Kumekucha Dodoma zengwe laandaliwa kumkata mtu

Kumekucha Dodoma zengwe laandaliwa kumkata mtu

damcon

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
214
Reaction score
72
Wakati joto la uchujaji wa majina ya wagombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) likizidi kuongezeka, taarifa zimezidi kuzagaa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kwamba, mikakati ya kumuondoa Edward Lowassa kwenye orodha ya watia nia nayo imezidi kupamba moto.

Kwa muda sasa NIPASHE imekutana na makundi mbalimbali ya wasaka urais na ajenda kuu inayozungumzwa ni mizengwe ya kumwengua Lowassa kwenye kinyang'anyiro hicho ili kuwarahisishia wengine njia ya kuteuliwa na chama kwa kuwa anaonekana kuwa kikwazo kwa baadhi ya washindani wake.

Ofisa mmoja wa CCM makao makuu mjini hapa, aliiambia NIPASHE kuwa wanachofanya wao kama watendaji ni kuandaa majina ya wagombea wote na fomu zao za udhamini na kisha kukabidhi kwa sekretarieti itakayopanga ajenda za vikao vya Kamati Kuu na baadaye Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya taifa.

Ofisa huyo alipoulizwa kama ana taarifa za kuwako kwa mizengwe dhidi ya Lowassa alisema kwa ujumla kwa sasa kuna maneno mengi sana yanazungumzwa juu ya mchakato wa uteuzi wa mgombea, ila akasisitiza kuwa la msingi ni kusubiri vikao vya maamuzi.

"Ndugu yangu ukiyatazama haya makundi (ya urais) ni vigumu kuamini kama wanatoka chama kimoja. Yaani kuna kukamiana kweli kweli.

Kila mmoja anataka kumwangusha mwenzake ili yeye apite," alisema na kuongeza kuwa:
"Hata kama kuna mizengwe, si unajua uchaguzi huu ni wa vyama vingi. CCM haishindani pekee yake, kwa hiyo mgombea anayekubalika ndiye anatakiwa."

Hata hivyo, kwa muda sasa kumekuwa na mfululizo wa habari za kupikwa kwamba jina la Lowassa litaishia Kamati Kuu kwa madai kwamba kuna ushahidi wa matumizi ya fedha kwa timu yake, tuhuma ambazo binafsi (Lowassa) amezikanusha mara kadhaa. Julai mosi mwaka huu siku anarejesha fomu za kuwania urais kupitia CCM alitoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi wa kuhusika kwake na rushwa ajitokeza na kusema alitoa lini, wapi na kwa nani.

Akizungumza na mamia ya wanachama wa CCM makao makuu Dodoma siku hiyo, mbali ya kuwashukuru wote waliomdhamini, Lowassa alisema amechoka kwa tuhuma za kipuuzi za kuhusishwa na rushwa na kusisitiza kuwa hakuna mwanachama yeyote miongoni mwa zaidi ya nane waliomdhamini aliyefanya hivyo kwa kishawishi cha fedha au fadhila yoyote.

NIPASHE imedokezwa kwamba miongoni mwa mikakati inayosukwa kumwangamiza Lowassa ni pamoja na kutengenezwa kwa taarifa za mawasiliano ya siku kuonyesha kwamba kuna fedha nyingi zimetumwa kwa wanachama wa CCM ili kuwashawishi kumuunga mkono.

Mgombea anayetajwa kutumiwa zaidi na kundi linalompinga Lowassa ni pamoja na Makongoro Nyerere, ambaye alifanya mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni na kuporomosha kauli kali za ukakasi dhidi ya Lowassa.

Wakati mizengwe ikizidi kusukwa dhidi ya Lowassa, ripoti ya kura zote za maoni ambazo zimekuwa zikitolewa katika miezi ya hivi karibuni zimeonyesha kuwa Lowassa anaongoza kwa mbali kama chaguo la wananchi wengi kwenye nafasi hiyo.

Miongoni mwa tafiti hizo ni ule wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, uliofanywa mwezi uliopita na matokeo yake kutolewa mwishoni mwa wiki unaonyesha kuwa Lowassa ni changuo la kwanza la wengi kwa kujipatia asilimia 27.0 ndani ya chama hicho, huku Bernard Membe akishikilia nafasi ya pili kwa kupata asilimia 8.2.

Katika utafiti huo ambao REDET walisema kuwa unaweza kuchukuliwa kwa ujumla wake kama maoni ya Watanzania endapo masuala yaliyoulizwa uchaguzi ungefanyika katika kipindi cha utafiti, wahojiwa walikuwa 1,250 kutoka wilaya moja moja katika mikoa 25 ya Tanzania Bara.

Wakati mkakati wa mizengwe ukiendelea kupamba moto, wajumbe wa sekretarieti ya Kamati Kuu ya chama hicho wanaanza vikao mjini hapa leo kundaa pamoja na mambo mengine ajenda na taarifa kwenye vikao vya Kamati Kuu itakayokaa Alhamisi mjini hapa.

