comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,014
- 6,834
MWANAUME ANAEPENDA MTEREMKO NI SAWA NA MBWA HATA UMPE NYAMA KILA SIKU HAWEZI KUACHA KWENDA KUONGEZEA MAKOMBO KWA JIRANI
Deus Mkombozi Kira
Binti mmoja alikuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu, alikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa anakuja kwake mara kwa mara, alikuwa anakuja kula, kunywa na kufanya kila kitu kwake. Yule kijana aliifanya ile sehemu kama yake, pamoja na kula na kunywa kwa yule dada alikuwa hatowi hata Shilingi kumi yake.
Dada aliumia sana na alikuwa akilalamika kwani mara nyingi alikuwa akimfumania yule kijana na wanawake wengine lakini yeye kuvumilia na kufanya kila kitu kwaajili ya kijana.
Siku moja alienda kwa Mama mwenye nyumba wake (Mama Rozza) kumuomba ushauri, alienda kumuomba ushauri na kumuambia tatizo lake.
Mama Rozza alimwambia subiri pale nje kwake kulikuwa na Mbwa ambao hupita mara kwa mara, Mama Rozza akawa ananunua nyama na kuwawekea. Alikuwa anaweka kila siku mpaka wale mbwa wakazoea na kuwa wanakuja pale kila siku, muda ukifika wanakuja wanakula na kuondoka.
Alimuonyesha yule binti na siku moja alimuambia yule binti wale Mbwa wakiondoka basi wawafuatilie, waliwafuatilia na kuona sehemu wanapopumzika, waliwaangalia lakini baadae walinyanyuka na kwenda sehemu nyingine ambapo chakula hutupwa nje na kula, walipotoka hapo walirudi kwa mwenyewe wakaingia kwenye Banda na kulala.
Mama Rozza alimuangalia yule binti na kumuuliza umejifunza nini Binti akamwambia hajui chochote. Mama Rozza alimwambia kuwa mwanaume anayehudumiwa ni sawa na Mbwa anaye zurura hubweteka, wewe kumpa chakula haimaanishi ni Mbwa wako, yeye huenda pale tu kwenye chakula na akishiba hutamuona tena.
Hawa mbwa tunawalisha lakini wanaenda na kwingine wanalishwa pia na kwingine kisha wanarudi kwa mwenye mbwa kulala, sisi kuwalisha hakuwafanyi kuwa wakwetu na kama tukiacha kuwalisha hawatarudi tena kwani kwetu wanafuata chakula na hawatufuati sisi.
Kweli alipoacha kuweka nyama wale Mbwa waliacha kuja akamwambia yule binti. “Mwanaume unayemhudumia anayependa mteremko siku ukiacha kumhudumia lazima ataenda kutafuta mteremko kwingine na siku akipata mtu wa kumlisha vizuri akashiba basi hatarudi tena kwako hivyo acha kumhudumia huyo mwanaume wako.
Kama unataka akupende muache akupende kwakuwa unamvutia na si kwakuwa unamhudumia vizuri.