Kumbe UDSM ina miaka 40 tu; Hii 50 imetoka wapi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,999
Katika pita pita zangu nikakutana na hotuba hii ya Rais wa Tanzania Mwl Julius Nyerere; utangulizi wake unasema hivi (msisitizo mweusi wangu):


Hotuba yenyewe ilianza hivi:


Kutoka (J.K. Nyerere, Freedom and Development, 192;1973)

Sasa, kwa mwanga huu na uelewa huu kuwa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam kama tunavyokijua sasa kilianza rasmi Augusti 29, 1970.. kwanini tunasherehekea miaka 50 wakati University College of Dar-es-Salaam (kilichoanza Juni 1961) kilidumu kwa chini ya miaka kumi tu? Labda nimekosea, tungemuuliza leo Baba wa Taifa UDSM ilianza lini rasmi kweli angesema ni 1961? Hadi historia tunachakachua?
 
nani anasoma tanzania? Wanataka dr kipeuo cha pili apate ujiko akipreside occation ile.pumbaf
 
Sasa wasomi "nguli" wakichakachua kakosa kadogo kama hako ka-historia unategemea nchi hii itatoka kwenye umaskini kwa kutumia mawazo yao ?...wanaabisha hadhi ya UDSM
 

Wewe Mzee Mwanakijiji ukisilimu leo na kupewa jina jipya la Hussein, ina maana umri wako utaanza kuhesabiwa pale jina jipya lilipoanza? UDSM (officially DAR) inatimiza miaka 50, hayo mengine ni mabadiliko ya majina tu.
 
Ni miaka 50, tangu kilipoanza pale Lumumba. Kilele cha sherehe ni mwakani, 2011. Jivunie nchi yako 'Plato', mkataa kwao ni 'MTUMWA' kama umejaliwa kusomea nje mshukuru Mola, usitoe kejeli.
 
Kwa mfano Ardhi University ina UMRI gani? Ni tangu UCLAS au Ardhi Institute?
 
Chuo kikuu cha Dar es Salaam kina miaka 5O kama chuo kikuu, ingawa jina la University of Dar es Salaam lilianza rasmi miaka 40 iliyopita; kilianza kikiwa kinajulikana kama Dar es Salaam University College of East Africa. Vyuo vikuu vingi huanza kwa jina jingine na baadaye hubadilisha majina hatua kwa hatua; ni tofauti na Chuo kinachoanza kama high school halafu baadaye kugeuka kuwa Chuo Kikuu; historia ya chuo cha namna hiyo itaanza wakati kilipogeuka kuwa chuo kikuu siyo wakati kilipoanza kama high school. Vyuo vingi vya serikali USA vina historia za namna hiyo kama ya UDSM. Angalia mfano wa historia ya North Carolina State


Kwa mfano Ardhi University ina UMRI gani? Ni tangu UCLAS au Ardhi Institute?

Historia ya Chuo Kikuu cha Ardhi inaanza pale kilipokuwa chuo kikuu siyo wakati kikiwa Ardhi institute, similarly, historia ya Mzumbe University inaanza pale kilipoanza kuwa University, siyo wakati wa IDM.

Baadaye nitaleta mifano ya vyuo vilivyokua kutoa chuo kidogo hadi kuwa chuo kikuu kuonyesha namna vionavyorekodi historia zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…