Kumbe soka letu bado | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe soka letu bado

Discussion in 'Sports' started by idumu, Jun 15, 2009.

 1. idumu

  idumu Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani Watz waache majigambo, Maana kuifunga new zealand tulioongea mno na TV zetu, na viredio vyetu. Jana wameangamazi 5 bila na SPAIN, Tujipime na timu za Afrika zilizo bora ili kujua kiwango chetu.

  Badooooooooo!!
   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  new zealand ni washindi wa oceania na bado kiwango chao sio kibaya hata kama tuliwafunga.mbona new zealand hao hao walifungwa kwa taabu sana na italy kwenye mechi ya kirafiki 4-3? spain moto mkubwa usifanye nao mchezo,ndio wako namba moja duniani mtu yoyote ukiingia vibaya pale unakula dozi.kwahio soka la tanzania limekuwa kwa kiasi flani na sio mbaya kujipima na timu kama hile.tuache kulinganisha mambo kiajabu ajabu.hata tukipewa mechi ya kirafiki na england sio mbaya , haina haja kucheza na waafrika wenzetu kila wakati kama unavyosema.kuna njia nyingi za kujifunza na kuna vitu vingi vya kujifunza.
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Sema na sisi tuliongea saana kuhusu ule ushindi!! Maximo alishangilia hadi akateguka mguu wakati hata kombe la challenge hajawahi kuchukua! Tumeharibu mpira wetu tumeingiza siasa ndani yake, mie nakwambia.
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hakika timu ya Tz ni bora na inahitaji timu timu za viwango kama hizo ili kupandisha kiwango chetu.

  Kucheza na timu kama hizo tunapata faida ifuatavyo
  1.kuwaondoa vijana uoga wachezaji wetu na kujenga kujiamini
  2.kuitangaza tz katika soka za kimataifa
  3. kuongeza rank katika fifa
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu mpira haufuati commutative au assiciative property za kwenye hesabu yaani; If A=B, and B=C, then A=C! No it doesn't work like that......! Sisi kumfunga Newzland na yeye kufungwa na Spain si lazima ati sisi tunaweza fungwa au kuifunga Spain automactically!

  Mpira huwa unadunda mkubwa...hukumbuki worldcup 2002 Senegal walivyoiharibia France?
   
Loading...