Siku ya tarehe 1/6/2018 baadhi ya wazee walienda makao makuu ya NSSF kufuatilia pension ya mwezi wa tano ambao baadhi yao hawajapewa hadi sasa kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.
Wazee wale wakionekana kuchoka na kukata tamaa, mmoja wa wale akina dada aliyekuwa anawahudumia pale makao makuu ghorofa ya 10 nadhani aliona kwake ni usumbufu akatoa kauli ya kuwaambia wale wazee kuwa 'hata hivyo hizi pension tunazowapa ni msaada tu NSSF inatoa kwenu hamjastahili kuzipata'.
Wazee wale walipigwa na butwaa kwa hiyo kauli na mmoja kati ya wale wazee alishindwa kujizuia na akamwambia yule dada kuwa hata yeye Mungu akimjalia atafikia umri kama wao na vilevile Mwenyezi Mungu akipenda anaweza asifike.
Wazee wale waliambiwa kuacha namba za simu warudi nyumbani watafahamishwa.Sasa kwa jambo hili la wazee kukosa pension na majibu tata ya kiwango hiki tunadhani NSSF kuna shida.
Ni vyema NSSF wakalitolea kauli hili swala kwa ujumla wake kwani watu wameanza kuwa na tafsiri mbaya.Sasa mifuko ikishaunganishwa na wanachama wakawa wengi zaidi hali itakuwaje?