Kumbe TFF inafanana na CCM?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Hapo jana tumeshuhudia shirikisho la kandanda nchini kwetu likifanya uchaguzi wake huko mjini Dodoma na kupata viongozi wapya wataoliongoza shirikisho hilo la mpira wa miguu kwa kipindi kijacho.

Katika uchaguzi huo aliyeshinda nafasi ya Urais wa shirikisho hilo ni Wallace Karia na aliyeshinda nafasi ya Umakamu wa Rais ni Michael Wambura.

Kabla ya kufanyika uchaguzi huo kulikuwa na kila aina ya mizengwe, kama vile kuweka zuio mahakamani ili uchaguzi huo usifanyike, mizengwe mingine ni kumuwekea pingamizi mgombea wa nafasi ya Urais Wallace Karia kuwa siyo raia wa Tanzania.

Hatimaye Mahakama ilitupilia mbali mapingamizi hayo na kusema kuwa Wallace Maria ni raia halali wa nchi hii na uchaguzi uendelee kama ulivyopangwa na hapo jana ukafanyika na Wallace Karia akaibuka na ushindi wa kishindo kwa nafasi ya Urais.

Tukumbuke pia katika uchaguzi wa jana TAKUKURU walitanda katika kila kona ya Hoteli zote walizofikia wajumbe hao kuhakikisha hakuna rushwa yoyote inayotembezwa kwa wajumbe wa mkutano huo.

Ingawa TFF ni shirikisho la kandanda Tanzania na CCM ni chama cha siasa, lakini vyama hivyo viwili vinafanana sana kwa matendo yao.

Tunaijua CCM kuwa ni mabingwa wa kuendesha siasa za mizengwe za kuwasingizia baadhi ya wagombea ambao wanawaona tishio kwa kuwaita siyo raia na katika chaguzi zao zote rushwa huwa inatembea nje nje, jambo ambalo huwa linassbabisha wagombea ambao huwa wanapata uongozi siyo wale viongozi bora ambao wangepaswa kupita kwenye nafasi hizo, Bali huwa inatokana na ubora wa kutengeneza mizengwe na ubora wa kutembeza pesa ya rushwa kwa wagombea wa chama chao.

Kitu ambacho tumejifunza kutokana na uchaguzi wa jana wa TFF ni kuwa kumbe hata katika uchaguzi mkuu wa vyama vya siasa,iwapo TAKUKURU na vyombo vya dola vitaamua kufanya shughuli zao kwa weledi kutokana na taaluma yao, ni dhahiri kuwa vyama vya upinzani vitapata ushindi wa kishindo dhidi ya CCM!
 
Mwakalebera kapigiwa debe na Lumumba buku 7 na kaangukia pua naona Msigwa kampa laana
 
Tukumbuke pia Michael Wambura ameshawahi kugombea mara kadhaa kwenye nafasi za juu kwenye chaguzi zilizopita, lakini kutokana na mizengwe ya TFF jina lake lilikuwa likiishia kukatwa!

Kama ambavyo CCM wanavyowakata wabaya wao......

Refer issue ya Lowassa mwaka 2015......
 
Kuthibitisha kuhusu mizengwe ya TFF inavyofanana na CCM

Katika uchaguzi huu wa TFF walimzushia Wallace Karia kuwa siyo raia wa Tanzania bali ni Msomali!

Vivyo hivyo kwa CCM waliwahi kumzushia mbunge wa Nzega, Hussein Bashe kuwa siyo raia wa Tanzania bali ni raia wa Somalia!
 
Tatizo la TAKUKURU % kubwa ya viongozi wake ni wana-CCM, ni vigumu mbwa kumng'ata mwenye mbwa.
It is very true.

Wanakuwepo kwenye mikutano ya CCM na wanashuhudia rushwa ikitembezwa nje nje......

Lakini wanasubiri maelekezo toka juu kuwa wamkamate nani na wamwache nani!

Haya ni maajabu ya chombo chetu cha kupambana na rushwa ambapo wao rushwa yao ina macho.....
 
Mfumo mbovu sana
 
umesahau pia kuwa uchaguzi ulikuwa live TBCCM
 
Mwakalebera Dene na Lumumba buku 7 na kaangukia pia naona Msigwa kampa laana
It is true.

Makada wameangukia pua Jana....

Kwa kuwa mbinu zao za kiccm zimeshindwa kufua dafu jana .....
 
Ikitokea uchaguzi mkuu wa vyama vya siasa mwaka 2020 ukawa huru kama ulivyokuwa wa Kenya uliopita, hakika CCM itashindwa uchaguzi huo kirahisi sana.....

Ikiwa pia vyombo vya dola vitaamua kukaa pembeni na visijihusishe na mambo ya kisiasa, hakika huo ndiyo itakuwa mwisho wa CCM!
 
Ccm wamepigwa Kwa Raira Odinga na Odinga wa Tanzania mashavu yamemshuka Leo.na wakajipanga Kwa Mwakalebera nae kaangukia pua Mwakalebera alizaliwa kukataliwa tu akafuge mbwa auze
 
Ccm wamepigwa Kwa Raira Odinga na Odinga wa Tanzania mashavu yamemshuka Leo.na wakajipanga Kwa Mwakalebera nae kaangukia pua Mwakalebera alizaliwa kukataliwa tu akafuge mbwa auze
Yaani huyo Mwakalebela aliangukia pua ubunge Iringa mjini kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Hivi sasa napo kala mweleka kwenye uchaguzi wa TFF

Kilichobaki akaanzishe mradi wa kuuza ulanzi kwao Iringa......
 
Mwakalebera kapigiwa debe na Lumumba buku 7 na kaangukia pua naona Msigwa kampa laana
Yaani huyo Mwakalebela ni bora astaafu soka na siasa kwa ujumla wake.....

Siasa walimpiga chini kwenye ubunge Iringa mjini na mpira wa TFF nako kabwagwa vibaya sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…