Sisemi kwamba house girls hawana haki ya kupenda au kupendwa. Ila ukweli mchungu ni kwamba wadada wa kazi wengi wanajikuta kwenye mahusiano na watoto wa kiume na mababa wenye nyumba sio kwa kupenda, wengi hawapendi ila wanajikuta tu wanakubali ili kulinda "vibarua vyao". Mdada hajiwezi, na anawaza je nikikataa nikafukuzwa, ntafanyaje na haya maisha.
Afu hawa wadada wa kazi ni kama watoto wa familia husika, mkatongozage huko nje jamani. Familia nyingine ptuuu, ndo madomo zege au kuonea tu mabinti za watu? Huwa mnakuwaga na nia za kuwaoa kweli, au kusuuza tu mirungu yenu. Hawa hata wakisema huyu mdada afukuzwe, akija mdada mwingine watamtongoza tu kama kawaida yao. Solution ni wao wenyewe kuanza kujiheshimu na kuwaheshimu hao madada. Muwe na aibu, muwe na Utu