Kumbuka ulipotoka, tazama ulipo leo, beba tumaini jipya halafu inuka tuendelee kupambana

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Katika umri wangu wa miaka 26 nilionao, sina nyumba, sina gari, sina kiwanja, sina kipato kikubwa na wala sina asset yoyote ya thamani mpaka muda huu. Mtu yeyote anaenifahamu akiniangalia lazima aniweke katika kundi la vijana ambao hawajafanikiwa..si uongo, ni ukweli kwa upande wake anavoyachukulia mafanikio.

Binafsi, najiona mmoja kati ya watu wenye mafanikio sana. Namshukuru Mungu kwani nilivyo leo kwani ni tofauti na nilivyokuwa mwaka jana. Ni tofauti kubwa sana na jinsi nilivyokuwa miaka 8 iliyopita. Na ninaamini kwa mapenzi ya Mungu kesho yangu itakuwa na tofauti kubwa chanya kuliko leo.

Nina afya, amani, nguvu, furaha, maarifa na skills ambazo zinanifanya niweze kupata japo kidogo cha kuniwezesha kusukuma siku. Nilikutana na watu wema ambao walinithamini na kunishika mkono kunivusha katika kipindi ambacho kila siku naomba kisijirudie. Hawana uwezo/nafasi kubwa ila hawakuchoka kugawana namimi sehemu ndogo ya vipato vyao vidogo. kuwa na watu wasiokutupa wakati wa shida ni moja ya mafanikio yasiyozungumzwa.

Jambo jingine la kumshukuru Mungu ni ukweli kuwa amenipa nguvu na uwezo ambao katika kipindi fulani cha maisha yangu niliutumia kugusa na kubadili historia za wengine. Wakati nikijivunia watu walionishika mkono kunivusha katika hali ngumu, nafurahi pia kuona nikiwa sehemu ya mafanikio ya vijana wenzangu. Siwadai, sitarajii malipo maana hata mimi sidaiwi ila naamini pia wao watagusa maisha ya wengine.

Haya ndio mafanikio niliyonayo na ninaamini siku moja nitafanikiwa kumiliki vyote ambavyo sina leo na kubwa zaidi nitafanikiwa kugusa maisha ya watu wengi zaidi na kuwa njia ya tabasamu kwao na kwa familia zao.

Kijana mwenzangu na mtu yeyote unaepitia changamoto tofauti za kimaisha leo, amini kuwa siku moja yatakwisha. Shukuru kwa mafanikio uliyonayo sasa. Hata mimi bado kuna vitu navitamani, kunachangamoto nazipitia sasa ila naamini kama 2012 na 2020 ni tofauti basi siku moja changamoto za leo zitakuwa historia na tutakutana na changamoto pya. Changamoto haziishi.

Mafanikio ya wengine yasitufanye tujidharau na kusahau kushukuru kwa hapa tulipo. Hakuna hali inayodumu milele, USIKATE TAMAA INUKA TUENDELEE KUPAMBANA.​
 
Back
Top Bottom