Kumbe mabadiliko wanayonadi UKAWA ni...

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,506
Reaction score
123,817
Inasikitisha sana.

Si muda mrefu uliopita ilikuwa ni kawaida kusoma humu JF na kusikia kauli za "ukombozi" kutoka kwa baadhi ya watu.

Mimi, kupitia hii hii JF nikasema hiyo ni kauli aliyoitumia Luther alipokuwa anajitenga na RC.

Haikupita muda Mkapa akawapa dozi live pale Jangwani, wale wote wanaosema "ukombozi" kwa kauli ya Mkapa alisema ni "wapumbavu na malofa".

Dozi hiyo ya Mkapa imewaingia vizuri sana na toka siku hiyo sijaliona hilo neno au kama nimeliona tena basi ni mara moja au mbili kwa wale ambao dozi haijawaingia vizuri.

Haikupita muda nikamsikia kwenye video, kupitia hapa hapa JF, Lowassa akiongea kanisa la kilutheri akisema wamchaguwe kwa kuwa yeye ni Mlutheri na hakuna Mlutheri aliyewahi kuwa Rais kwa hiyo sasa ni zamu yao.

Kwa hayo, sasa nnaamini "mabadiliko" wayatakayo UKIWA ndio hayo ya kutaka dhehebu fulani na watu wa kanda ndiyo watawale.

Kwa sababu nimewasoma sana humu JF, wao wanasema wanataka mabadiliko tu, ukiwauliza "ya nini hayo mabadiliko" hawasemi! Jibu lao ni "sisi tunataka mabadiliko tu"!

Magufuli ananadi mabadiliko na anaeleza hayo mabadiliko yatakuwa yepi.

Ukweli ni kuwa hawa wote wanaobwabwaja mabadiliko domo linakuwa zege inapokuja kusema mbele za watu ni mabadiliko yepi wayatakayo na sababu ni hiyo, wanataka mabadiliko ya dhehebu na ukanda. Hata Lowassa alipolisema hilo aliwafukuza waandishi wa habari kanisani akabaki na Walutheri wenzake tu.

Watanzania tusiwasikilize hawa hata kidogo, hiyo agenda yao ya udini na ukanda waliifanya siri lakini Mwenyeezi Mungu hamfichi mnafik, Lowassa alidhani anaongea siri na Walutheri wenzake, kumbe kuna mtu amemrekodi, ni hatari sana.

Tazama list ya ukawa inayoongozana na Lowassa. Wote Walutheri na wote wa Kaskazini; Lowassa, Mbowe, Sumaye, Mbatia.

Nnamuombea salama tu yule mtu aliye mrekodi Lowassa, maana watu wakifikia kiasi hicho wanakuwa ni hatari sana.

Hawa watu ni hatari sana tena sana na ni wabaguzi wa hali ya juu. Tuhakikishe hawapati kura za kila mwenye kujitambuwa.

#HapaKaziTu
 
UKAWA pamoja na kuwa ni muunganiko wa vyama vinne lakini havina ajenda ya Pamoja.

Ni kama wamekurupushwa, wakati uchaguzi ni maandalizi ya miaka mitano baada ya uchaguzi mwingine.

Tulitegemea huu muungano ungekua na hoja za msingi za kukitikisa ccm, lakini hawajafika hata nusu ya uwezo wa Chadema 2010.

Zaidi wanachotegemea ni mafuriko (ya kutengeneza)na ccm kuchokwa na wananchi.
 
mnafik,-mnafiki
wakutheri-walutheri
yyatakuwa-yatakuwa
kawwaida-kawaida
Hii inaonyesha kiasi gani ccm mmepaniki sasa mbona mnahangaika na mambo ya #UKAWA kuliko ya ccm?
TANZANIA MPYA INAKUJA CHINI RAISI MTARAJIWA EDWARD LOWASA KIPENZI CHA WATANZANIA.
 

Hahahah eti na ww unajitambua na lukuvi kipind cha katiba mpya huko makanisani alikuwa anahubiri nn kuhusu uislam mtabadilika kama kinyonga kwa kila propaganda saiv watu nta zimenasa masikioni wao ni lowasa tu hasa malofa na malofa ndo wengi kweli tofaut na nyie mnaojitambua lazima mjutie kwa uamuz wenu wa kujipendelea werevu ghalika hilo werevu na malofa kuanzia mwez wa 11 tutakuwa ktk gurudumu moja noma sna
 
^^^M^^^A^^^G^^^U^^^F^^^U^^^L^^ ^I^^^^©2015 Ven conmingo si quieres vivir °°°°°°°°°°°°
°°°°°°°°°°° magufuli si la presidente en la
Tanzaniano.
Grac-ous..... >^^^^^>>>^^^^^>>^^^^^>>>^^^^^^
>>>>>^^^^^^
#HaPaKaZiTu
Imejipost
 
Interesting mwaka huu FaizaFoxy na Dr Slaa na Mwanakijiji wote team moja wanaiponda CHADEMA..

mwaka huu una mengi ya ajabu
Lowassa na Mnyika marafiki
Lowassa na kubenea marafiki
Lowassa na tundu Lissu marafiki
Tundu Lissu na Slaa maadui
Mbowe na Josephine maadui
Lipumba na Seif maadui
Slaa na Mwakyembe marafiki
Slaa na TISS marafiki..
Gwajima na Slaa maadui
 
Last edited by a moderator:
kawwaida-kawaida
Hii inaonyesha kiasi gani ccm mmepaniki sasa mbona mnahangaika na mambo ya #UKAWA kuliko ya ccm?
TANZANIA MPYA INAKUJA CHINI RAISI MTARAJIWA EDWARD LOWASA KIPENZI CHA WATANZANIA.

Mambo yanayohusu kuligawa taifa inabidi tuyakemee kwa nguvu zote na kuyalaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…