Kumekucha Korea, nyambizi kubwa ya mmarekani yawasili

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_95773344_8d91ba22-dfe2-40fb-b189-54a95d1cdf13.jpg

Nyambizi ya jeshi la Marekani imewasili katika pwani ya Korea Kusini huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au silaha za nyuklia.

Meli hiyo kwa jina USS Michigan, ambayo ina uwezo wa kushambulia kwa makombora, inatarajiwa kujiunga na kundi jingine la meli za kivita zinazoelekea eneo hilo, zikiongozwa na meli kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson.

Korea Kaskazini inaadhimisha miaka 85 tangu kuanzishwa kwa jeshi lake Jumanne.

Miaka ya nyuma, imekuwa ikiadhimisha siku hiyo kwa kuzindua makombora na silaha nyingine.

Wasiwasi umeongezeka wiki za karibuni kutokana na Marekani na Korea Kaskazini kujibizana vikali na kutoleana vitisho.

Hayo yakijiri, katika tukio ambalo si la kawaida, bunge lote la Seneti nchini Marekani limealikwa kwa kikao cha kupashwa habari kuhusu Korea Kaskazini siku ya Jumatano katika ikulu ya White House.

Nyambizi ya USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia na hubeba makombora aina ya 154 Tomahawk na wanajeshi 60 pamoja na meli nyambizi nyingine ndogo, gazeti la Korea Kusini la Chosun Ilbo limeripoti.

Meli hiyo inatarajiwa kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi pamoja na kundi la meli zinazoongozwa na Carl Vinson, kundi ambalo lilitumwa eneo la Korea kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani.

_95774377_cae785aa-d731-465b-961a-cad2733ceebb.jpg

Meli hizo za kivita wakati mmoja zilizua utata baada ya suitafahamu kuhusu iwapo zilikuwa hasa zinaenelekea eneo la Korea.

Lakini maafisa wa jeshi la wanamaji la Marekani kwa sasa wamesema zinaelekea eneo hilo kama ilivyoamrishwa.

USS Carl Vinson mwanzoni ilikamilisha mazoezi na jeshi la Australia na kisha kuondoka ikidhaniwa kwamba ilikuwa inaelekea pwani ya Korea.

Lakini meli hiyo na meli nyingine zilipita na kuelekea upande wa Bahari ya Hindi.

Pyongyang ilikerwa sana na kutumwa kwa meli hiyo na imetishia kuizamisha kwa "shambulio moja kubwa" dhidi ya ilichosema ni uchokozi wa Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema mapema mwezi huu kwenye mahojiano ya runinga kwamba angetuma "kundi kubwa la meli zenye nguvu" na kwamba Marekani ina nyambizi ambazo "zina nguvu zaidi, nguvu zaidi kabisa kushinda meli hiyo (Carl Vinson) ya kubeba ndege".

China imeendelea kuhimiza kuwepo kwa utulivu.

Rais Xi Jinping, akizungumza kwa simu na Bw Trump mnamo Jumanne, alizihimiza pande zote "kuvumiliana na kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza vikaongeza wasiwasi zaidi".

Chanzo: BBC Swahili
 
Mmarekani huwa haogopi kama wengi mnavyodhani jamaa huwa anajifanya kama mwoga kumbe shida yake ni kukuondoa kwenye tension then utashangaa siku anakupiga kwa kushtukiza na hautoamini

Mfano mzuri ni kule syiria kunakipindi mmarekani alionekana kushindwa lakini juzi kamchapa assad na huyo puttin kakaa kimya
 
USA huu sasa ni utoto, yaani mkisikia DPRK wanaadhimisha jambo fulani basi ndo wivu unawabana hatari. Sasa kwa nini msiweke program maalum ya kummaliza huyo mnaemwona mdogo tena kwa mara moja badala ya kuwa na matukio ya hivi kila siku.
Hata hivyo China kama moja ya mataifa yenye nguvu kubwa kabisa duniani imetoa tahadhali kwa kutumia maneno ya Hekima sana.
 
Halafu tumejulishwa humu kwamba Senators wameitwa White House kwa kujulishwa plan nzima na pengine kutoa kibali kwa maamuzi mazito kuwahi kutokea tangu dunia hii iwepo. Maana naona hadi vichaa nao wanatishia nyuklia.
 
USA huu sasa ni utoto, yaani mkisikia DPRK wanaadhimisha jambo fulani basi ndo wivu unawabana hatari. Sasa kwa nini msiweke program maalum ya kummaliza huyo mnaemwona mdogo tena kwa mara moja badala ya kuwa na matukio ya hivi kila siku.
Hata hivyo China kama moja ya mataifa yenye nguvu kubwa kabisa duniani imetoa tahadhali kwa kutumia maneno ya Hekima sana.
Tahadhari ya kibwege tu ile, ukiichungulia vizuri utagundua kuwa ndio anajitoa kumsaport mkorea maana kichapo ni eminent.
 
Mmarekani anatabia ya kupiga kwa kushtukiza...

Na kwa hali ya sasa ilivyo, huyo s.korea yupo standby kwaolote kwa sababu ashajua muda wowote kinanukishwa...


Ni kama mtu ambae anakuambia hataki ugomvi... Lakini ukimpa kisogo tu anakutandika na jiwe la usogo... Alafu anatangaza ushindi ukiwa unatapa tapa hoi...


Cc: mahondaw
 
Tahadhari ya kibwege tu ile, ukiichungulia vizuri utagundua kuwa ndio anajitoa kumsaport mkorea maana kichapo ni eminent.
Mabwege wana msaada na askari mzuri hapuuzi ushauri au wazo lolote analopewa. Hata ukimwita DT pembeni atasema nimemsikia China vizuri. Let us assume and take it as a grant kwamba China hatatoa support kwa NK endapo makombora ya USA yatakapoanza kuichakaza NK.
Kwa maneno yako mengine unategemea NK hana hata tofali la kujibu hicho unachodhani hatapata msaada.
Kumbuka ni miaka 50 sasa USA anabweke juu ya "uchokozi" (sasa sijui NK anamchokoza nani) wa NK. Hebu aache maneno aweke mziki tumalize mjadala
 
Mmarekani huwa haogopi kama wengi mnavyodhani jamaa huwa anajifanya kama mwoga kumbe shida yake ni kukuondoa kwenye tension then utashangaa siku anakupiga kwa kushtukiza na hautoamini

Mfano mzuri ni kule syiria kunakipindi mmarekani alionekana kushindwa lakini juzi kamchapa assad na huyo puttin kakaa kimya
Syria sio NK, nenda kaone Military Demarcation line inavyolindwa usiku na mchana more than 40yrs none stop. Huku usa na SK kwa pamoja against NK. Hiyo ni mbali na ulinzi imara katika mipaka yooote ya NK; Ardhini, Angani na Majini.
Mleteni huyo maana maneno yamezidi.
 
Marekani asitumie silaha za maangamizi kama alivyofanya huku Japan na tangu kipindi kile marekani alitakiwa aminywe asimiliki silaha za maangamizi kwani ushahidi unaonyesha si mtu makini!
 
Back
Top Bottom