umefanywa Tanzania na MtambuziIngawa nakubaliana na hayo maoni ya kwamba Watanzania wengi hawana kawaida ya kuchunguza au kujiuliza kuhusu mambo yawazungukayo, ila habari hii haijaweka wazi huo utafiti uliofanywa hivi karibuni umefanywa na nani na umefanyikia wapi.
Ingawa nakubaliana na hayo maoni ya kwamba Watanzania wengi hawana kawaida ya kuchunguza au kujiuliza kuhusu mambo yawazungukayo, ila habari hii haijaweka wazi huo utafiti uliofanywa hivi karibuni umefanywa na nani na umefanyikia wapi.
Ahaaa, nimekumbuka, aliwahi niambia kwamba kale ka - Simu kake ka Kichina kalishalambwa na wenyewe.... Chezeya vibaka wa Keko Magurumbasi weye..............LOL
Kwani hujui uvumi ndio unapendwa sana hapa JF...?
Umeona hali ya barabara ya kuelekea Isimani ilivyo? Naogopa kuvuka nitagongwa na magari....LOL
Mamndenyi unakumbuka ile ya yule mtu aliyegeuka nyoka kule Buiguruni..?Mtambuzi si umnunulie tu kasimu ka tochi
au unataka ule hayo mema ya nchi peke yako.
Uzushi mwingine - majuzi tu wakasema kale katoto kamepewa dhamana bana, kweli bongo ni zaidi ya unavyoifahamu.
ngoja nimwambie shemeji mjeda aje akuvushe! bado una kamba mguuni kumbe! lol pole yake Mama Ngina
Ingawa nakubaliana na hayo maoni ya kwamba Watanzania wengi hawana kawaida ya kuchunguza au kujiuliza kuhusu mambo yawazungukayo, ila habari hii haijaweka wazi huo utafiti uliofanywa hivi karibuni umefanywa na nani na umefanyikia wapi.
Mamndenyi unakumbuka ile ya yule mtu aliyegeuka nyoka kule Buiguruni..?
Lile tukio sitalisahau maana nilivunjika hadi mkono pale Buguruni kituo cha Polisi kutokana na kusukumana tukitaka kumuona huyo Nyoka mtu.
Magazeti ya wakati ule likiwemo gazeti la MFANYAKAZI, walichora hadi picha ya nyoka mtu, mbona waliuza...!
Bwana eh, hebu niwache kwanza nijadili mambo ya uvumi...!
Vipi kuna Kahawa nije?
Utafiti uliofanywa hivi karibuni umeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo watu wake hupenda sana kuvumisha mambo na yakaonekana kama kweli. Pamoja na kuwa na vyombo vingi vya habari ambavyo vingasaidia kufafanua mambo, utafiti huo unasema, vyombo hivyo, navyo husaidia kuvumisha uongo na ukaonekana kuwa kweli.
Inaelezwa kwamba, wananchi wa Tanzania hawana kawaida ya kuchunguza au kujiuliza kuhusu mambo yanayowazunguka. Kila siku wanaamini wanakutana na jambo jipya hata kama liliwatokea jana na juzi. Ndio maana, matumizi ya wizi wa ulaghai (Utapeli) umekuwa ukifanikiwa sana.
Taarifa zinasema, nchini Tanzania mtu anaweza kuzusha jambo la kijinga na jambo hili likashika kasi na kufikia mahala ambapo hata mamlaka fulani zikaingilia kutaka kufanya utafiti au uchunguzi. Hata hivyo utafiti huo haukutoa mifano ya mambo ambayo yamekuwa yakizushwa hapa nchini na kuonekana kama kweli. Lakini huenda suala la mwanaume na mke wa mtu walionasiana guest wakati wakizini ni kati ya mambo hayo.
