Kumbe, kupaki Bodaboda kijiweni lazima utoe malipo?

Kumbe, kupaki Bodaboda kijiweni lazima utoe malipo?

wakunyonya

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2024
Posts
858
Reaction score
2,058
Aise! Maisha siyo lelemama! Katika pitapita zangu kwenye mitandao ya kijamii nikakutana na mijadala ya bei za kupaki bodaboda katika vijiwe mbalimbali, kwa Dar na mikoani.

Kilichonishangaza, mfano kwa Dar, vijiwe vingi kuanzia Laki Tano na kuendelea. Ili upake boda yako kijiweni, mfano stendi ya Magufuli nasikia ni Laki Nane (800K), Ubungo Terminal Milioni moja na Laki Tano (1.5m), Kimara Terminal Laki Tano (500K), na hapo unaambiwa nafasi zimejaa, hivyo usubiri mpaka mtu atoke.

Baadhi ya wadau wakauliza: “Hizo hela hupelekwa wapi?” Majibu ni kuwa hupelekwa katika halmashauri husika. Nikajiuliza, hawa madogo wanaoingia boda za mkataba wanatoboa vipi kwa milolongo:
  • Pesa ya Boss
  • Leseni
  • Latra
  • Kijiwe
Kwa kujihakikishia, nikamcheki boda mmoja hivi ninayemjua, kumuulizia akaniambia: “Ni kweli, yeye kijiweni kwake kiingilio ni Laki sita (600K).
 
Boda wa town wanaingiza hela sana, ni vile ni matumizi yanaenda kwenye mambo yasiyo ya msingi. Moja ya kazi zenye risk kubwa sana.
Hata kama, lakn vp Kwa madogo wanao Anza kujitafuta maana nilijua huku ndio kimbilio la kuaza kujitafuta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom