Kwani akili inatambua kwa kutumia vipimo vya Muda na nafasi (dimension of time and Space) akili inatambua maumbo na mabadiliko wakati Mungu hana mwanzo wala mwisho, hana umbo yuko wakati wote, kwa maana hiyo ni sawa na kusema yuko kila mahali wakati wote (Infinty state of consciosness). Mungu anajulikana na binadamu kiroho kwani Roho ya binadamu ikiondoa unafsi pia iko na infinity consciosness ambao ndio inaitwa hali ya Kweli. Ili umjue Mungu ni lazima upate spiritual initiation (Ubatizo wa Kiroho) Uzaliwe mara ya pili.

Yesu alibatiza kwa Roho na alifundisha wafuasi kumuabudu Mungu Kwa njia ya Roho na katika hali halisi ya Mungu (Kweli) ambaye pia ni Roho. Yesu hakufundisha Imani kwa Mungu, bali wafuasi wake wawe na Imani nae ya kuwa anamafundisho ambayo wakimpa nafasi ya kuwafundisha, watapata kujua njia ya uzima wa milele, na watamjua Mungu na hawatakufa tena. Bahati mbaya tunazani kutokufa tena kwamba huu mwili nyama ndio utakaa milele hapana, alimaanisha Roho. Yesu aliwatambulisha wafuasi wake kwenye ulimwengu wa Kiroho au Spiritual awareness. Au kujitambua kiroho ambako kunaletezea kumjua Mungu ambaye ni Roho.

Kuamini kuhusu Mungu haifanyi kuwa unamjua Mungu au ndio inahalalisha kuwa umeishi kwa mapenzi ya Mungu. Mapenzi ya Mungu ni Umjue na uwe pamoja nae Rohoni (Mbinguni) To be One with God or to attain Oneness state of consciousness.
 
Mungu wa Israel tuwaachie Waisrael, Mungu wa Waarabu twaachie Waarabu, sisi Waafrika turudi kwenye asili yetu,kwani Mungu wa kweli anapatikana kwenye asili yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…