Lakini inaelezwa kwamba, huenda sababu ya watu kuwa wambea na wavumishaji ni kutokana na mfumo wa utoaji habari kwa umma kwa siku za nyuma. Magazeti na redio zilizokuwa zinaruhusiwa nchini zilikuwa ni za serikali peke yake. Wananchi walikosa nafasi ya kujua ukweli kuhusu mambo mengi yenye kuwazunguka, kwani mengine yangeweza kuikwaza serikali.
Kwa hiyo wananchi wakawa wanavumisha na kuzua pale jambo fulani dogo linapotokea mahali. Utamaduni huu umeendelea hadi sasa. Magazeti redio na televisheni zinadaiwa kwamba, nazo zimekuwa zikieneza umbea bila zenyewe kujua. Mwandishi anajua habar fulani ni uzushi, lakini kwa sababu anataka kuonekana amefuma habari nzuri, huupamba uvumi hadi unaonekana kama ni kweli.
Lakini katika mauvumi yote, nadhani ule wa jamaa kugeuka nyoka,kwa kumnanihii.... mke wa mtu, miaka michache iliyopita kule kipande cha Buguruni, utaendelea kushika chart ya "Rikodi za Guiness" maana maelfu ya watu ya watu walifurika kituo cha polisi Buguruni, na kila walipoambiwa huo ni uvumi, hakuna huyo nyoka-mtu wa kusadikika, hawakutaka kuamini, hadi wakaja kutawanywa na magari ya washa washa kutoka kwa wale vijana wa "Fanya Fujo Uone' kutoka ile kipande ya Ukonga!! Lakini yote hiyo inasababishwa na idle minds, wabongo wengi hawana shughuli za kuwakeep busy, kwa hiyo ubusy wao ni kuconcentrate na hayo mauvumi ya ooh... mara wamenatiana, ooh... mara kageuka chatu!! Kama Taifa linapaswa kuangalia namna ya kuwakeep busy wananchi wake, ili kuyapiga stop hayo mauvumi yasiyokuwa na kichwa wala miguu!!
umenikumbusha hizi stori
saa zingine nashangaa waTZ tunashindwaje kung'amua even the simplest of information kama ni ukweli au la.
- amina chifupa (RIP) kafufuka
- babu wa loliondo
- mtoto wa kanumba
- utata wa castor semenya
- freemason blah blah
- popobawa
- albino wanaleta utajiri
- etc
omba Mungu akunyime kila kitu kasoro umaskini wa akili -_-
Nyani Ngabu ilikuwa ni mwaka 1988 wakati huo ndio nilikuwa ni miongoni mwa walami wa pale Buguruni kwa Makukula.......Hivi ile ilikuwa ni 1987 au 1988?
Anyway kwa tukio hilo la Buguruni, naweza kusema, sina kumbukumbu nzuri sana, lilitokea mwaka gani, kwa wale wanaokumbuka vizuri, siyo vibaya, wakatujuza!!Hebu ngoja kwanza...hiyo ya jamaa kugeuka nyoka ilisababishwa na jamaa kutoka na mke wa mtu ama ilisababishwa na dawa ya penzi ambayo mkewe na huyo nyoka mtu alimwekea mumewe kwenye maji ya kuoga ndiyo jamaa akageuka chatu?
Halafu kwa kumbukumbu zangu, hiyo ilitokea miaka ya '87 au '88. Hiyo si miaka michache iliyopita. Ni miaka 26 au 25 iliyopita...hiyo ni miaka mingi.
Hebu ngoja kwanza...hiyo ya jamaa kugeuka nyoka ilisababishwa na jamaa kutoka na mke wa mtu ama ilisababishwa na dawa ya penzi ambayo mkewe na huyo nyoka mtu alimwekea mumewe kwenye maji ya kuoga ndiyo jamaa akageuka chatu?
Halafu kwa kumbukumbu zangu, hiyo ilitokea miaka ya '87 au '88. Hiyo si miaka michache iliyopita. Ni miaka 26 au 25 iliyopita...hiyo ni miaka mingi.