Kumbe mgao wa umeme ni Tamthilia ?

Kumbe mgao wa umeme ni Tamthilia ?

uporoto01

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
4,698
Reaction score
1,429
Jamani mbona mgao ni kama haupo tena baada ya wabunge wa CCM kugeuka wapinzani hapa juzi kati.

Kumbe wakitaka wanaweza kulimaliza tatizo.
 
Mkuu uporoto01, hivi ulikuwa unafikiri mgawo huo ulikuwa wa ukweli? kwa taarifa fupi, ni mgongano wa kimaslahi kwenye dili za hiyo wizara.

Saizi wakubwa wamekaa wameyatatua mambo baada ya hali kuendelea kuwa mbaya.
 
Kama mwendo utakuwa hivi, nadhani Ngeleja akirudi tena kuwasilisha bajeti ya Wizara yake hakutakuwa na matatizo.
 
Kuna mzee mnoko mtaani kwetu baada ya umeme kutokatwa siku kadhaa kawapigia Tanesco eti wamesahau kukata jibu alilopewa 'acha tabia za shangazi yako' hahaha! sidhani kama atawapigia tena.
 
Iko siku wataacha kugawana majasho ya Watanzania. Siku ipo na inakuja na PATACHIMBIKA hakika.
 
Hali ya umeme ni tata kaka, mitambo inayotumika alinunu nyerere!yaani wamejitahidi ili bajeti ya nishati ya madini iishe mambo yaanza, ka huamini subiri uone!ni kiini macho ndugu zangu!
 
Kama mwendo utakuwa hivi, nadhani Ngeleja akirudi tena kuwasilisha bajeti ya Wizara yake hakutakuwa na matatizo.

Yaani wakilogwa waipitishe bajeti yake.. huo mgao utakaofuatia haujawahi kuonekana.. jiulize mbona wakati wa kampeni mwaka jana umeme haukukatika hata siku moja eti leo maji yamekauka ghafla.....
 
Back
Top Bottom