Makamanda na Wana JF;
Ule Waraka uliosomwa mbele ya vyombo vya habari uko Dodoma na THOBIAS MWESIGA RICHARD
aliyekuwa anadai anausoma KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA ni "FAKE", JF imegundua.
Siku ya tarehe 19-11-2010 kijana Thobiasi Mwesiga Richard alisoma waraka aliodai ni "TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE".
Kijana Thobias aliyejibandika jina la 'Usomi" bila hata kuhitimu masomo yake ya shahada kumwezesha kuitwa msomi amedaiwa na viongozi wake wakuu kuwa anajipendekeza kwa wanasiasa ambao wengine ni watoto wa vigogo wakuu wa chama tawala ili aonekane kada mzuri kwa ajili ya maslahi yake binafsi.
Mwandishi wa Thread hii, leo akiwa katika mji wa Dodoma alifanikiwa kuonana na mmoja wa Viongozi wa St. Johns University na viongozi watano wa University of Dodoma ambao wote walikanusha vikali kuwa hawajawahi kuidhinisha kutoa tamko hilo na wala hawajawahi kukutana na kujadili jambo hilo ili litolewe tamko.
Leo, nikiwa katika shughuli zangu UDOM nilibahatika kukutana na viongozi wa juu wa Serikali ya wanafunzi wapatao watano na wote walikanusha vikali kuwa tamko lililotolewa hawalitambui kama wawakilishi halali wa wanafunzi na wala hawezi kujiingiza katika malumbano ya kisiasa bila sababu za msingi na bila kufuata utaratibu wa vikao husika.
Walishangazwa sana na tamko lililotolewa ambalo walikiri huenda ni kujipendekeza kwa mtoa tamko na kwamba Serikali ya Wanafunzi itakutana na kulifanyia kazi suala hili kabla hatua stahiki hazijachukuliwa.
Wote kwa pamoja walikiri kuwa tamko hilo waliliona katika magazeti na kuwa hakuna aliyemtuma Thobiasi wala hakuwa na baraka za wanafunzi. Thobiasi ambaye ni mwanafunzi wa kitivo cha sheria UDOM ambaye "Google Search" inaonyesha awali alichaguliwa kujiunga Tumaini University lakini akachakachua na kujiunga UDOM, inasemekena ni moja kati ya Mawaziri katika Chuo Kikuu cha Dodoma katika Serikali ya Wanafunzi.
My Take:
Natoa wito kwa viongozi wa wanafunzi, kufanya mambo yao kwa kuzingatia utaratibu waliojiwekea badala ya kufanya mambo wao binafsi na kudai kuwa ni mawazo ya wote. Kufanya hivyo ni kuwadhalilisha wanafunzi ambao katika suala husika lilotolewa tamko limeligawa taifa wakiwepo wanafunzi wenyewe ambao ni wapenzi wa vyama na itikadi mbalimbali.
QED