Kumiliki gari Tanzania kumegeuka kuwa ng'ombe wa serikali

akazuba

JF-Expert Member
May 16, 2014
533
484
Wanabodi Salaam

Huwa najiuliza huu ukamuliwaji kwa wamiliki wa magari umetokana na nini?

Ushuru bandari juu, motor vehicle kila mwaka juu, mafuta juu maana kila mradi unaokwama kupata fedha anaangaliwa mmiliki wa gari achangie kupitia ushuru wa mafuta. Hivi think tank wa vyanzo huona magari tu?

Hapo bado halimashauri nazo zikudake kwenye parking mpaka maeneo ya umma mfano pale cocobeach napo ulipie kisa umeingia na gari. Bado wapiga noti wanaoshinda tenda za ukusanyaji ushuru nao wanakupiga tu, tena ukiwa mmbishi breakdown hiyo inaitwa.

Bado wazee wa "hela ya kiwi" nao wanashindana kila uchao na TRA kumkamua mwenye gari! Hata kwa vijikosa vya kupeana maelekezo. Na sasa hivi ukijikakamua kwamba ujitete unalazwa mahali salama.

Spare nazo juu kisa mamlaka za mapato zinawakamua wafanyabiashara ya vipuri vya magari.

Bado waosha vioo barabarani, list ni ndefu mno but bottom line kunakitu hakiko sawa kwenye hii nchi kuhusu umiliki wa gari\magari.
 
Ndio sababu serikali imeweka malengo yake ya kuhakikisha public transport inakuwa transformed ili kukidhi mahitaji ya taifa. Kiherehere cha kwenda na gari kila mahali ambako public transport ya uhakika ipo itakuwa ni hadithi. Haya magari yanaongeza pollution tu.

Kuhusu swala la kodi Wacha wenye magari walipe tu, maana hakuna wa kuwalipia, Serikali haiwezi kutekeleza malengo yake kwa kutegemea kodi kutoka kwa walalahoi na walipa kodi wa hali ya chini pekee, kuwaacha wanaoishi kifahari kutokuchangia kwenye maendeleo ya nchi hii haiwezekani. Walipa kodi wakubwa ambao wengi wao wanakwepa kodi lazima walipe hakuna namna, ukitaka gari nzuri lipa kodi, huo ndio mwendo wenyewe.
 
Hahaha unakaribia kuwa Bashite kwa maoni haya.

Back
Top Bottom