Kumiliki gari bovu huchangia msongo wa mawazo

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,408
Katika watu ambao nawaheshimu ni wamiliki wa magari mabovu;

Utafiti uliochapishwa katika jarida moja nchini Uingereza unaonesha kwamba mtu mmoja katika kila watu 10 wanaomiliki magari mabovu hukutwa na ugonjwa wa presha. Nimejaribu kutafakari utafiti huo, nikakumbuka gari yangu ya kwanza kumiliki ilivyokuwa kimeo.

Kila mmoja ana history yake katika gari yake ya kwanza kumiliki. Gari yangu ya kwanza kununua mkononi, ilivyonitesa kisaikolojia, ilikuwa ni mark II grande used, ile gari kwakweli ilikuwa yataka moyo, nilikuwa natembea na lita 20 za Maji kwenye buti, ilikuwa inachemsha hatari, maprug yalikuwa yanamis sana, yaani ile gari ilikuwa haipiti siku tano sijaenda gereji; ile gari mwisho wake niliiuza laki 8 ilala wakakata screper.

Tangu kipindi hicho nikimwona mtu anagari bovu huwa namheshimu sana.
 
Kwa magari au mashine za kazi, nadhani ni vyema kununua kitu kikiwa kipya. Vitu used pasua kichwa sana maana unakuwa kama unavaa historia ya mtu.
 
Back
Top Bottom