Kumbe tumbo ni kitu kibaya sana

Kumbe tumbo ni kitu kibaya sana

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,190
Agenda ya CHADEMA ya No reform No Election imepelekea baadhi ya wanachama wa CHADEMA kuelekea kuasi kwa sababu ya tumbo. Wengi wao wako pale kwa kutafuta masilahi na siyo vinginevyo. Agenda hii ilianzishwa na Mbowe mwenyewe leo hii mnamlaumu Lissu. Kumbe wengi hawapo pale kwa ajili ya Chama ila kwa ajili ya matumbo yao. Wanatia aibu sana.
 
Tumbo a.k.a stomach ni konyo, yani leo wale wale waliokua wanatuaminisha kuwa Chadema hawagawani vyeo na madaraka bali wanagawana majukumu leo hii wamegeuka? Safari bado ni ndefu sana
 
Haishangazi. Hata Yuda Iscariote alimsaliti Yesu kwa vipande vya fedha ila hakufanikiwa kutimiza lengo la waliomtuma
 
Agenda ya CHADEMA ya No reform No Election imepelekea baadhi ya wanachama wa CHADEMA kuelekea kuasi kwa sababu ya tumbo. Wengi wao wako pale kwa kutafuta masilahi na siyo vinginevyo. Agenda hii ilianzishwa na Mbowe mwenyewe leo hii mnamlaumu Lissu. Kumbe wengi hawapo pale kwa ajili ya Chama ila kwa ajili ya matumbo yao. Wanatia aibu sana.
Jamaa wanajidanganya sana, yaani dola na chama cha kijani wanaweza kukubali kupoteza majimbo/ubunge wakati nafasi za chini kabisa za wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji wamekwapau kwa kishindo.
 
Tumbo a.k.a stomach ni konyo, yani leo wale wale waliokua wanatuaminisha kuwa Chadema hawagawani vyeo na madaraka bali wanagawana majukumu leo hii wamegeuka? Safari bado ni ndefu sana
Mungu ameamua kuwaonyesha wazi,Ili kuondoa najisi kwenye kazi yake anayoifanya kupitia Tundu A.Lissu🇹🇿✝️
 
Hauwezi kuwa na akili timamu halafu ukafuatulia siasa labda uwe mwanasiasa unayenufaika moja kwa moja.
 
John Mrema hajawahi kufanya kazi nyingine yoyote popote zaidi ya chadema HQ . Huyu alikuwa mwandani w mbowe akibadilishiwa vyeo tu
Shida ya huyo jamaa ni hapo amekulia Chadema akila mshahara na akutegemea kama atatoka kule jikoni sasa amevurugwa
 
Sitatia neno maana huwa nikipinga jambo naishia kupewa matusi,Bora mmeanza kuona mapema
 
Agenda ya CHADEMA ya No reform No Election imepelekea baadhi ya wanachama wa CHADEMA kuelekea kuasi kwa sababu ya tumbo. Wengi wao wako pale kwa kutafuta masilahi na siyo vinginevyo. Agenda hii ilianzishwa na Mbowe mwenyewe leo hii mnamlaumu Lissu. Kumbe wengi hawapo pale kwa ajili ya Chama ila kwa ajili ya matumbo yao. Wanatia aibu sana.
Ni aibu mno. Nimeumia sana,kuona mijitu ipo tayari kupoteza Uhuru unaotafutwa wa kudumu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Njaa,njaa zimewafanya wanaanzisha kampeni za kipumbavu kupigania matumbo yao tu.

Kenyatta hakukosea kusema ni maiti hawataamka milele
 
John Mrema hajawahi kufanya kazi nyingine yoyote popote zaidi ya chadema HQ . Huyu alikuwa mwandani w mbowe akibadilishiwa vyeo tu
Mtu wa namna hii lazima tu awe na maumivu makali. Maana atalazimika sasa kuishi kwa jasho kama wengine, jambo ambalo inawezekana hakuwahi kulifikiria hata siku moja.
 
Back
Top Bottom