Kumbe Tamko La "Wasomi" Ni Fake

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,698
1,250
Makamanda na Wana JF;

Ule Waraka uliosomwa mbele ya vyombo vya habari uko Dodoma na THOBIAS MWESIGA RICHARD
aliyekuwa anadai anausoma KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA ni "FAKE", JF imegundua.

Siku ya tarehe 19-11-2010 kijana Thobiasi Mwesiga Richard alisoma waraka aliodai ni "TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE".

Kijana Thobias aliyejibandika jina la 'Usomi" bila hata kuhitimu masomo yake ya shahada kumwezesha kuitwa msomi amedaiwa na viongozi wake wakuu kuwa anajipendekeza kwa wanasiasa ambao wengine ni watoto wa vigogo wakuu wa chama tawala ili aonekane kada mzuri kwa ajili ya maslahi yake binafsi.

Mwandishi wa Thread hii, leo akiwa katika mji wa Dodoma alifanikiwa kuonana na mmoja wa Viongozi wa St. Johns University na viongozi watano wa University of Dodoma ambao wote walikanusha vikali kuwa hawajawahi kuidhinisha kutoa tamko hilo na wala hawajawahi kukutana na kujadili jambo hilo ili litolewe tamko.

Leo, nikiwa katika shughuli zangu UDOM nilibahatika kukutana na viongozi wa juu wa Serikali ya wanafunzi wapatao watano na wote walikanusha vikali kuwa tamko lililotolewa hawalitambui kama wawakilishi halali wa wanafunzi na wala hawezi kujiingiza katika malumbano ya kisiasa bila sababu za msingi na bila kufuata utaratibu wa vikao husika.

Walishangazwa sana na tamko lililotolewa ambalo walikiri huenda ni kujipendekeza kwa mtoa tamko na kwamba Serikali ya Wanafunzi itakutana na kulifanyia kazi suala hili kabla hatua stahiki hazijachukuliwa.

Wote kwa pamoja walikiri kuwa tamko hilo waliliona katika magazeti na kuwa hakuna aliyemtuma Thobiasi wala hakuwa na baraka za wanafunzi. Thobiasi ambaye ni mwanafunzi wa kitivo cha sheria UDOM ambaye "Google Search" inaonyesha awali alichaguliwa kujiunga Tumaini University lakini akachakachua na kujiunga UDOM, inasemekena ni moja kati ya Mawaziri katika Chuo Kikuu cha Dodoma katika Serikali ya Wanafunzi.

My Take:

Natoa wito kwa viongozi wa wanafunzi, kufanya mambo yao kwa kuzingatia utaratibu waliojiwekea badala ya kufanya mambo wao binafsi na kudai kuwa ni mawazo ya wote. Kufanya hivyo ni kuwadhalilisha wanafunzi ambao katika suala husika lilotolewa tamko limeligawa taifa wakiwepo wanafunzi wenyewe ambao ni wapenzi wa vyama na itikadi mbalimbali.

QED
 

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,704
2,000
Well done Super Man, huyu kadogoo alitutoa jasho saana. Inabidi wenzake wamwajibishe na hizo taarifa tuzipate. Sio mtu anakurupuka na kufanya mambo yake anadharirisha taaluma na usomi, kumbe ni fake.

Atulie amalize hayo masomo kwanza kabla ya kudandia ufisadi.
 

Big Lady

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
548
195
Hii ndiyo Tanzania zaidi ya uijuavyo.Kila mwenye namna anataka afanye mambo anavyotaka yeye na si matakwa ya wengi yanavyotaka. Kazi kweli kweli. Tunawasubiri kwenye system wakimaliza chuo waone maisha halisi.
 

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,698
1,250
Well done Super Man, huyu kadogoo alitutoa jasho saana. Inabidi wenzake wamwajibishe na hizo taarifa tuzipate. Sio mtu anakurupuka na kufanya mambo yake anadharirisha taaluma na usomi, kumbe ni fake.

Atulie amalize hayo masomo kwanza kabla ya kudandia ufisadi.

Mkuu tupo pamoja.