Kikao cha Kamati Kuu kinatarajiwa kuchuka majina ya watia nia 38 waliojitokeza kutafuta ridhaa ya chama hicho na kubakisha majina matano tu yatakayopelekwa NEC kwa kupigiwa kura.

NEC inayotarajiwa kukutana Ijumaa wiki hii, itatoa majina matatu kwenda Mkutano Mkuu unaotarajiwa kukutana Jumamosi kwa ajili ya kupata jina moja la mgombea urais wa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.


CHANZO: NIPASHE
 
Bora jambazi lowasa akatwe mapema.Tukichekea nyani tutavuna makapi.
 
fisadi mbona anaondolewa kwa vile vigezo 13 tu, hakuna haja ya zengwe!!!
 
Zaidi ya bilioni 50 zimetengwa na timu lowassa kushinda urais, sasa atazirudishaje?
 
Hivi nipashe ni team lowassa nchi kweli kali
 
Tatizo ni kwamba kuna mgombea anadhani ni "haki" yake kuupata urais.

Kama ingekuwa ni haki yake, mchakato mzima kuanzia kwenye vyama vya siasa hadi uchaguzi wenyewe usingekuwa na maana yoyote.

Watanzania wataamua nani atakuwa Rais wao bila shinikizo au ujanja ujanja wa aina yoyote. Anayedhani urais ni bidhaa, atausikia redioni tu.
 
Kama CC itapitisha jina la Lowasa tutahitaji watusaidie kutoa majibu ya mswali haya;

1. Ile dhana ya kujivua Gamba ilimlenga Rost-m na nani? Tuliambiwa wapo watatu, wa pili ni nyoka wa makkengeeeza;

2. Fedha anayotumia kujitangaza kupitia vyombo vya habari na njia nyinginezo atazirudishaje?
3. Ripoti ya Kamati Maalumu ya Bunge kuhusu Richmond inasemaje? Au ilikuwa kiini macho ili kulinda wakubwa?
 
Kuna jamaa amekuja na thread kuwa jamaa kisha katwa na mmoja ya sababu ni hii;

(v) Sababu ya tano ni mgogoro wa afya yake. Mzee huyu ni mgonjwa sana ingawa anajitutumua na kujikaza, lakini ukweli ni kwamba Edward anaumwa maradhi mazito ya kutetemeka viungo na ubongo. Kutokana na maradhi hayo ambayo ni ya kudumu, Lowassa hatoweza kumudu majukumu mazito ya Urais ambayo ni magumu mno katika nyakati hizi za sasa kuliko ilivyokuwa miaka 5 tu iliyopita. Urais wa zama hizi sio lelemama. Inatakiwa mtu awe na afya madhubuti siyo afya ya kuungaunga kama ya Mheshimiwa Edward Lowassa.

Hivi hayo maradhi mazito ya kutetemeka Ubongo ndiyo yapi!!?
 
waandishi wa habari wanashiriki kikamilifu kudumaza demokrasia na pia kutokuwapa nafasi wanawake
hivi katika hiyo list yupo el tu???
kwanini basi azungumzwe/aandikwe yeye tu

kwanini kumkata yeye iwe zengwe na sio kumkata ASHA iwe zengwe???
inamaana kati ya watia nia wote el tu ndo dhahabu na vigezo vyote kiasi kwamba akikatwa atabakizwa ambaye hamfikii hata robo au nusu au aliemzidi kwa mengi
hizi timu hizi zitatugarimu miaka mingi sana ikiwa magazeti yanazichukulia siriaz namna hii
 
Zengwe ?au kanuni tu na what he really are..ndo vinavyomwengua.?
 
Kuna jamaa amekuja na thread kuwa jamaa kisha katwa na mmoja ya sababu ni hii;



Hivi hayo maradhi mazito ya kutetemeka Ubongo ndiyo yapi!!?

Hicho kikao kimekaa saa ngapi?
 
ipp media yote ni lowasa....propaganda za kijinga kabisa...
 
cooked story
najiuliza sana hili suala la kukatwa mapema jina la LOWASA munaamini Maneno ya nani NAPE AU MWE
NYEKITI wa chama?
jK ALISHIKA MKONO WA LOWASA MWAKA 2010 nakusema ni mtu safi achaguliwe tena nape alisema anatembea na Barua za mapacha watatuza kufutwa uanachama wa ccm
 
Kama CC itapitisha jina la Lowasa tutahitaji watusaidie kutoa majibu ya mswali haya;

1. Ile dhana ya kujivua Gamba ilimlenga Rost-m na nani? Tuliambiwa wapo watatu, wa pili ni nyoka wa makkengeeeza;

2. Fedha anayotumia kujitangaza kupitia vyombo vya habari na njia nyinginezo atazirudishaje?
3. Ripoti ya Kamati Maalumu ya Bunge kuhusu Richmond inasemaje? Au ilikuwa kiini macho ili kulinda wakubwa?

Mkuu kama issue ni ufisadi basi kwa sasa ndani ya ccm hakuna mwenye sifa ya kutuongoza
 
Back
Top Bottom