ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,552
Kuna tatizo hili ktk Makazi hasa yaliyo sehemu pembezoni mwa Jiji ama maeneo yenye nyumba chache.
Kuna report za watu kuvamiwa usiku na makundi makubwa ya vibaka, wahalifu wakiwa na silaha aina mbalimbali.
Linavamia kundi la watu takriban 30 wanapora, kupiga watu, kubaka na mwishowe wanatoweka na mali na huku wakiacha uharibifu mkubwa.
Jeshi la Polisi tunaomba juhudi zenu kwa hili kutuhakikishia ulinzi kwani ni moja ya jukumu lenu kubwa kwetu.
Baadhi ya Maeneo athirika ni
- Chamazi
- Mivumoni
- Chanika
- Kijichi/Miande
- Msongola
- Bangulo
- Mbande
- Majohe
- Baadhi ya maeneo ya Kigamboni
Inafikia mahali mtu amemaliza nyumba yake pahala anashindwa kuhamia kuhofia usalama wa mali na familia yake.
Chonde Kamanda wetu Sirro changamoto ipo mikononi mwenu.