Kumekucha Bajeti: EU yaongeza masharti ya misaada kwa Tanzania

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
1,250
william_mgimwa.jpg

EU yaongeza masharti ya misaada kwa Tanzania

JUMUIYA ya Ulaya (EU), imeongeza masharti kwa Serikali ya Tanzania ili iweze kupatiwa msaada wa Bajeti kwa mwaka ujao wa fedha 2013/14.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili imezipata, masharti mapya yaliyotolewa na jumuiya hiyo ni pamoja na kuitaka Serikali ya Tanzania kusimamia kikamilifu masuala ya haki za binadamu, utawala wa sheria, kuwapo mfumo madhubuti wa uwajibikaji katika usimamizi wa Bajeti na ushirikishwaji wa taasisi huru.

Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini, Filiberto Ceriani Sebregondi alibainisha hayo jana katika mawasiliano na gazeti hili kwa njia ya mtandao kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Wahisani Wakuu wa Bajeti ya Serikali (GBS), wamechelewa kuwasilisha fedha hizo katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha nchini. Balozi Sebregondi alitaja maeneo mengine yaliyosisitizwa na EU kuwa ni pamoja usimamizi sahihi wa rasilimali za taifa na kuongeza uwajibikaji kwa viongozi wa Serikali.

Alisema kuwa kikao cha mwaka cha mapitio ya uchangiaji wa Bajeti ya Serikali kilichofanyika wiki iliyopita kilichowahusisha wachangiaji wakubwa wa GBS, ikiwamo EU na Serikali ya Tanzania kiliweka wazi juu ya kuwapo kwa uboreshaji wa mfumo wa utoaji msaada na kuridhiwa na pande zote.

Balozi huyo alisema, “EU kupitia chombo cha kutoa msaada wa kibajeti, mara kadhaa imekuwa ikifanya majadiliano na Serikali ya Tanzania juu ya kuongeza juhudi katika kuleta mabadiliko yakinifu kwenye maeneo ya uwajibikaji na vita dhidi ya rushwa.

“Wiki iliyopita wachangiaji wa GBS ikiwamo EU, walikutana na Serikali ya Tanzania kufanya tathmini ya mwaka wa fedha uliopita na kufikia makubaliano juu ya mabadiliko ya mfumo wa utoaji misaada kwa nchi zote zinazofadhiliwa.

Alipoulizwa kuhusiana na masharti hayo jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alikiri kufanyika kwa mazungumzo baina ya Serikali na wahisani na kwamba waliyapokea na wapo tayari kuyatekeleza.

Waziri Mgimwa alisema, “Masharti hayo hayana athari yoyote kwa Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha ujao wa 2013/14.”

Alisema kuwa hadi sasa Serikali inaendelea vyema na utekelezaji wa masharti hayo akiongeza kwamba walishawasilisha taarifa zote kuhusu maendeleo hayo.

Hivi karibuni Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EUC) na Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi wa Umoja huo walikutana jijini Brussels, Ubelgiji kujadili Bajeti ya mwaka 2013 ya umoja huo, ambapo walitangaza masharti mapya ya utoaji misaada kwa nchi zinazoendelea.

Pamoja na mambo mengine, masharti hayo yanahitaji uboreshwaji wa haki za binadamu, utawala wa sheria, uwajibikaji katika matumizi na kudhibiti rushwa.

Akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 bungeni mjini Dodoma Juni mwaka huu, Dk Mgimwa alisema kuwa katika mwaka huo wa fedha jumla ya Sh15 trilioni zinatarajiwa kutumika.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
1,250
Malalamiko na manung'uniko dhidi ya uvunjwaji wa haki za binadamu nchini umefanikiwa kupenya hadi kufikiwa kiwango cha kutambulika kimataifa. Hatua hiyo inajionyesha wahisani wa nchi za Ulaya ambao ni wachangiaji wakubwa wa bajeti ya serikali kuongeza masharti zaidi ya utoaji misaada ikiwa ni pamoja na
 • uboreshwaji wa haki za binadamu,
 • utawala wa sheria,
 • uwajibikaji katika matumizi na kudhibiti rushwa.

Mambo haya ni kimhutasari tu lakini kwa wenye uelewa wa watu hawa (wazungu) imejidhihirisha hawakubaliani na mambo yanavyokwenda nchini na hivyo wameongeza masharti kwa nia ya kuibana zaidi serikali kutekeleza matakwa hayo kwa ajuli ya ukuzaji demokrasia ambayo ndio kisingizio cha serikali ya Tanzania ukiukwaji wa haki za binadamu, utawala bora na rus
hwa.
 
 • Thanks
Reactions: Ame

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
1,225

Mgogoro wa ziwa
 
Chimbuvu

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
4,404
2,000
Hili swali nilimuuliza zitto kabwe alipokuwa anahojiwa jf ,nilimuuliza hv,nyie kama viongozi mna mpango gani wa kuongeza mapato na kupunguza utegemezi kutoka nchi za ulaya ambazo sasa hivi tunaona zipo katika mdororo wa uchumi na inawezekana wakapunguza msaada wao ama kuongeza masharti kutokana na hali ya kiuchumi waliyonayo,je nyie viongozi mmejiandaaje?,,akalipotezea hilo swali na leo ndio ninaona hii makala.big up zitto
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,928

Unampa big up kwa kupotezea swali lako? Au sijaelewa?
 
Chimbuvu

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
4,404
2,000
Ndio,kwa kuwa inamaanisha mimi niliona mbele kabla yake ilhali yeye kama kiongozi alitakiwa alione mapema.big up Zitto

Unampa big up kwa kupotezea swali lako? Au sijaelewa?
 
