Kumbukumbu ipi ya mlevi kila ukiikumbuka unabaki kucheka??

tozi25

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
5,963
2,000
Nakumbuka wakati wa Bia ya Bigwa ndio kwanza inatoka kuna shombeshombe mmoja alikunywa kama bia mbili tu. Jamaa hakuweza kutembea basi rafiki zake wakambeba na kumuingiza kwenye Taxi, Yule dereva wa taxi akawauliza mnaelekea wapi. Duh yule shombeshombe si akaanza kutapika mule ndani ya taxi,:eek:o_O Haikuchukuwa hata dakika akaanza kutokwa na haja kubwa akiwa ndani ya taxi.:D Yule dereva alibaki kutukana pale:mad: na kutaka alipwe hela nyingi zaidi.
 

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,759
2,000
Aisee bora vile bia ya Bingwa iliondolewa sokoni,

Yaani ukiipiga kizembe jua imekula kwako.

Wakati huo mzee mmoja alizipiga mbili akashindwa kutembea, kutokana na mvua kunyesha na yeye amelala barabarani kwa kushindwa kutembea, maji yaliingia puani na ndo ukawa mwisho wa uhai wake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom