Kumbe Magari Ya Dar Yote Ni Ya Kaskazini?

Kumbe Magari Ya Dar Yote Ni Ya Kaskazini?

Juuchini

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2018
Posts
1,968
Reaction score
2,832
By Daniel Mjema na Jesse Mikofu,
dmjema@mwananchi.co.tz
Moshi/Mwanza. Ile adha ya foleni za magari iliyokuwa katika Jiji la Dar es Salaam imehamia Moshi.
Msongamano mkubwa wa magari uliojitokeza kwa saa sita mfululizo juzi hadi saa tatu usiku ni hali ambayo haijazoeleka kwa watumiaji wengi wa barabara mjini Moshi ambao walilazimika kutumia muda mrefu kutoka eneo moja kwenda lingine.
Dalili za msongamano zilianza kujitokeza tangu juzi asubuhi na ilipofika saa 10 alasiri, hali hiyo ilijidhihirisha hasa katika ni barabara kuu ya Njiapanda ya Himo hadi Mailisita na barabara za katikati ya mji kwenye masoko na maduka makubwa huku magari yakikosa maeneo ya maegesho katikati ya mji.
Mkurugenzi wa Moshi Hugos Garden, Bosco Simba alisema msongamano wa magari haukuwa jambo la kawaida na ilimchukua muda mrefu kufika nyumbani.
“Huwa natoka hapa Hugos hadi nyumbani pale Mjohoroni sanasana natumia dakika 10 lakini jana (juzi) usiku nilitoka hapo mzunguko wa YMCA hadi nyumbani nikatumia dakika 60,” alisema.
Dereva wa magari ya kusafirisha watalii, Haji Sadiki alisema msongamano ulioshuhudiwa juzi usiku ulikuwa si wa kawaida.
Wakati Moshi wakilia na wingi wa magari, Mwanza hali ni tofauti. Jiji hilo limeelezwa kuwa na idadi kubwa ya watu.
“Unajua kwenye sikukuu kila mmoja anataka ale na kuvaa vizuri zaidi ya siku nyingine na huduma hizi nyingi zipo mjini hivyo hilo linachangia kuongezeka kwa watu wakati wa kipindi hiki,” alisema Faustine Grervaz mkazi wa Nyegezi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna alisema jana kwamba ameshuhudia wingi huo wa watu tofauti na alivyozoea.
“Hata mimi nimezunguka maeneo mbalimbali jana (juzi) leo (jana), nimeshuhudia kuwapo kwa watu wengi. Mwaka jana sikuwapo lakini hata askari wangu wameniambia kuwa watu ni wengi kuliko wa mwaka jana,” alisema Shanna.
Source Mwananchi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maelezo hayo ndio ukaja na conclusion kuwa magari ya Dar yote ni ya kaskazini??.....kazi kweli kweli
 
Mkoa wa Kilimanjaro nadhani unaongoza kwa kuwa na watu wengi wanaomiliki magari.
Ukianzaia Same ,Mwanga, ROMBO ,Moshi mjini, Moshi vijijini ,Mapaka Hai. Ukifanya sensa ya watu wa mkoa huo wanaomiliki magari basi ni wazi kuwa magari mkoa huo ni mangi kuliko mikoa Yote.
Na hii haina ubisi wala sio siasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo Mimi hata kwenye miji kama dar mz mby magar mengi ni ya watu wa k'njaro
 
Hapana, si kweli..
1. Wapo waliokodi Magari kwenda nayo Moshi toka nje ya Dar
2. Wapo walioazima magari kwenda nayo huko toka nje ya Dar
3. Wapo waliotoka nje ya Dar eg. Mbeya, Mtwara, Mwanza, Nairobi etc na magari yao
4. Wapo wenye magari yao toka Dar (hawa nadhani ndo uliwadhamiria)
5. Wapo wanaoishi Moshi huko huko, wajaji wameongezea magari
6. Wapo wanaotengeneza magari yao Disemba tu huko Moshi ili mnaokwenda Moshi mkute nao wanayo

Hivyo basi, kujaa kwa magari ya Moshi si yote yanatoka Dar
 
Mkoa wa Kilimanjaro nadhani unaongoza kwa kuwa na watu wengi wanaomiliki magari.
Ukianzaia Same ,Mwanga, ROMBO ,Moshi mjini, Moshi vijijini ,Mapaka Hai. Ukifanya sensa ya watu wa mkoa huo wanaomiliki magari basi ni wazi kuwa magari mkoa huo ni mangi kuliko mikoa Yote.
Na hii haina ubisi wala sio siasa!

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE
Takwimu hizi ulizotoa umezipata mamlaka ipi mkuu?
 
Nimepita ubungo nimetokea Tazara, foleni kama kawaida kuanzia mataa ya Tazara (ukiondoa barabara ya Pugu road ambapo gari zinapita juu ya flyover) Buguruni, Tabata mpaka Ubungo.
 
Back
Top Bottom