Last edited by a moderator:
 • Thanks
Reactions: SG8

Easyway

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
2,606
2,000
wasitupe kabisa misaada yao ili tuwe na akili sisi tuna gesi.dhahabu,tanzanite,uranium,shaba,almasi,ardhi yenye rutuba,milima,mito,maziwa,mabwawa,bahari,bandari,misitu, vitu ambavyo nchi nyingi za ulaya hawana,wakitunyima misaada yao watatufanya tuwe wabunifu wa kutumia rasilimali zetu vizuri na tutapiga hatua.

aibu miaka 51 ya uhuru bado tunawategemea wao tu.
 
Jiwejeusi

JF-Expert Member
May 3, 2011
753
0
ni lini mbolea ujinga itakwisha katika bongo za watz. Raslimali zote hizo na bado mnaomba misaada. Pumbafu kabisa, yaone masura yao. Hayooo, oooh. Majinga kabisa. Hasa wewe ccm
 
Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,892
2,000
Hoja Kama hizi wakina Ritz wanazikimbia Kama ukoma wanasubiri Le mutuz aje na za CDM wazivamie Kama viwavi
 
Last edited by a moderator:

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,892
2,000
Hoja Kama hizi wakina Ritz wanazikimbia Kama ukoma wanasubiri Le mutuz aje na za CDM wazivamie Kama viwavi
 
Last edited by a moderator:

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Malalamiko na manung'uniko dhidi ya uvunjwaji wa haki za binadamu nchini umefanikiwa kupenya hadi kufikiwa kiwango cha kutambulika kimataifa. Hatua hiyo inajionyesha wahisani wa nchi za Ulaya ambao ni wachangiaji wakubwa wa bajeti ya serikali kuongeza masharti zaidi ya utoaji misaada ikiwa ni pamoja na
 • uboreshwaji wa haki za binadamu,
 • utawala wa sheria,
 • uwajibikaji katika matumizi na kudhibiti rushwa.

Mambo haya ni kimhutasari tu lakini kwa wenye uelewa wa watu hawa (wazungu) imejidhihirisha hawakubaliani na mambo yanavyokwenda nchini na hivyo wameongeza masharti kwa nia ya kuibana zaidi serikali kutekeleza matakwa hayo kwa ajuli ya ukuzaji demokrasia ambayo ndio kisingizio cha serikali ya Tanzania ukiukwaji wa haki za binadamu, utawala bora na rus
hwa.

Ni bora hao wahisani wangakazia kabisa msimamo wao,au hata waisishe kbs hiyo misaada.Serikali yetu haifikiri nje ya bakuli(kuomba misaada)ni jambo baya sana kwa nchi tajiri kama hii yenye raslimali za kutosha.Matokeo yake tunafikiri kuiba na kuomba tu.Raisi amehamishia ikulu ktk anga,ni ufujaji tu wa fedha pasi na sababu za msingi.HIVI HATUWEZI KUFIKIRI NJE YA KUTEMBEZA BAKULI KWA WAGENI?
 
Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,892
2,000
Magufuli alimwambia sultani kikwete asafiri ili nchi ipate misaada ya kujenga vichochoro wanavyoviita barabara sasa hayo masharti mropokaji magufuli alikuwa hayajui?
 
Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,714
2,000
Na kwanini lazima tupewe misaada ili kusukuma bajeti yetu.
Mi nadhani tujifunze kuishi kulingana na kilichopo, tufunge mkanda. Huku kupenda dezo ndio kunafanya hata wenye madaraka wasiwe na uchungu na taifa, maana wana uhakika fedha za misaada zitakuja tu.
Natamani tufute huu msamiati 'wahisani' kwenye kamusi yetu ya bajeti...
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,158
2,000
Ni bora hao wahisani wangakazia kabisa msimamo wao,au hata waisishe kbs hiyo misaada.Serikali yetu haifikiri nje ya bakuli(kuomba misaada)ni jambo baya sana kwa nchi tajiri kama hii yenye raslimali za kutosha.Matokeo yake tunafikiri kuiba na kuomba tu.Raisi amehamishia ikulu ktk anga,ni ufujaji tu wa fedha pasi na sababu za msingi.HIVI HATUWEZI KUFIKIRI NJE YA KUTEMBEZA BAKULI KWA WAGENI?

Kama walivyosema wakuu Kitulo na Baikoko hawa wanajiita wahisani cum marafiki wa maendeleo ni matapeli na wezi wakubwa.

Kwani masuala ya utawala wa sheria na uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za taifa, wameanza kuyapigia kelele leo? Sasa kama wanaona kelele zao hazisikilizwi kwanini wanaendelea kutoa hivyo vijimisaada vyao?!?

Hapa ndiyo yale mambo ya kiranja mkuu, "ukitaka kula, sharti uliwe!!!"

Mimi kwa kweli ninatamani sana siku ifike misaada yote isitishwe. Siku hiyo wadanganyika tutapata akili.

Ee Mola niweke hai nione siku hiyo. Amina.
 
Last edited by a moderator:

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,714
2,000
Ni bora hao wahisani wangakazia kabisa msimamo wao,au hata waisishe kbs hiyo misaada.Serikali yetu haifikiri nje ya bakuli(kuomba misaada)ni jambo baya sana kwa nchi tajiri kama hii yenye raslimali za kutosha.Matokeo yake tunafikiri kuiba na kuomba tu.Raisi amehamishia ikulu ktk anga,ni ufujaji tu wa fedha pasi na sababu za msingi.HIVI HATUWEZI KUFIKIRI NJE YA KUTEMBEZA BAKULI KWA WAGENI?

Unajua penye wanauza bastola used?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom