Kumbe michango bado ipo shule za serikali!

Mkwere Sumbawanga

JF-Expert Member
Sep 28, 2015
744
660
Habari Wana JF
Katika Joining Instructions za form five naona michango kama vile ya madawati bado ipo, hivi hadi awamu hii ya 5 bado ipo mm nlijua imeisha.

Kwa mfano Jangwani Sekondari, Michango mingine ya shule inayotakiwa kulipiwa ni
1.Tsh. 10,000/- kwa ajili ya taaluma
2.Tsh 15,000/- kwa ajili ya dawati
3.Tsh. 10,000/- kwa ajili ya tahadhari
4.Tsh. 15,000/- kwa ajili ya ulinzi
5.Tsh. 15,000/- kwa ajili ya usafi

Unaweza pitia attachment ya mifano ya joining instructions za baadhi ya shule hapa chini
 
Attachments

  • JANGWANI.pdf
    3.8 MB · Views: 125
  • KIFARU.pdf
    178.7 KB · Views: 130
  • ILBORU.pdf
    1.8 MB · Views: 87
  • KISIMIRI.pdf
    1.3 MB · Views: 124
Michango imeondolewa Elimu msingi tu kwa sekondari inaendelea. Elimu msingi inaishia kidato cha NNE. Kuanzia kidato cha tano hadi cha sita ni sekondari. Shule ulizotaji zinatoa Elimu ya sekondari, tuna imani hapo mbeleni serikali itafuta na kwa ngazi ya sekondari
 
Mkuu michango imeondolewa kwa wanafunzi wa kuanzia chekechea hadi kidato cha nne tu. Waliobaki wataendelea kulipa michango kama ilivyokuwa miaka iliyopita.Chakuangalia ni kuwa wakuu wa shule wasio waaminifu wanaweza kuongeza michango kwa wanafunzi wa vidato vya V na VI ili kufidia michango iliyofutwa na serikali.
 
asante mkuu nimekupata vizuri
 
hapo sawa
 
Back
Top Bottom