Mimi nilipoonana na hawa vijana ambao kwa kweli walikuwa makini sana, niliwauliza imekuwa vipi kuhusu "Tamko" lao na limepokelewa vipi? Hakika walieleza masikitiko yao makubwa kuhusu huyu bwana. wamenieleza kuwa huenda wakatoa tamko kukanusha kuwa lile halikuwa tamko lao.

Na wala kwa sasa hawna forum yoyote rasmi inayowaunganisha wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma.
 

Njilembera

JF-Expert Member
May 10, 2008
1,479
2,000
Hii inatisha! Anaanza kuchakachua hata kabla hajamaliza shule! Inabidi ashughulikiwe mapema ili asije akapotea njia huyu mtoto. UDOM wanapaswa wamtafute wampe ushauri nasaha, tumkunje ingali yu bichi
 

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,698
1,250
Hii ndiyo Tanzania zaidi ya uijuavyo.Kila mwenye namna anataka afanye mambo anavyotaka yeye na si matakwa ya wengi yanavyotaka. Kazi kweli kweli. Tunawasubiri kwenye system wakimaliza chuo waone maisha halisi.

Hakika usemayo ni kweli BL. lakini ni vema Watanzania sasa tuanze kubadilika. Naamini kila mtu kwa wakati wake anaweza kufanya sehemu yake. Huyu bwana mdogo Thobias "amechakachua" mchana kweupe. Kwa kweli si uungwana.
 

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,698
1,250
Hii inatisha! Anaanza kuchakachua hata kabla hajamaliza shule! Inabidi ashughulikiwe mapema ili asije akapotea njia huyu mtoto. UDOM wanapaswa wamtafute wampe ushauri nasaha, tumkunje ingali yu bichi

Mkuu, tuone hao viongozi wakuu ambao ni madingi wake watafanya nini.
 

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
UDOM hakuna the invisible Mzee Punch ...... na sijui mzee siku hizi yupo wapi....... makunji nayo yamepungua .... ndio maana kadogoo anatesa.... mzee atumiwe sms arudi .... tena aanzie hapa JF
 

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,966
2,000
Jamani kuna yeyote humu anaweza akaniletea huyo mtoto aliyeandaa huo waraka?
Nina mazungumzo naye.
 

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,698
1,250
UDOM hakuna the invisible Mzee Punch ...... na sijui mzee siku hizi yupo wapi....... makunji nayo yamepungua .... ndio maana kadogoo anatesa.... mzee atumiwe sms arudi .... tena aanzie hapa JF


Mzee Punch angekuwepo asingethubutu . . . .

Kuna binti tulikuwa nae UDSM somebody @sh@ ambaye aliendekeza sana masuala ya ngQnQ. Ingawa sikuunga mkno lakini Mzee Punch alimuumbua sana. Kisha baba yake akatumiwa cheti cha kufuzu masomo ya ngQnQ chenye sahihi ya makamu mkuu wa chuo. Mzee libidi aje UDSM kumhoji makamu mkuu wa chuo iweje binti kafuzu masomo tena katika fani ambayo siyo iliyompeleka kusomea?

Sasa huyu dogo, tumfunze tu kwamba maisha hayaendi hivyo.
 

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
Mzee Punch alikua ana nguvu kubwa na ilikua ni system ya kutengeneza discpline ndani ya chuo ili unapohitimu uje mtaani msafi.... sasa Mzee sijui yuko wapi jamani au kina Ch ng wameshampa visenti
 

Sisimizi

JF-Expert Member
Nov 10, 2009
495
195
Uongozi halali wa UDOM ukanushe kwa maandishi. Hatutaki geresha geresha hapa!!! Bado wanawajibika kuweka suala hili kinagaubaga.
 

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,704
2,000
Well done Ndg yangu Supper Man hawa vijana wanahitaji elimu ya maisha halisi.Maana wanaanza kujikomba kwa hao mafisadi. Huo si mwelekeo mzuri wakanywe!

What you get by reaching your destination is not nearly as important as what you will become by reaching your destination. Zig Ziglar.
 

October

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
2,145
1,195
UDOM hakuna the invisible Mzee Punch ...... na sijui mzee siku hizi yupo wapi....... makunji nayo yamepungua .... ndio maana kadogoo anatesa.... mzee atumiwe sms arudi .... tena aanzie hapa JF

Mzee PUNCH ali-DISCO.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom