Kumbukumbu mjarabu

Kumbukumbu mjarabu

englibertm

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2009
Posts
9,252
Reaction score
6,211
Itakumbukwa, kwenye mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia Juni 8, 1990 kule Italia, Argentina, mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia kwa wakati huo, walibaki midomo wazi wasiamini kilichotokea. Ilukuwa ni kisa cha mende aliyeangusha kabati.Kule Italia mwaka 1990 tuliona jinsi Argentina walivyoweweseka uwanjani mbele ya Cameroon.

Pamoja na kushuhudia beki wetu Andre Kana Biyik akitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika ya 62 ya mchezo kwa kumpiga daruga Claudio Cannigia na si hapo tu, Benjamini Massing, naye akapigwa kadi nyekundu baada ya kumkaba kwa nguvu Diego Maradona karibu katika muda wote alipokuwa uwanjani kiasi cha Maradona kuonekana kupotea kabisa uwanjani. Ili kumpa nafasi Maradona kupumua, na hivyo kuwabeba mabingwa watetezi Argentina, refa ikafika mahali akachomoa kadi nyekundu kwa Benjamin Massing.

Hata hivyo, pamoja na kadi hizo nyekundu, Cameroon ikafanikiwa kupata bao la kuongoza kwa bao maridhiwa la kichwa la Omam Biyik. Argentina kama kabati, likawa limeangushwa na mende!

Mmoja wa watu watakaoishi wasisahau kipigo kile ni Diego Armando Maradona. Na kwa maneno yake mwenyewe baada ya mpira kumalizika, Maradona alisikika akitamka; " Si Cameroon iliyoshinda, bali ni sisi tuliopoteza mchezo!"
 
" Si Cameroon iliyoshinda, bali ni sisi tuliopoteza mchezo!"


Nimeyapenda bure haya maneno. Ni maneno ya mkosaji.


Tiba<!-- google_ad_section_end -->
 
" Si CCM iliyoshinda, bali ni sisi tuliopoteza muelekeo!"
 
Bonge la timu,Kunde,Milla,Makanaly,Biyik,Mfede,Massing, tulikuwa tunatia maguu pale Livingstone kwa Bharesa au kwa shekh Yahya...
 
Kandanda haikaukiwi simulizi. Mwaka 1974, nchi jirani ya Zaire, sasa inaitwa DRC Congo, iliandika historia kwa kuwa nchi ya kwanza kusini ya jangwa la sahara kushir...iki fainali za kombe la dunia. Ilikuwa ni nchi ya kwanza ya waafrika weusi kushiriki kombe la dunia.

Na kila kukicha Afrika kunazuka kituko, alisema mwanafalsafa Plotemy wa ugiriki. Zaire ilipangwa kundi moja na Brazil. Rais wa Zaire, Papaa Marshall Mobutu Sese Seko Kuku Mbangu wa Zabanga , jina lenye maana ya yule anayetembea na kuacha moto nyuma, aliamini kuwa kandanda ni ndumba na ngaye, kwamba ni uchawi. Aliamini katika timu za kundi lao ajipange zaidi kiuchawi kuwakabili Brazil.Iliaminika kuwa Brazil ni wachawi zaidi.

Mobutu akawaita wachawi wote Kinshasa. Akawakodia ndege kwenda Ujerumani mwaka ule wa 1974.
Masikini, wachawi wale waliwafanya wachezaji wa zaire wakeshe hotelini wakufukizwa ndumba. Hawakulala vema, siku ya mechi ya kwanza ilipofika dhidi ya Yugoslavia, Zaire walipigwa 9-0! Na walipokutana Brazil pichani juu napo wakaambulia kipigo.

Pichani ni Boba Lobilo na Mwepu Ilunga wakimkabili Edu wa Brazil
 
Back
Top Bottom