Kumbe Zari na Madam Ritha ni ndugu

Kumbe Zari na Madam Ritha ni ndugu

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,213
Reaction score
18,455
VMachoni pa wengi maswali yaliibuka miongoni mwa mashabiki wa mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz’ , Zarinah Hassan ‘ The Boss Lady ’ baada ya kumuona akiwa ‘ klozi ’ na Bosi wa Bongo Stars Search ( BSS ), Rita Paulsen ‘ Madam ’ kwenye shoo ya Zari All White Party iliyofanyika juzikati kwenye Ukumbi wa Mlimani City , Dar .
Madam Rita akiwa katika pozi na Zari walipokua kwenye Zari All White Party .
Katika ‘ iventi’ hiyo, Madam Rita alikuwa beneti na Zari hivyo baadhi ya watu walikwenda mbali zaidi na kudhani labda Madam alikuwa kama bodigadi ’ wa Zari ili kusaidia linapokuja suala la kumwaga ung ’ eng ’ e a . k.a kutema yai lakini Ijumaa Wikienda limefanya kazi yake na kubaini kwamba wawili hao ni ndugu kabisa .
Wakiwa katika pozi .
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba Zari na Madam Rita si ndugu wa tumbo moja ila mama zao ndiyo wenye undugu wa damu kwani wanaitana binamu .
Ilifahamika kwamba , Zari amekuwa akikutana na Madam Rita mara kwa mara anapokuwa Bongo , ikiwa ni pamoja na kushauriana mambo kibao ya kimaendeleo hasa katika suala zima la kuona fursa kwenye ishu za burudani .
Madam Rita, Diamond na Zari wakiwa katika picha ya pamoja .
Imebainika kuwa ukiachana na kukutana Bongo , ndugu hao wamekuwa wakikutana Sauzi kwenye mishemishe zao za kusaka ‘ mahela ’ .
Kwa mujibu wa Madam Rita, mbali na undugu , anamkubali Zari katika pilikapilika za kusaka maisha lakini pia Zari naye anamkubali Madam Rita kwa harakati zake za utafutaji na kupambana na umaskini.
“Zari ni mwanamke mtafutaji na ni ndugu yangu kabisa . Unajua pale Mlimani City watu walikuwa wanauliza tupoje, wengine walidhani nipo na AKA (msanii wa Afrika Kusini ) lakini ukweli ni kwamba mimi na Zari tunafahamiana vizuri , ” alisema Madam Rita.
 

Attachments

  • 1431328605178.jpg
    1431328605178.jpg
    55.4 KB · Views: 2,312
Undugu huu wa kuunganishwa na white party banaa,haya hatujabisha wawe ndugu tu kwani sh.ngapiii
 
AHahah marienge, mbona mimi na wewe ni mtu na binamu yake ila watu hawashangai? MXiuuu

Shangaaaa undugu huuu ,ni kama kuna rafiki yangu mmoja hivii yaan ye kila mtu huaga ni ndugu yakee ashanichoshagaaa
 
Alikuwa nae pia SA wakati D ameenda na UG kwenye party huko.

Ila Zari ana dada yake mkubwa wa damu anaishi TZ.
 
Inawezekana..maana madam rita sio pure tanzanian
 
Nje ya Mada Kidogo: Kuna kipindi kulikuwa na uvumi kwamba ALIKIBA anapumzika kwa Madam Ritha sijui kuna ukweli? nataka kuunganisha doti.. hapa
 
Ndiyo maana nilisema wewe uko management ya domo, hongera

lol si naona wanavyojitangaza kuhusu show zake jamani na safari, leo karudi bongo wana bday party ya meneja yake...eti private party. nipe basi username yako ya insta nitakuwa na ku tag then uweke on notifications kutakucha pia nitakutag kwa walio karibu nae nao utawaona wanayorusha. ila duh yamaana utanijua kule...nafunika uso sasa...hakuna matata.
 
yupi huyo nami nika induce undugu!

Yupo kaolewa picha zao zimo humu ila sura hazionekani bali zipo kwenye insta yake kama wiki 46/47 zilizopita toka leo. Wadogo zake wawili walikuja ZWP hukuwaona?
 
Tumechoka na huyu Zari wenu na Diamond mazafanta, vimtu vyenyewe hata havijai mkononi kutwa kuvileta humu *****...too much make hana uzuri wowote.
 
Back
Top Bottom