Kumbe ukiwaona wakubwa wanakusaidia TRA .

Maalim Jumar

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,259
117
waheshimiwa Salaam.

Nilifika TRA kujiandikisha ili nipewe TIN kwa kupata Driving Licence mpya...nikaambiwa ni bure na ndani ya siku 7 naipata.
Lakini tangu Mwezi wa sita nilikua nasumbuliwa ''njoo baada ya wiki...mara kajiandikishe manzese...na maneno mengine kibao''

Leo nikawaondolea uvumilivu nikaenda kumweleza Region Manager nikapewa kiongozi (namuhifadhi) nmeshughulikiwa kila kitu leo leo.
Nawapa hongera viongozi aina hii.
Tuijenge Nchi kwa Pamoja.

Nawakilisha!
 
Mpe hongera kwa kukusaidia lakini ili awe kiongozi anatakiwa ashughulikie/awajibishe wa chini yake ili wataka huduma wengine wakifika wahudumiwe kwa haraka kwa taratibu zilizopo siyo mpake uonane na boss au kutoa rushwa kupata haki yako ambayo ni ya bure kabisa
 
MPAKA NAENDA NGAZI ZA JUU NIMEKIMBIA HIYO MIANYA YA rUSHWA!
SASA WAJITAHIDI KUWAWAJIBISHA ...MAANA HAYO MALALAMIKO YANGU NDIO KUONESHA CHINI KUMEOZA!
 
umekuta kaamka vizuri sio jadi yao kaka, so umemuotea. mi nilitoa elf tano ndo nikapewa tin namba
Mimi ndie nilieamka vizuri si wao. Halafu mbaya zaidi mtandao wao nilikuta unawasumbua hao mabosi labda ndio maana alipata mda wakunishughulikia!
Lakin nilipokewa vzuri jaman!
Ukitoa buku tano? Akina nyie ndio mnaharibu huduma ...mnawazoesha halafu yanatukuta sie tusiozoea hiyo njia haram.
Usirudie tena!
 
mimi simlaumu aliyetoa hyo buk 5, kwa sababu la cvyo hacngepata huduma na ana haraka nayo!
<br />
<br />
Sasa ukizungukia ofisi nyingi za serikali huwa hawatatui matatizo kwa mda muafaka...huoni ulimshaur afanye hivyo atakua mtoaji zaidi?
Vizur ni kuwazindua na hatua kuchukuliwa.
 
TIN Namba ni Tsh 10,000/= wala huhitaji kumwona mkubwa labda hutaki kupanga foleni TRA/
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom