Kumbe Mheshimiwa Raisi yuko Malawi kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Mheshimiwa Raisi yuko Malawi kweli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakati, Apr 22, 2012.

 1. Kakati

  Kakati Senior Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  MICHUZI: Rais Kikwete amewasili mjini Blantyre ,Malawi leo jioni kuhudhuria Mazishi ya Rais wa Malawi,Profesa Bingu wa Mutharika

  [h=3]Rais Kikwete amewasili mjini Blantyre ,Malawi leo jioni kuhudhuria Mazishi ya Rais wa Malawi,Profesa Bingu wa Mutharika[/h] Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Blantyre ,Malawi leo jioni kuhushuria Mazishi ya Profesa Bingu wa Mutharika, aliyekuwa Rais wa Malawi., aliyefariki tarehe 5 April, 2012 Kufuatia matatizo ya MoyoRais Kikwete ni miongoni mwa Viongozi wakuu Saba kutoka nchi jirani na Malawi.Nchi hizo ni Afrika Kusini, Benin, Kenya, Msumbiji, Zimbabwe na Zambia.Wakati huohuo Ikulu inapenda kukanusha taarifa zilizonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kudai kuwa Rais ametofautiana na Waziri Mkuu kuhusu aina ya hatua za kuwachukulia Mawaziri wanaotuhumiwa na ubadhirifu katika Wizara zao.Napenda kueleza Umma kuwa taarifa hizo si za kweli.Pia nitumie nafasi hii kuwatahadharisha waandishi wa habari kuwa makini, waangalifu na wachambuzi wakati wa kupokea, kusikiliza na kuandika au kutangaza taarifa wanazopata.Rais kikwete aliwasili kutoka Brazil alipokuwa amekwenda Kwa Ziara ya kikazi ya siku tano tarehe 21 April, 2012.Kwa hivyo basi Rais hajapata taarifa yeyote rasmi kutoka kwa Waziri Mkuu, na bado anasubiri kupewa taarifa hyo rasmi Kwa vile suala la tuhuma hizo limetokea Bungeni.Na kama kuna Waziri ambaye ameandika barua ya kujiuzulu, basi atakua amemuandikia Rais na kama zipo Rais ndiye atakaye zipokea na kuamua hatua inayofuatia.Kwa hivyo sio busara hata kidogo kwa vyombo vya habari kueneza uongo na fitna zenye lengo la kuchonganisha si viongozi tu , bali hata viongozi na wananchi kwa ujumla.Rais Kikwete anatarajia kurejea nchini kesho tarehe 23 April mara baada ya maziko..............................Mwisho ..................
   
 2. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Huyo ndio ****** bwana
   
 3. franktemu123

  franktemu123 JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 775
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 80
  Hivi najiuliza huyu VASCO DA GAMA ni lazima kila safari ya nje aende yeye? MAKAMU WAKE anafanya nini? Waziri wa Mambo ya Nje kazi yake nini? MALAWI ni majirani but hatupo close kiviile kama zilivyo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi(member wa EAC) hata MUTHARIKA hakuwa mtalii kama Mkuu sasa hii courage hii ya kuhudhuria kila tukio anapata wapi...nnavomfahamu mkulu lazima ahudhurie pia OLYMPICS 2012. kufanya kazi na Mkulu ni kaazi kweli kweli labda uwe mzee wa Dar es Salaam ndo mtaelewana.
   
 4. simaye

  simaye JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nashindwa kabisa kuelewa huyu rais wa tanzania anasafiri sana huyu jamaa. Katika hali ambayo si ya kawaida , katika hali hii ambayo nchi iko katika hali ngumu kiuchumi na wananchi wengi wanalalama maisha magumu bado tunaona Rais anakuwa na safari nyingi ambazo najua kwa namna yoyote fedha nyingi zinatumika.Safari anazofanya Kikwete usema kweli zinaliumiza Taifa sana pamoja na wananchi.Hivi wanauchumi hawalioni hili wakamshauri nchi kama Marekani tunasikia waziri wa mambo ya nje ndiye anasafiri sana Tanzania naona hakuna utaratibu yani Rais na viongozi wengine wanajisikia tuu kusafiri na ndiyo maana matumizi ya kawaida ni makubwa zaidi kuliko matumizi ya maendeleo.Huyu jamaa mpaka 2015 atakuwa ameiacha nchi mifupa mitupu
   
Loading...