kumbu kumbu mjarabu

englibertm

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2009
Posts
9,252
Reaction score
6,211

Huenda si wengi wenye kufahamu, kuwa George Weah ndiye mchezaji wa kwanza kutoka nchi ya Kiafrika kupata kutunukiwa t...uzo ya Mwanasoka Bora Duniani. George Weah anatoka nchi ya Liberia.
Ilikuwa ni mwezi Desemba, mwaka 1995, ni pale FIFA ilipoitangazia dunia ya soka, kuwa George Weah amechaguliwa kwa kupigiwa kura kuwa mwanasoka bora wa dunia.

Na mwaka huo huo, George Weah akawa Mwanasoka Bora wa Ulaya, na haikuishia hapo, akatangazwa pia kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika! Mwaka mmoja mataji matatu!

George Weah alianza kusakata kabumbu nchini mwake Liberia kabla ya kuhamia klabu cha Monaco, na baadae Paris Saint Germain. Mwaka 1995 akaenda kwenye klabu ya Milan na ndipo akafikia kilele cha mafanikio yake katika soka. Kwenye uwanja wa nyumbani wa San Siro wa timu ya Milan, George Weah alikuwa mfalme aliyependwa sana na wapenzi wa Milan.

Baadae, George Weah akaenda kuchezea Chelsea na Manchester City.
 

asante sana ni kweli wengi hawalijui hilo hasa hichi kizazi kipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…