Kumbukizi ya wimbo wa Kala Jeremiah

Kumbukizi ya wimbo wa Kala Jeremiah

Fifteen

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2021
Posts
583
Reaction score
721
Naomba kala Jeremiah asikilize huu wimbo wake tena kisha aje atuambie ulikua unahusu nini? Ndipo asifie serikali ya awamu hii inaupiga mwingi maana huu wimbo ni kama alitabiri yatakayo tokea awamu hii na ndo anayo yasifia

UBETI WA 1


Rest in peace Kawawa Karume Baba Nyerere
Mlipanda mahindi sasa vipi hawa ngedere?
Wameshiba, tuna njaa
Hawaijui shida ya mtaa
Wamekula kila kitu, wakajibanza juu ya paa


Leo twiga anapanda ndege, mmang'ati anapunga mkono
Nikisema No! Ni nani ataniunga mkono?
Kipigo cha daktari siyo dawa ya huo mgomo
Let me stay conscious, usinizibe mdomo
Damu ya Mwangosi inageuka promo
Inawafuata mpaka uani mnakopaki hizo limo


Mpiga kura mmembana kama mjusi chini ya mlango
Mwanafunzi anarudishwa kisa hela ya mchango
Baba hana hata mia, anadaiwa hela ya pango
Daily ugali na bamia, mama akishauza matango
Ndo life ya Kibongo – tajiri mpe bia, masikini gongo




KIITIKIO


Masikini wale wale, matajiri wale wale
Masikini yeeeeeeeeah, matajiri ooooooowah
Masikini (tupooooooo)
Matajiri (tupo)
Masikini yeeeeeeh, matajiri oooooooowah




UBETI WA 2


Masikini wale wale, matajiri wale wale
Wagonjwa wanaongezeka, bado wodi zile zile
Sewa haji ile ile
Wagonjwa wanalazwa koridoni pale pale
Wamevunjika miguu, mikono vile vile


Dereva wa boda boda, nipeleke pole pole
Maana yanatisha niliyoyaona kule
Utandawazi umewachanganya watoto wa shule
WhatsApp, Facebook, BBM vile vile
Wazungu wameturudishia ujinga wa kisasa


Brother, uza smartphone, fuga kuku wa kisasa
Obama si urudi tena, barabara zipigwe msasa – hahahaha!
Tanzania yangu, Tanzania yangu, nakupenda nakupenda sana nchi yangu
Sema Tanzania yangu oooh... Tanzania yangu oooh...
Tanzania nakupenda sana nchi yangu




RUDIA KIITIKIO


Masikini wale wale, matajiri wale wale
Masikini yeeeeeeeeah, matajiri ooooooowah
Masikini (tupooooooo)
Matajiri (tupo)
Masikini yeeeeeeh, matajiri oooooooowah




UBETI WA 3


Usilie mama yo, kwanza futa chozi njoo
Shika jembe ukalime japo pembejeo no
Ule mtaji wa mkaa umeshafilisika
Na mkopo uliokopa bado haujaulipa


Mvua za masika zimeshakatika
Na mazao yote tayari yashanyauka
Kinachofuata ni njaa, dhiki na balaa
Ukahaba, ukabaji – ndizo ndoto za mitaa

Tuna dhahabu toka Bara
Gesi toka Mtwara
Tuna maziwa, tuna mito, Ngorongoro na Manyara
Kilimanjaro mlima wa bara
Almasi, Tanzanite – daa! Aise huu ni u.........

Walimu wamekonda kwa udogo wa mshahara
Wanafunzi wanafeli kwa ubovu wa mitaala
Madawa ya kulevya, nchi yetu ndiyo ghala?
Huu wimbo wakiuliza, waambieni ameimba KALA.
 
Damu za kina Mzee kibao zinawafuata mpaka uani mwao ndio maana wanaropoka tu
 
Huyo jamaa wasiye mjua ni mtu na panya kwa tabia zake.
Kwanza wimbo alitengenezewa na mpaka beat ila kilichotokea kama tabia za CCM.
 
Huyo jamaa wasiye mjua ni mtu na panya kwa tabia zake.
Kwanza wimbo alitengenezewa na mpaka beat ila kilichotokea kama tabia za CCM.
Akajipa credit zote menyewe basi ndo maana hayaoni ya saivi kwasababu wimbo hauko moyoni mwake
 
Back
Top Bottom