Vijijini Lawama
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 298
- 73
Kuna kitu cha kushangaza katika ilan ya uchaguzi ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
katika sura ya nane MAENEO MENGINE MUHIMU Demokrasia na maendeleo katika eneo linalosomeka "chama chamapinduzi na Muungano".
katika kifungu cha 141 kinasomeka hivi "Chama Cha Mapinduzi kimekuwa muhimili wa Muungano tangu vyama vya TANU na Afro viungane tarehe 5 Februari 1977. Muundo wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni muungano wenye serikali mbili, Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar"
My take: hivi tujiulize je ni kweli serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni ni muungano wenye serikali mbili, serikali ya muungano wa Tanzania na serikali ya Zanzibar? ndg wanajamvi naomba kufafanuliwa huu muungano wa Tanzania ulitokana na nchi zipi tena zilizoteengeneza huu muungano? Je kuna nchi zaidi ya mbili zinazotengeneza Jamhuri ya muungano ya Tanzania?
hili lichama halian tofauti na panga butu, kenye kutu kuingizwa theatre ili Daktari wa upasuaji alitumie mkata mgonjwa .
Kuna kitu cha kushangaza katika ilan ya uchaguzi ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
katika sura ya nane MAENEO MENGINE MUHIMU Demokrasia na maendeleo katika eneo linalosomeka "chama chamapinduzi na Muungano".
katika kifungu cha 141 kinasomeka hivi "Chama Cha Mapinduzi kimekuwa muhimili wa Muungano tangu vyama vya TANU na Afro viungane tarehe 5 Februari 1977. Muundo wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni muungano wenye serikali mbili, Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar"
My take: hivi tujiulize je ni kweli serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni ni muungano wenye serikali mbili, serikali ya muungano wa Tanzania na serikali ya Zanzibar? ndg wanajamvi naomba kufafanuliwa huu muungano wa Tanzania ulitokana na nchi zipi tena zilizoteengeneza huu muungano? Je kuna nchi zaidi ya mbili zinazotengeneza Jamhuri ya muungano ya Tanzania?
Kijana hata kama unichukia sana CCM (nami naichukia) usiwe mvivu wa kusoma na kuelewa mantiki ya maneno yalitotumiwa.
Imesema "ni muungano wenye serikali mbili"; haijasema "ni muungano unaotokana na serikali mbili".
Na kwa kuwa muktadha ni muundo wa Jamhuri ya Muungano, ni kitu kilicho cha kweli kuwa ndani ya Jamhuri ya Muungano utakuta Serikali ya Jamhuri ya Muungano w Tanzania na Serikali ya Zanzibar.
Tatizo lako (na la hao wengine wenye kukuunga mkono lakini "wavivu" wa kusoma) liko wapi katika kuelewa?