Uchaguzi 2020 Kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais ni kuikabidhi Tanzania kwa Mabeberu. Tusifanye kosa twende na John Pombe Magufuli

Hahaha Leo Lumumba hali si hali. Mnahamisha tu magoli. Na jiandaeni tu kumkabidhi nchi mwana wa Singida, mtoto wa Ilboru, Tundu Antipas Lissu
Mkuu jipe moyo kwa hilo. Lakini wenzio wakiongozwa na huyo Tundu wenu wanajua watashindwa vibaya na mwamba JPM na kwa kuficha hiyo aibu wameanza kuweka visingizio vya kuibiwa kura.
 
Tumeshawazoea maneno yenu. Wa mitandaoni ndo tulijitokeza kwa maelfu kumpokea airport tarehe 27 na kama message nauhakika mliipata hakika

Kamwe hatuwezi kuwa na amiri jeshi wa vile. Atakagua vipi gwaride la makamanda wetu wakakamavu. Elewa ulemavu wa kiongozi ni ulemavu wa nchi anayoiongoza. Tuna akili timamu hatuwezi kulemaza nchi yetu kwa kumchagua Lissu
 
Mitano kwa Jiwe INATOSHA.

Kwa miaka hii mitano tu, zaidi ya trilioni 2.5 HAZIJULIKANI ZILIPO. Pesa hizo ni zaidi ya wizi wote uliofanyika kwa awamu zote tangu tulipopata uhuru, ujasiri wa kupamba na kusifu MHALIFU wa kiwango hicho unautoa wapi Mkuu?
Hizo ndege ananunulia ela ya baba yako? Bwana la umeme ajengea fedha yako? reli anajengea fedha yako? dodoma imejengwa na fedha ya baba yako? kijana acha maneno ya kuokoteza, hivi unajua fedha tilioni 2.5 au unabwabwaja tu, watu wakati enzi za Kikwete waliiba fedha za escow bilion 230 walikuwa wanasomba kwa viroba Kwa mjibu wa bunge, sembuse tilioni, eti nyinyi mnalilia uhuru wa habari, hapa ukiulizwa eleza vizuri Kwa ushindi, unaanza hii serikali ya dicteita kumbe wewe mwenyewe unaandika usiyo yajua mradi una smart na unajua kuandika.

Haya tueleze kidogo hizo ela zimefichwa benki hipi hapa Tanzania au nje ya nchi?. Tujifunze kutumia uhuru wa kutoa maoni, siyo haya ambayo hayana ushaidi . Sema siku hizi jamii forums kumejaa utoto mwingi, jamii forums ilikuwa enzi za kina mwanakikiji, mkulima masikini, sasahivi angarau amebaki Pasco kidogo enzi za akina mwanakikiji mtu akiweka bandiko anabandika na ushaidi, hata hukipinga ukweli unabaki nao moyoni, sio hizi takataka za siku hizi.
 
Kwani mabeberu waliokwapua madini yetu tangu mwaka 1995 mpaka leo, waliouza vitalu vyetu kwa "mabeberu" na kwa waliopiga dili za Richmond,Escrow na upotevu wa 1.5Trillion (kama ilivyoainishwa na CAG waliyemfukuza) ni akina TUNDU LISSU?

Endeleeni kuwadanganya wajinga, lakini wanaomfahamu Lissu (kabla na baada ya kuwa mbunge) wanajua moyo wake wa dhati kabisa katika kutetea maslahi ya nchi hii, alianza kupiga kelele juu ya ufujaji wa rasirimali zetu tangu enzi za Mkapa mpaka leo...
 
Mtumishi wa leo kiukweli jukwaa limevamiwa
 
hujafa hujaumbika!
 
Mtaimba sana taarabu Lisu hafai ila matokeo hapo Oct 28 ndiyo yataamua kati ya Tundu &
Magufuri nani anafaa.


Tulia kada wa Lumumba mtanyooka tu CDM ya 2020 sio ilee ya 2015
 
Hata sasa ipo chini ya mabeberu, wapi 1.5 T zetu?
 
Mtaimba sana taarabu Lisu hafai ila matokeo hapo Oct 28 ndiyo yataamua kati ya Tundu &
Magufuri nani anafaa.


Tulia kada wa Lumumba mtanyooka tu CDM ya 2020 sio ilee ya 2015
Mpaka mtazeeka mnabadili misemo tu,sizitaki hizi mbichi
 
Hivi wakati tunapigwa kwenye deal ya rada,meremeta,escrow,mikataba mibovu ya madini,bomba la gesi,ni chama gani kilikuwa serikalini?
Uwe unatumia akili,waza kwa kutumia ubongo sio makamasi.
Geita,Kuna dhahabu,lakini ka mji kabovu ksbisa,fika kahama,nenda kalumwa,nenda kakola,uone umaskini wa wananchi ambao wamezungukwa na dhahabu na almasi,nchi hii imekuwa inaliwa na mabeberu tangu Nyerere afe.
Anaetunga mikataba na Sheria za madini,nj wabunge wa ccm,na serikali,sasa TL anaingiaje hapo,anaikabidhi vp nchi kwa mabeberu,wakati wamekuwa wanaitafuna tangu akiwa shule.
Ukiona wizi,ufisadi ,wa Mali ya umma,wote unafsnyika wakati ccm ipo Madarakani,that is fact,Chadema haijawahi kuchukua madaraka,usiwe mtabiri.
 
Kwani hizo pesa anazitoa mfukoni kwake? Hizo ni kodi zetu na pesa za Wafadhili, uwe na akili usiwe kama wale wenzio walioshindwa kujenga choo kule Rufiji.
 
Ukweli wengine ni mijibwa koko msiofaa! Hivi kuna lipi la maana kipindi hiki zaidi ya maumivu na utumwa? Walio serikalini wanaogopa kutoka wamefungwa ni watumwa! Kwa mara ya kwanza watanzania utumwa umeletwa na mtanzania mwenzetu. Huyu si tu ni zaidi ya beberu ni kaburu mbaguzi wa kutisha huyu lazima aondoke!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…